Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Asiwatie mbaroni hao wa Tundu Lisu tu bali aanze na wale wa Arusha Olasiti, wale waliomuua Mawazo na Saanane. Akiweza hayo, tutajua kweli ana kiu ya kumaliza genge la wasojulikana
Wa olasiti mwambie Mbowe alete mkanda wa video alioahidi atautoa kama ushahidi!
 
Inaelekea waliomdhuru Lissu wanafahamika na hakuna wa kuwachukulia hatua.
Ndugu ulitegemea wakubaliwe?, kamwe hawawezi kukubali kuvuliwa nguo mchana kweupe! Pale Soweto Arusha ilidaiwa tume huru ya kimahakama nayo waliikataa. Mnakumbuka jinsi polisi ilivyo wapiga lisasi watu waliomkimbiza mtuhumiwa?. Amini nakwambia hatokamatwa yeyote katika hili!!!...... Sasa hivi viroba vya maiti hawatupi mto ruvu tena bali kule nungwii baharini!. Naskitika kuwa tumekosa kiongozi miongoni mwetu hadi tuanze kuongozwa kutoka Kigali kweli??????...
 
Yupo sahihi mwigulu
Nchi hii ni huru
sio lazima uchunguzi ufanywe na vyombo vya usalama toka nje!
 
Misheni imekamilika.hata mkiwakamata kazi bure.maana haitarudisha UZIMA WA LISSU.mbwa was muindaji akiuliwa kwenye mapambano.muindaji HANA HASARA.atatafuta mbwa mwingine.
Mwenye masikio asikie

Mwenye akili AFIKIRI.
 
Ovyo kabisa. Atasemaje hata Osama alitafutwa kwa muda mrefu? Atambue kwamba uchunguzi wa kumbaini Osama kama ndie mtuhumiwa wa ugaidi tayari ulishakamilika na wao kuridhika na hizo evidence. Alipaswa aseme ikiwa watakaobainika watatoroka tutawasaka hata kwa miaka mingi kama ilivyofanyika kwa Osama.
 
amenikumbusha pale aliposema kwamba ana ushahidi wa jinsi chadema wanavyopanga mauaji na hasa Rwakatale
 
Tuwaache wafurahi wao.lisu alikuwa homa ya CCM.wameanza kupona.
 
Akili inayohitajika kuwafahamu wahusika wa shambulizi kwa Lissu ni ile darasa la pili!!! It's not a rocket science!!!
 
Huyu mwigulu hakuelimika Bali ali-graduate

Hakuna aliyesema vyombo vyetu havina weledi wa kushughulikia suala la Lissu. Tatizo ni kuwa according to CHADEMA serikali ni kati ya SUSPECTS wa shambulio hilo hivyo wanapoteza credibility ya kuchunguza suala hili..
Exactly.

How can you allow one of the suspects to do the investigation?
 
Miafrika kila siku inawaza Utumwa tu Kutawaliwa yaani hakuna hata uwezo wa kufikiri mtoeni huyo Dereva ahojiwe kwanini anafichwa?
 
Kwa maoni yangu tu lakini; Namshauri Mh Mwingulu, ili kuiosha serekali yetu tukufu na pia jeshi letu pendwa la polisi, waseme hivi; Kama mlimpeleka wenyewe Nairobi kutibiwa, basi malizieni pia kwa kuwaleta hao wapelelezi wenu waje kupeleleza kwa gharama yenu.
Si Chadema wanataka hayo?? Wapeni ruksa kwani mtoto akililia wembe mpe.
Wwkitoa kibali,ikabaki suala la kugharimikia watavuna aibu mkuu.
 
Back
Top Bottom