Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Kwahiyo wanampango wa kujitia mbaroni wenyewe?? Hauitaji P.hD kujua watu wasiojulikana ni kina nani?
  • Watu wenye uwezo wa kuingia kwenye makaazi rasmi ya viongozi kisha kufyatua makumi ya risasi na kuondoka bila kuzuiwa
  • Watu wenye uwezo wa kutoroka dodoma baada ya tukio la uharifu bila hata juhudi za kukimbizwa na polisi
  • Watu wenye uwezo wa kumfuatilia mtu kwa wiki kadhaa na hata akitoa taarifa polisi na kwenye vyombo vya habari lakini bado wanao ujasiri wa kuendelea kumfuata
  • Watu wanaofanya jaribio la mauaji na wiki kadhaa zinapita hakuna taarifa ya maana kutoka polisi zaidi ya porojo kua vyombo vya ndani vinauwezo wa kuchunguza tukio hilo
Kila mtu anawajua watu hao ni kina nani na wanaripoti kwa nani.
 
Kashindwa kumtia hatian yule cho.ko alievamia offc za clouds media na picha zipo atawaweza watu wasiojulikana?

Kashindwa kuwatia nguvun wale waliomtolea bastola Nape mchana kweupe sembuse hao wasiojulikana?

Huyo nae kawa mchumia tumbo tuh
 
Mbona aliyemtishia bastora rafiki yake nape hajamkamata sembuse hawa wa SMG, it's beyond his reach, I'm sure.
 
Alishawapata waliowashambulia Sheikh Ponda na wengineo?
Je alishawapata waliowateka kina Ben Saanane na R.O.M.A?
Wanajenga maswali badala ya majibu!
vi-wonder in action.
Tunamuomba Mola atuvushe salama maana...
 
Mbona aliyemtishia bastora rafiki yake nape hajamkamata sembuse hawa wa SMG, it's beyond his rich.
Maajabu ya ajabu! Hatupaswi kuhoji hayo wala kuuliza kwa maana tu wasahaulifu
 
Ndoto ya mchana, kama aliyemtishia Nape kayeyuka sembuse wavamizi wa Lissu. Hizo ni kelele tu wakati huo tunasogeza muda
 
Kashindwa kumtia hatian yule cho.ko alievamia offc za clouds media na picha zipo atawaweza watu wasiojulikana?

Kashindwa kuwatia nguvun wale waliomtolea bastola Nape mchana kweupe sembuse hao wasiojulikana?

Huyo nae kawa mchumia tumbo tuh
Nchi inaongozwa na IKULU, hawa wengine ni justification ya katiba tu, it's one man show
 
Wwkitoa kibali,ikabaki suala la kugharimikia watavuna aibu mkuu.

Nimeshauri kuwa wawape ruksa ya kutafuta Private Investigator aje kuchunguza kivyake apewe ruksa kumleta muuaji mahakamani na iwe mahakama yeyote wanayotaka kufungua kesi yao. Kama wakifanya hivyo malipo watajua wenyewe Cdm
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Mwigulu Nchemba ameahidi kwamba vyombo vya dola lazima vitawatia nguvuni watu ' wasiojulikana' waliomdhuru ndugu yetu Lissu pamoja na jenersli wa jeshi na yule hakimu wa kule Mtwara. Amesema watu hau wanaotajwa kama ' wasiojulikana' siku zao zinahesabika. Source EATV habari!

Baada ya kujibizana risasi waliwahiwa no bolisi. Hivyo hakuna wa kumshtaki
 
Umekariri chombo cha dola ni polisi pekee!
usiniwekee hisia zako.nimetaja chombo cha dola na sijasema ni polisi pekee.nimeandika kwamba kuchukua video hakumfanyi mtu kuwa chombo cha dola !.that is all!!
 
Home boy wake kabisa anamtosa eti kisa siasa, ujinga mtupu, wakati Jamaa halijiulizi Bashite anatesa kama PM hata yeye anamgwaya, kisa nini?
 
Back
Top Bottom