Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Kushambuliwa Tundu Lissu: Mwigulu aahidi vyombo vya dola vitawatia mbaroni watu wasiojulikana!

Naam huo ndiyo ukweli. Walimdhuru Lissu wamo Serikalini na wala si watu wasiojulikana. Wanajulikana sana na ndiyo sababu wanahofia wapelelezi wenye uwezo mkubwa kuingia nchini na kufanya vitu vyao maana ushahidi utawaumbua hawa ambao wamekuja na huu mtindo wa kutisha wa kuua wapinzani tena kwa kuwawinda.

Inaelekea waliomdhuru Lissu wanafahamika na hakuna wa kuwachukulia hatua.
 


Huyu mwigulu hakuelimika Bali ali-graduate

Hakuna aliyesema vyombo vyetu havina weledi wa kushughulikia suala la Lissu. Tatizo ni kuwa according to CHADEMA serikali ni kati ya SUSPECTS wa shambulio hilo hivyo wanapoteza credibility ya kuchunguza suala hili..
 
huyu kazi anayoweza ni kujifunga skafu na kuvaa tie yenye rangi za bendera ya tanzania tu labda na kulea familia yake
afadhali yeye hata kufunga skafu wewe kipi unaweza? Kukaa nyuma keyboard kulialia acha majungu
 
Naam huo ndiyo ukweli. Walimdhuru Lissu wamo Serikalini na wala si watu wasiojulikana. Wanajulikana sana na ndiyo sababu wanahofia wapelelezi wenye uwezo mkubwa kuingia nchini na kufanya vitu vyao maana ushahidi utawaumbua hawa ambao wamekuja na huu mtindo wa kutisha wa kuua wapinzani tena kwa kuwawinda.
Hizo ni hisia zako lakini tutakutaka uonyeshe hisia zako pamoja Na ushahidi kwahiyo uwe Na ushahidi wakutosha
 
Mwi guru I believe wewe ni church goer kuwa mkweli kama hamkuhusika mnachoogopa ni nini kuwa ruhusu fbi au Scotland yard kuja? Kukataa kwenu kuna maanisha mnajua ni nani anahusika. Benny yuko wapi? Wauaji wa mawazo vipi? Mteja wa nape vipi? U limbo ka kibanda vipi?
 
Huyu naye si ndo alisema atatoa majibu ya aliyetoa bastola kwa nape, njaa inakosesha Utu na ucha Mungu, nayeye namwonaga kanisani akigongaga ishara ya msalaba
 
Inaelekea waliomdhuru Lissu wanafahamika na hakuna wa kuwachukulia hatua.

Umemaliza kila kitu kwa sababu ya sababu alizo ziainisha Mh Waziri hazina mashiko hasa ukizingatia nabtukio lenyewe na Historia mbaya ya Serikali (ya awamu hii) dhidi ya Wapinzani...
 
View attachment 596161

Singida. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema hakuna haja ya kuanza kuhangaika kutafuta wachunguzi kutoka nje kwa ajili ya kufuatilia wahusika wa shambulizi la Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu kwa vile vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinajitosheleza na vina weledi na kazi hiyo.

Waziri huyo amesema haoni kwa nini baadhi ya watu wanasisitiza kuletwa kwa wataalamu wa nje kwani hata kama wataletwa bado watalazimika kufanya kazi kwa mazingira ya Kitanzania wakitumia wataalamu waliopo na hata ikiwekezana watahukumiwa kwa kutumia sheria za nchini.

“Nchi yetu inajitegemea hakuna haja ya kuleta vyombo vya nje kufanya uchunguzi...upelelezi utafanywa na vyombo vyetu, watafikishwa katika vyombo vya muhumu na watahukumiwa na watoto wetu,” alisema.

Hivi karibuni Chadema ilitaka wachunguzi nje kuendesha upelelezi kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa Lissu ikidai kuwa hatua yake hiyo haimaanishi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havina uwezo bali vimetuhumiwa katika tukio hilo.

Hata hivyo, Waziri Nchemba alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama daima viko macho na vinaendelea na kazi ya kuwasaka wale wote wanaojihusisha na matukio ya kushambulia watu.

Amesema suala la uchunguzi haliwezi kukamilika kwa siku moja akitolea mfano jinsi Marekani ilivyotumia muda mwingi kumsaka mtuhumiwa wa ugaidi, Osama bin Laden aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaida.

“Uchunguzi hauna ukomo...unaisha pale tu wanapokamatwa wahusika wote lakini vinginevyo uchunguzi hauishi maana hata Marekani walimtafuta Osama kwa muda mrefu sana hawakusema sasa tumesitisha kumsaka,” amesema.
Kiongozi huyo wa Al Qaida aliuawa Mei 2, 2011 na vikosi vya Marekani vilivyoendesha operesheni maalumu iliyoratibiwa kutoka Pentagon na kufuatiliwa kwa karibu na Rais Barack Obama ambaye hivi sasa amestaafu.

Osama alikuwa amejichimbia katika maficho yake nchini Pakistan katika eneo lililojulikana Abbottabad.

Waziri Nchemba aliwatumia salamu wale wanaojulikana kama ‘watu wasiojulikana’ akisema kasumba ya wahalifu wachache kufanya mauaji na kisha kujinadi kwa jina la watu wasiojulikana inaelekea ukingoni.

Ameeleza kuwa dakika za wale wanaojihusisha na uhalifu huo kufikishwa kwenye mkono wa sheria zinahesabika.
mwigulu umenena vyombo vya nje ni kujishushia heshima kwani tuna jeshi imara
 
Safi sana,lakini hili la sasa halina sababu.Aanze kwanza na la Ben Saanane.
 
Mwigulu ‘awagomea’ CHADEMA kuhusu wachunguzi huru
Mwigulu hajawagomea Chadema kwa sababu mbili; kwanza, hayo mamlaka ya kutoa maamuzi hana...ayatoe wapi? Pili, hata kama angekuwa nayo, hawagomei Chadema, anawagomea raia wapenda haki wa nchi wanaotaka kuona haki inatendeka. Labda nimuulize mtoa mada je katika hii katuni, nafasi ya Mwigulu iko wapi?

udikteta1-jpg.596531


 
Waziri wa mambo ya ndani mh Mwigulu Nchemba ameahidi kwamba vyombo vya dola lazima vitawatia nguvuni watu ' wasiojulikana' waliomdhuru ndugu yetu Lissu pamoja na jenersli wa jeshi na yule hakimu wa kule Mtwara. Amesema watu hau wanaotajwa kama ' wasiojulikana' siku zao zinahesabika. Source EATV habari!
Kwani nani alowabatiza jina la "Wasiojulikana?"
 
Mimi Sioni sababu ya kumsema sana mwigulu, yawezekana hiyo mission ya kummaliza Lissu hajui chochote Ila maelekezo kutoka juu ndio yanatenda kazi.
 
Back
Top Bottom