Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Kumbe hata maana ya Sunnah huijui. Kwanini hamsomi vijana ?
Kwa hiyo mtume aliamrishwa kufuga ndevu kweny Qur an ?Ebu soma uelewe.

Yapo mafunzo ya kisunnah juu ya umuhimu wa ndevu ila sio lazima
 
Ni jirani yetu huko nyumbani kwetu, pia kuna kaurafiki kwa mbali baina yetu. Likizo sometimes tulikuwa tunajisomea pamoja kwakuwa tulikuwa darasa moja.

Jamaa akawa teacher wa Serikali baadaye. Sasa nasikia walimu wana miiko mingi kutokana na mazingira yao ya kazi, sometimes wanakuwa walezi.

Sasa jamaa hakuacha sunnah ya Mtume akafuga ndevu vizuri. Mkuu wa shule akamwambia Mr nyoa hizo ndevu hii shule ni secular, jamaa akakataa.

Alipoona anazidi kuhimizwa kunyoa uchebe na sometimes kutishiwa kufutwa ajira akamwahi boss wake akaandika 24 hrs resignation letter, mkuu wa shule akaipitisha, na Mkurugenzi akamaliza kazi.

Jamaa sasa kwa moyo mweupe analima kijijini. Kaka yake aliyemsomesha wamegombana baada ya jamaa kupiga kalamu chini lakini anasema hawezi kurudi.

Tatizo watu wanachukuwa utamaduni na kufanya ni dini. Vilemba na ndevu ni utamaduni sio dini. Ni kwamba wenye utamaduni fulani ni wa dini fulani hii inachanganya wanaopenda kuiga
 
Sio lazima, hata ukienda kwao kweny taasisi zao sio wote wanafuga ,wengine hawana kabisa kutokana na maumbile yao.

Mi nakumbuka kuna rasta mmoja mwanae hakusoma kwa vile aliambia akate nywele ndio aanze darasa la kwanzq ,walikataa kabisa yaani.
Sasa hivi kuna waraka unaoruhusu rasta shuleni.
 
Duniani kote wanafikiria namna ya kuzipata rasilimal za africa, lakini waafrika wanawaza namna ya kwenda mbinguni, hapo hapo nikaachana na usabato rasmi [emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwamba akiwa na ndevu ndefu utilio hauwezi kushuka ?

Anyway to each their own...; Kama hio Shule inaona hizo Ndevu ni Kero na yeye anaona hawezi kunyoa basi Busara ni kila mmoja kuchukua hamsini zao...

Ila hii shule ingeweza kumfukuza hata Archimedes sababu ana ndevu ndefu....
 
Wasabato nakumbuka nilikuwa mwaka 2012 wakasema miaka kumi ijayo sitanunua kitu bila chapa 666 nashangaa saiv nipo 2024 sijui hao jamaa wanatuonaje
Jamaa huwa wanajiona wana VISA ya kwenda Mbinguni yaani. Na sisi wengine tunaonekana wa motoni daima. Waulize tu wakufafanulie hiyo 666 kwa maelezo yao inapatikana wapi ndio utasikia mapicha picha.
 
Mods naona mmeamua kuchagua kuwa upande wa mtoa hoja kusambaza sumu hii! Kwanini kwenye heading msiondoe hiyo sentensi ya kwanza ikabaki ya pili tu?
 
Kuna vijana wawili waliacha kibaha boys PCB, wakisema hii elimu inaukafiri,

They were more than smart guys, nataman nijue sasa wako wapi
They were more than smart guys

[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Kuna vijana wawili waliacha kibaha boys PCB, wakisema hii elimu inaukafiri,

They were more than smart guys, nataman nijue sasa wako wapi
Kuna mtoto wa mama mkubwa alimuambia mwanae asiendeleee kusoma sheria sababu ni kazi ya dhulma. Dogo akapelekwa VETA. Sasa hivi kawa mvuta bangi na kunywa pombe. Hataki kazi yoyote. Dini hizi ni noma.
 
Inaongelea dini gani ?

Kwenye Uislamu kama ndevu unazo ni lazima kuzifuga kama huna kabisa, hii Sheria haikuhusu.

Kufuga ndevu ni Sunnah za mitume wote.
Umeshasema ni suna halafu hapohapo unasema ni sheria.
 
Kwahiyo usecular hautaki ndevu ama? basi watunge sheria tu kuwa kufuga ndevu ni marufuku. Tz.

Mleta mada umeshindwa kumuelewe mwenye matatizo ni nani kwenye hiyo hadithi yako. Jamaa yupo sahihi 100% na hivyo ndivyo wanaume wanavyotakiwa wawe sio kuyumbishwa yumbishwa.
Huyu mwalimu ni dhaifu ndio maana kakimbia kazi. Angetakiwa apambane na huyu mwalimu mkuu kutumia sheria.
 
Mkuu inategema na Madhahab Gani?
Niliwahi kuwa Salafiya.na Answar pia..
Usipofuga Ndevu hata swafu ya Mbele ya Swala utaisikia tu utapelekwa safu ya Nyuma..
Na utapigwa Vijembe na kuitwa mwanamke..

Kuna hadithi Nyingi wanazo za kuhalalisha wasemacho kuwa Ni sunna Zenye Faradhi ndani..
Kama hujawahi kuwa hilo dhehabu huwezi kunielewa
Yaani inaonyesha ni jinsi gani hata Quran hawaijui. Madhehebu yamekatazwa kwenye Quran lakini bado watu wanajigawanya. Ila hizi dini 2 ndio zimeleta majanga duniani.
 
Back
Top Bottom