Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Tundu lissu mwenyewe hakutaka uchunguzi ufanyike mana alikimbia yeye pamoja na shahidi namba moja ( dereva ) ulitaka Askari waanzie wapi uchunguzi kama mashahidi wote hawataki kutoa ushurikiano?
Muwe mnaangalia vyakula mnavyojua,si kubugia tu maharage hata kama hayajawiva.
 
Mhhh mimi naangalia kwa upande huu mwingine wa mashimo. Sio kwamba mashimo alilijua hili either direct au indirect na akafanya kutangaza ili aonekane ana maono ya kinabii kukuza jina lake na kujipatia wafuasi/waumini? Basi akamatwe yy kwanza kama kweli wanachunguza kesi hii.
Mbona kwenye inshu ya Ben Saa8 hamkusema Kubenea akamatwe ilihali mlimsikia mwenyewe kwa maandishi yake, akikiri kujua mahali Ben aliko na sababu ya kujificha?
Mashimo ni Nabii na unabii hauna ushahidi katika ulimwengu wa mwili labda wote wawe kwenye ulimwengu wa Roho.
 
Ungekuwepo maana maiti zingepelekwa mortuary zikafanyiwe post mortem simu zao zingeangaliwa mazungumzo ya mwisho na vitu kama hivyo ambavyo ni ngumu kama mtu yuko hai

Kwani mlivyodukua mawasiliano ya kina Kinana walikuwa mortuary? Kwanini msitumie mbinu hizo hizo kujua kilichokuwa kwenye simu zao?
 
Polisi wafanye kazi kwa weledi wao kubaini wahalifu walihusika
 
Kwani mlivyodukua mawasiliano ya kina Kinana walikuwa mortuary? Kwanini msitumie mbinu hizo hizo kujua kilichokuwa kwenye simu zao?
Watu wapotezw rasilimali kumsaidia mtu ambae haonyeshi ushirikiano BOSS huo ujinga hakuna jeshi linalofanya Afrika nzima
 
Anasemekana alikuwa na mbunge wa viti maalumu na ndio alietoa taarifa polisi,swali saa Saba usiku uko na mbunge wa kike nyumbani kwako mnafanya Nini???
Kuna kosa gani kuwa alipokuwa.
 
Leo wakati Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika akiongea amesema kuwa serekal inatakiwa iwafanyie uchunguzi baadhi ya watu ambao tayari walikua wameshatoa kauli mbaya juu ya kiongozi wao Mbowe kwa kudai kua maneno waliyo ongea yanaendana na tukio.

Pia, Chadema wamesema Polisi TANZANIA wamkamate Mashimo ili wamuhoji sababu anaweza kusaidia katika uchunguz. Hili ni sawa ila hili apa linafikirisha.

Ameweza kumtaja Mchungaji Mashimo ili akamatwe ahojiwe Kama kutoa ushirikiano kwa Polis Ila kakataa kuwataja aliokuwa nao Mbowe ili Polisi isiwahoji, sasa niwaulize chadema mnataka polisi ifanikishe au ifeli?

Kwanini waliokuwa pamoja na Mbowe muwafiche Kuna Sir gani na je wakat mwenyekit Mbowe anashambuliwa wao walikua wanafanya Nini?

Kwani hamuoni kuna umuhimu wa kuwaleta au kuwataja wale waliokuwa na MBOWE ili wahojiwe, waweza kulisaidia jeshi la Polisi?

Kwanini Mashimo ametajwa na hakuwepo eneo la tukio ila waliokuwepo wamefichwa? Mkiulizwa sababu et mnafanya uchunguzi. Uchunguzi gan huo? Hamtak kuonyesha ushirikiano kwa Polis wakiacha kufatilia Mambo yenu mnasema wanatumika, why?


Hili tukio ni kubwa na linasikitisha. Tafadhali acha kufundisha vyombo vya dola vifanye nini. Tumefika pabaya kwa sasa.
 
Watu wapotezw rasilimali kumsaidia mtu ambae haonyeshi ushirikiano BOSS huo ujinga hakuna jeshi linalofanya Afrika nzima

Ni raslimali Kiasi gani mlipoteza kwa kudukua mawasiliano ya kina Kinana?
 
“Wewe unaisumbua sana Serikali” .. kuna viongozi wa nchi hawana damu ya Kitanzania
 
Katika eneo husika ni lazima kutakuwa na CCTV cameras. Na safari hii, tofauti na ilivyokuwa wakati wa tukio la kumdhuru Lissu zikapate kutumiwa pia ktk uchunguzi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema leo alfajiri walipokea taarifa kutoka kwa Mbunge wa Viti Maaalum, akiwa na Dereva wa Mbowe, Wilhad Urassa (34) kuwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA wakati akipandisha ngazi kuelekea ndani kwake inadaiwa alishambuliwa na watu 3

Kamanda Muroto amesema “Inadaiwa watu hao 3 waliokuwa wamevaa jackets (makoti) walimshambulia kwa kumkanyaga na kumpiga mateke hasa mguu wake wa kulia. Kutokana na taarifa hizo majeruhi alipelekwa katika Hospitali ya Ntyuka anakopatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.”

