Kushabikia Polisi kuua watuhumiwa, ni ujinga uliopitiliza

Kushabikia Polisi kuua watuhumiwa, ni ujinga uliopitiliza

Hizi IQ zetu za kula tunda kimasikhara ndio zinazotutesa.
Unamkamata kibaka unampeleka Mahamani ikibainika kuwa ameua sheria inaamuru anyongwe.
Sasa tusipofuata sheria tulizojiwekea na kuamua tu kujichukulia sheria mkononi itafikia wakati watu wasiokuwa na hatia kuuwawa au mahasimu wa biashara au siasa kuuwawa.
 
Kwa hiyo na hao Panya Road wanavyowavamia wananchi, kupora mali zao na kuwau hao hao wananchi ni sawa? Maisha ya panya road yaa thamani zaidi kuliko maisha ya wananchi wengine??? Tusidanganyane jamani; wacha na wao wauawe kama walivyokuwa wanaua wananchi wasiokuwa na hatia.

Nimekwambia miye ni mhanga wao. Nimeitisha nguvu zetu wenyewe, kujilinda. Sina hakika ni wapi unaponisoma nikisema awaye yote kuuwawa ni sawa.

Panya road, polisi muuwa panya road, shabiki wa uuwaji huu, wote hawana tofauti.

Zama hizi hata Ben, Azory, Lijenje, Lissu na wote waliopotezwa au kushambuliwa tungeambiwa ni panya road.
 
Nafikili kwa jicho la tatu sisi watanzania shida yetu kuu ni upumbavu na sio ujinga , jiulize mtu upo radhi kushabikia mtu kuvunja sheria na katiba anaona ni swala dogo tu.

Napatwa nawakati mgumu sana na ikitokea ukasimamia sheria na katiba kama swala linahusiana na uhalifu tegemea kuitwa wewe ni miongoni mwao ,mfadhili au mnufaika na huo uhalifu

Kama taifa tunapaswa kukemea Kwa nguvu zote kuharisha uvunjifu wa sheria/katiba Kwa mwamvuli wa kupambana/kutokomeza uhalifu. Niliwahi kushuhudia raia kujichukulia sheria mkononi alimanusula imuue mume halali kisa tu kaitwa mwizi

Mtu kusikia neno mwizi huyo kufika na kuanza kushusha kipondo pasipo kuuliza ilikuwaje , tabia hii imeshamiri miongoni mwetu 95% . Hili ni janga kwelikweli
 
Mkuu ujinga una dawa. Mtu akielimishwa ujinga humtoka. Upumbavu ni ujinga uliopitiliza kuwa kipaji. Huu sasa hauna dawa. Kwa definition unakuwa upumbavu sasa ndiyo aliouangazia mwalimu.

Ujinga uliopitiliza = upumbavu
 
Unamkamata kibaka unampeleka Mahamani ikibainika kuwa ameua sheria inaamuru anyongwe.
Sasa tusipofuata sheria tulizojiwekea na kuamua tu kujichukulia sheria mkononi itafikia wakati watu wasiokuwa na hatia kuuwawa au mahasimu wa biashara au siasa kuuwawa.

wanaofanya mahakama imkute mtu na hatia ni hao hao polisi???

hivi unafikiri wakitaka kuua watu hovyo ni mpaka wawabambikie kesi ya upanya road??
 
Mimi sina upande kwenye jambo hili. Ila nakazia tu kwa maneno kutoka kwenye maandiko matakatifu.... "AUAE KWA UPANGA, ATAKUFA KWA UPANGA"

Habari hii iwafikie wote bila kuwasahau waliotokomea kusikojulikana na Ben, Lijenje, Azory na waliomtamani Lissu na kusokomeza watu kwenye viroba.
 
Hivi ndivyo polisi Tanzania wanavyouwa watu wakiwamo watuhumiwa wa u panya road.

View attachment 2367623
Ama kwa hakika wao na mashabiki wao, Mwalimu ana maneno sahihi zaidi kwao:

View attachment 2367622
Ulitaka wachekewe kwa sababu hujafyekwa mkono si ndio?

Bora kuwa mpumbavu na kuua majizi..

Yaani majizi yanaenda jela yanarudi yanaendelea na ushenzi wao ,fyeka hao wapuuzi wote..

Tena kwa taarifa yako huku mtaani tukiwanasa na tukawaambia Polisi huwa wanasema tuwamalize kabisa wakute mizoga Ili wazoe..
 
Habari hii iwafikie wote bila kuwasahqu waliotokomea kusikojulikanq na Ben, Lijenje, Azory na waliomtamani Lissu na kusokomeza watu kwenye viroba.
Yeyote aliyehusika na kumuua binadamu kwa upanga, neno linamtabiria kufa kwa upanga.... Hii haibagui Polisi wala Raia wa kawaida.
 
Back
Top Bottom