Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Watu "wasiojulikana" hawajawahi kupatikana nchi hii hata kama wakifanya tukio hadharani mbele ya kamera na picha zao kuonekana kwenye magazeti kama tukio la clouds fm na la Nape. Hivyo hakuna haja ya kuleta wachunguzi wa nje wakati inafahamika kuwa watu "wasiojulikana" hawawezi kujulikana!
 
Karibia mwezi unakatika wewe Mwigulu kama waziri wa mambo ya ndani ndo unajitokeza tena kwa maneno ya kunipa matumaini badala ya majibu.

Hii serikali ni ya kikatili sana kama kama waziri wa usalama wa watu ni Bomu kiasi hiki.
 
Karibia mwezi unakatika wewe Mwigulu kama waziri wa mambo ya ndani ndo unajitokeza tena kwa maneno ya kunipa matumaini badala ya majibu.

Hii serikali ni ya kikatili sana kama kama waziri wa usalama wa watu ni Bomu kiasi hiki.
Umeambiwa hao wahalifu watapatikana sasa unataka majibu gani tena?
 
Hivi sheria za nchi zinanizuia kuwa na private investigator?
 
Asiwatie mbaroni hao wa Tundu Lisu tu bali aanze na wale wa Arusha Olasiti, wale waliomuua Mawazo na Saanane. Akiweza hayo, tutajua kweli ana kiu ya kumaliza genge la wasojulikana
Mbona wa mkuranga na kibiti una waisoleti, au si wenzenu?
 
View attachment 596161

Singida. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema hakuna haja ya kuanza kuhangaika kutafuta wachunguzi kutoka nje kwa ajili ya kufuatilia wahusika wa shambulizi la Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu kwa vile vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinajitosheleza na vina weledi na kazi hiyo.

Waziri huyo amesema haoni kwa nini baadhi ya watu wanasisitiza kuletwa kwa wataalamu wa nje kwani hata kama wataletwa bado watalazimika kufanya kazi kwa mazingira ya Kitanzania wakitumia wataalamu waliopo na hata ikiwekezana watahukumiwa kwa kutumia sheria za nchini.

“Nchi yetu inajitegemea hakuna haja ya kuleta vyombo vya nje kufanya uchunguzi...upelelezi utafanywa na vyombo vyetu, watafikishwa katika vyombo vya muhumu na watahukumiwa na watoto wetu,” alisema.

Hivi karibuni Chadema ilitaka wachunguzi nje kuendesha upelelezi kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa Lissu ikidai kuwa hatua yake hiyo haimaanishi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havina uwezo bali vimetuhumiwa katika tukio hilo.

Hata hivyo, Waziri Nchemba alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama daima viko macho na vinaendelea na kazi ya kuwasaka wale wote wanaojihusisha na matukio ya kushambulia watu.

Amesema suala la uchunguzi haliwezi kukamilika kwa siku moja akitolea mfano jinsi Marekani ilivyotumia muda mwingi kumsaka mtuhumiwa wa ugaidi, Osama bin Laden aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaida.

“Uchunguzi hauna ukomo...unaisha pale tu wanapokamatwa wahusika wote lakini vinginevyo uchunguzi hauishi maana hata Marekani walimtafuta Osama kwa muda mrefu sana hawakusema sasa tumesitisha kumsaka,” amesema.
Kiongozi huyo wa Al Qaida aliuawa Mei 2, 2011 na vikosi vya Marekani vilivyoendesha operesheni maalumu iliyoratibiwa kutoka Pentagon na kufuatiliwa kwa karibu na Rais Barack Obama ambaye hivi sasa amestaafu.

Osama alikuwa amejichimbia katika maficho yake nchini Pakistan katika eneo lililojulikana Abbottabad.

Waziri Nchemba aliwatumia salamu wale wanaojulikana kama ‘watu wasiojulikana’ akisema kasumba ya wahalifu wachache kufanya mauaji na kisha kujinadi kwa jina la watu wasiojulikana inaelekea ukingoni.

Ameeleza kuwa dakika za wale wanaojihusisha na uhalifu huo kufikishwa kwenye mkono wa sheria zinahesabika.
Mwigulu ni msukuma anayeishi singida sio mtu wa singida kibaiyolojia,hawezi kuwa na uchungu na mh tundu lisu
 
Watu "wasiojulikana" hawajawahi kupatikana nchi hii hata kama wakifanya tukio hadharani mbele ya kamera na picha zao kuonekana kwenye magazeti kama tukio la clouds fm na la Nape. Hivyo hakuna haja ya kuleta wachunguzi wa nje wakati inafahamika kuwa watu "wasiojulikana" hawawezi kujulikana!

Inawezekana hao watu wanajulikana sana tu.. Na bila shaka viongozi wa serikali wanatuchora kwa jinsi tusivyoweza kuwafanya lolote..
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Mwigulu Nchemba ameahidi kwamba vyombo vya dola lazima vitawatia nguvuni watu ' wasiojulikana' waliomdhuru ndugu yetu Lissu pamoja na jenersli wa jeshi na yule hakimu wa kule Mtwara. Amesema watu hau wanaotajwa kama ' wasiojulikana' siku zao zinahesabika. Source EATV habari!
Pigia mstari zinahesabika.
 
NAOMBA MWIGULU AOMBEWE MAANA ANAKOKWENDA SIKO. MWIGULU SI UNYAMAZE! WEKA MAJI MDOMONI AND YOU WILL BE SAFE
 
Mwigulu ni mtoto mdogo sana,atawezaje kuwatia mbaroni wakubwa zake,kaeni msubirie kama ataweza,yule wa Nape Nauye mbona hakumfanya chochote.
 
Back
Top Bottom