Ameeleza, “Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi bila kuacha chochote ili kupata ukweli na usahihi wa tukio hilo. Tukio hili lisitumike kisiasa au kwa njia yoyote ya kujiongezea umaarufu kwa mtu au watu na ni marufuku kuingilia uchunguzi huo.”

Amesisitiza kuwa eneo lile lina Walinzi na Majirani watafanya uchunguzi kujua ukweli wa tukio. Pia, amewaonya Wafuasi wa CHADEMA wanaohamasishana kukutana kwani Jeshi la Polisi lipo macho na yeyote anayefanya mikusanyiko isiyo halali atashungulikiwa kweli kweli

Aidha, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Polisi wanapofanya Uchunguzi hawapaswi kufunga milango ya uchunguzi na kuliita hili ni tukio la kawaida kwasababu viashiria vinaonesha tukio hili lina muelekeo wa kisiasa

Mnyika amesema kati ya watu waliokuwa wanamshambulia Mbowe wapo waliosikika wakisema “Wewe unaisumbua sana Serikali, tunakushughulikia tuone kampeni utafanyaje.” Ametoa wito kwa Polisi na vyombo vya Usalama kuchunguza tukio hilo kwa mapana ili waliohusika wachukuliwe hatua

Amesema siku chache kabla ya Mbowe kushambuliwa, katika mitandao ya Kijamii kulisambaa video ya mtu anayejiita Mchungaji wa Kitaifa, Mchungaji Mashimo akisema “Kuna tukio litatokea mbele kwa Kiongozi wa Upinzani kushambuliwa” na kati ya majina aliyoyataja, jina Freeman Mbowe lilikuwepo. Ametoa wito kwa Polisi wamkamate ili aleeze hizo kauli zake.
Itakuwa ni jambo lenye hisia mbaya, endapo yatatolewa maelezo kuwa hazifanyi kazi ama zimeondolewa. Na pia ni lazima tujiulize ni kwa nini ktk matukio yote mawili ya kuwadhuru hawa viongozi, kuna kuwa hakuna sababu za kuridhisha kw walinzi kutokuwepo lindoni?

Hivi kweli inaingia akilini ya kwamba walinzi kutokuwepo lindoni kutokana na kuondolewa maeneo wanaoishi viongozi kutokana na ugonjwa wa Corona! Si tumepewa taarifa rasmi ya kuwa gonjwa hili si tishio tena hapa nchini, na tena wagonjwa wapo wachache ambao wapo Dar.
 
Chadema sisa imewashinda sasa wanatafuta visingizio,
Eti mwenyekiti ashushwe kisha dereva asijue kama bosi wake ameingia ndani salama?
Na kama derva aliondoka mapema kabla mbowe hajaingia ndani basi huyo deleva anajua kinachoendelea.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuandika tu umedhihirisha kuwa wewe ni matanga, bisha??
 
Chadema sisa imewashinda sasa wanatafuta visingizio,
Eti mwenyekiti ashushwe kisha dereva asijue kama bosi wake ameingia ndani salama?
Na kama derva aliondoka mapema kabla mbowe hajaingia ndani basi huyo deleva anajua kinachoendelea.
Sio kweli, kumbuja nyumba ya Mbowe ilikua juu ghorofani, dereva yupo chini, atasubiri chini atajuaje kama ameshafika nyumbani kwake?, kama hakuna mzigo wa kumsaidia, dereva hapaswi kuhakikisha kwamba ameingia ndani, hiyo ni kazi ya walinzi kumpeleka hadi mlangoni.
 
Uchunguzi gan huo? Hamtak kuonyesha ushirikiano kwa Polis wakiacha kufatilia Mambo yenu mnasema wanatumika, why?
Mpwa kwani wewe kitu gani kinakuwasha? aliyejeruhiwa ni kiobgozi wa Chadema na sio CCM, wewe ni CCM, sasa mambo ya Chadema yanakuhusu nini? unaweza kufunga bakuli lako ukatuachia sisi wenyewe?
 
"Taarifa ya Kamanda wa Polisi imetoa viashiria kwamba, kama ilivyokua kwa tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, ambapo polisi walijitokeza harakaharaka na kutoa kauli ambazo hazionyeshi uhalisia wa tukio.>>> https://t.co/BJ02dEStLC

Katika tukio hili napo polisi wamejitokeza wakijaribu kueleza kama vile ni tukio la kawaida na wakitaka lisihusishwe na siasa" -John Mnyika. #HATUCHUJI #KwanzaHabari
 
Back
Top Bottom