Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Walimuonea Hakuna sheria inayozuia kufuga Ndevu
 
Kama ana amani ya moyo hilo latosha.

Tunatofautiana maono na ndoto katika maisha.

Ostadh piga jembe na sala 5 kwa sana.
Alwaz
 
Kumbe siku hizi hapa Tanzania kuna sheria inayo tambua ndevu kama kiwakilishi cha dini fulani? Mimi nilikuwa sijui.

Halafu nyinyi si mnashinda humu mkiuponda ualimu kuwa ni kazi ya hovyo na walimu wana maisha magumu, kwa hiyo sasa hivi imekuwa kazi nzuri sana mpaka umponde jamaa kwa kuiacha?

Yeye ali amuwa kuacha kazi kwa sababu zake ndevu kilikuwa kisingizio tu maana tofauti na jeshini hakuna sehemu nyingine ambayo Serikali ina mkataza mtu kufuga ndevu akiwa kazini.
 
Ni lazima kwa baadhi ya Madhebu ya kiislamu Kama ibadhi,Answar,salafiya,malikiya na wengine
Sio lazima, hata ukienda kwao kweny taasisi zao sio wote wanafuga ,wengine hawana kabisa kutokana na maumbile yao.

Mi nakumbuka kuna rasta mmoja mwanae hakusoma kwa vile aliambia akate nywele ndio aanze darasa la kwanzq ,walikataa kabisa yaani.
 
Kuna vijana wawili waliacha kibaha boys PCB, wakisema hii elimu inaukafiri,

They were more than smart guys, nataman nijue sasa wako wapi
Wengi wa namna hii huishia kwenye makundi ya ugaidi ama maisha yakiwachapa huishia kujuta na kuachana na dini.

Mimi kuna jamaa tulisoma nae chuo Mwaka wa pili akaacha kwa sababu kama hizohizo, aliporudi kitaa kakaa kama miaka miwili ngoma ikawa tight akili zikamrudi akaanza kutafuta opportunity ya kurudi chuo Ardhi
 
Kila mtu aishi maisha yake kwake swala la dini yake lilikuwa ndio priority kwake hayo mengine ni ziada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…