Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Ndevu mpaka Prince Harry anafuga.Nyinyi sijui mna nini na ndevu.
Zamani mababu zetu mliwalazimisha mpaka kubadili majina na dini ili wasome.Kama wasingetokea mashujaa wakakataa sijui tungekuwa wapi leo hapa Tanzania
 
Atakuwa anakula ndevu zake sahiv kama chakula.Kuna watu wahovyo sana kutaka kulazimisha mambo yao Kila sehemu Kwa kuhisi ndiyo wenye haki kumbe ujinga TU.
Kama huyo mwalimu mkuu anayeingiza chuki zake kwa waajiriwa wenzake
Wapi imeandikwa kuwa ndevu si maadili ya mwalimu
mnaona jeans na vimini mnavyovaa nyinyi ndio maadili ya ualimu.
Acheni ujinga huo.
 
Sio lazima ,hata ukienda kwao kweny taasisi zao sio wote wanafuga ,wengine hawana kabisa kutokana na maumbile yao.

Mi nakumbuka kuna rasta mmoja mwanae hakusoma kwa vile aliambia akate nywele ndio aanze darasa la kwanzq ,walikataa kabisa yaani.
Rasta haziruhusiwi kwa sheria!
Na pia..
Kama nilivyosema tu inategemea na Madhehebu kila Dhehebu lina itikadi zake na kuna Ulazima wake katika kufanya mambo..
Na hata hizo Taasisi inategemea ni za Dhehebu gani
 
hahahahahaa
dini imeleta msala afirika
 
Kuna maza fulani alikuwa anaishi karibu na chuo cha butimba, nasikia alikuwa askari nilikuwa namwona akiuza mboga mboga, kumbe aliacha kazi baada ya kulazimishwa kuwa anafanya kazi siku ya sabato. Maza alikuwa anatembeza mboga pale shule iliyopikwa anatuletea tunanunua na kumix kwenye ugali.
 
Hatari
 
Inaongelea dini gani ?

Kwenye Uislamu kama ndevu unazo ni lazima kuzifuga kama huna kabisa, hii Sheria haikuhusu.

Kufuga ndevu ni Sunnah za mitume wote.
umesema sunna, kivipi iwe lazima? mbona mnafanya waislam wengine waonekane kituko? ndevu sio lazima kufuga japo pia haipendezi kwa (mwanaume kunyoa kabisa pakabaki kama shavu kwa mtazamo wangu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…