Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756



Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema leo alfajiri walipokea taarifa kutoka kwa Mbunge wa Viti Maaalum, akiwa na Dereva wa Mbowe, Wilhad Urassa (34) kuwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA wakati akipandisha ngazi kuelekea ndani kwake inadaiwa alishambuliwa na watu 3

Kamanda Muroto amesema “Inadaiwa watu hao 3 waliokuwa wamevaa jackets (makoti) walimshambulia kwa kumkanyaga na kumpiga mateke hasa mguu wake wa kulia. Kutokana na taarifa hizo majeruhi alipelekwa katika Hospitali ya Ntyuka anakopatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.”

Ameeleza, “Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi bila kuacha chochote ili kupata ukweli na usahihi wa tukio hilo. Tukio hili lisitumike kisiasa au kwa njia yoyote ya kujiongezea umaarufu kwa mtu au watu na ni marufuku kuingilia uchunguzi huo.”

Amesisitiza kuwa eneo lile lina Walinzi na Majirani watafanya uchunguzi kujua ukweli wa tukio. Pia, amewaonya Wafuasi wa CHADEMA wanaohamasishana kukutana kwani Jeshi la Polisi lipo macho na yeyote anayefanya mikusanyiko isiyo halali atashungulikiwa kweli kweli

Aidha, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Polisi wanapofanya Uchunguzi hawapaswi kufunga milango ya uchunguzi na kuliita hili ni tukio la kawaida kwasababu viashiria vinaonesha tukio hili lina muelekeo wa kisiasa

Mnyika amesema kati ya watu waliokuwa wanamshambulia Mbowe wapo waliosikika wakisema “Wewe unaisumbua sana Serikali, tunakushughulikia tuone kampeni utafanyaje.” Ametoa wito kwa Polisi na vyombo vya Usalama kuchunguza tukio hilo kwa mapana ili waliohusika wachukuliwe hatua

Amesema siku chache kabla ya Mbowe kushambuliwa, katika mitandao ya Kijamii kulisambaa video ya mtu anayejiita Mchungaji wa Kitaifa, Mchungaji Mashimo akisema “Kuna tukio litatokea mbele kwa Kiongozi wa Upinzani kushambuliwa” na kati ya majina aliyoyataja, jina Freeman Mbowe lilikuwepo. Ametoa wito kwa Polisi wamkamate ili aleeze hizo kauli zake.
 
Uchunguzi ufike mwisho na taarifa ya uchunguzi itolewe.

Hizo marufuku wanazotoa sijui wanazitoa kwa malengo gani, kama hamtaki tukio lihusishwe na siasa mnataka lihusishwe na Corona au kitu gani?!

Tukio lolote lazima lihusishwe na shughuli ya mtu anayoifanya, kujaribu kulitoa nje ya hapo ni sawa na kutengeneza mfereji upeleke maji mlimani.
 
Mhhh mimi naangalia kwa upande huu mwingine wa mashimo. Sio kwamba mashimo alilijua hili either direct au indirect na akafanya kutangaza ili aonekane ana maono ya kinabii kukuza jina lake na kujipatia wafuasi/waumini? Basi akamatwe yy kwanza kama kweli wanachunguza kesi hii.
 
Back
Top Bottom