meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,425
- 4,768
Ni wazi kuwa Chadema ilijaribu kucheza karata zake kisiasa kadri ilivyowezekana ili kujirudisha kwenye ramani ya siasa Tanzania.
Uchaguzi uliopita uliiacha chadema kwenye anguko kubwa yaani kutokuwepo kwenye eneo muhimu la kimaamuzi kupitia uchaguzi. Naamini baada ya kuliona hili viongozi wa CHADEMA walitafakari na kujipanga vyema ili waweze kurejea japo kwa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Ajenda za ushindi katika uchaguzi zinajulikana zaidi niseme ni maswala ya huduma za jamii,maswala ya biashara ,uchumi wa mtanzamia mmoja mmoja na ikibidi kujenga hasira dhidi ya chama tawala.
Kwa upande wa ajenda za huduma za jamii Rais Samia amefanya mengi na ameyaeleza,kwa upande wa biashara amejitahidi kufanya vyema ikiwemo kupambana na majaribio kadhaa ya migomo iliyoratibiwa vyema na wapinzani ya wafanyabiashara .
Kwa upande wa uchumi pamoja na presha kubwa ya hali ya kidunia bado ameweza kuhimili.
kwa upande wa kuibua hasira za wananchi pia alifanya vyema kwa kuja na 4 Rs. CHADEMA imekosea kutumia turufu hii ya mwisho au niseme haikujiandaa vyema au pengine ni ugumu waliokutana nao kutoka kwa intelijensia ya Serikali ya Samia.
Hivi karibuni tumeshuhudia mabadiliko makubwa na kushtua au kushtukiza yaliolenga vyombo vya kiusalama na diplomasia ikiwemo kuondolewa kwa Makamba na Nape(Niliwahi kuhoji kama Nape alitaka kuandaa vonoco dhidi ya Magufuli)
Soma Pia:
- Je, Nape alikuwa ni mmoja wa waandaaji wa #VoNoCo dhidi ya Rais Magufuli?
- Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024
Mabadiliko haya makubwa na ya hatari katika Taifa yasingeweza kupita hivi hivi bila misukosuko mikubwa.
Mwezi septemba tunajionea kashikashi kubwa inayotaka kumtokea Rais Samia ambayo unaweza kuifananisha na kashikashi nyingi zilizowahi kuwakuta kina Jakaya Kikwete na John Pombe Magufuli, mfano maandamano makubwa ya wamasai,Utekaji na mauji mfululizo yenye kuibua ghadhabu za umma na sasa jaribio la maandamano la CHADEMA .
Hata hivyo inaionekana Samia alijipanga mno tena sana.
Leo inaweza kuwa ni siku muhimu kwa Rais Samia kwa kufanikiwa kuzima jambo kubwa pengine Jaribio baya la kumuangusha. Ila kwa mafanikio haya naiona njia nyeupe kuekelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na hatimaye 2025
FOR GTs ONLY