Kusoma Postgraduate (Master/PhD) UDSM majanga

Mfumo wetu wa ELIMU ni wakumpima mtu anae weza kukumbuka vitu vilivyo fundishwa na ukiwa na uwezo mkubwa wa kukariri unaitwa una akili.....

Nimebadilisha mtazamo kuhusu ELIMU na AKILI ni vitu viwili tofaut akili ni Zaid ya hizi certificate zetu tunazo jinasibu nazo humu...................

ELIMU sahihi ni Ile itakayo mfanya binadamu akaweza kuyatawa maisha yake...

Umenena vyema! Mafanikio ya kielimu na Akili ni vitu viwili tofauti.
 
Tatizo letu watanzania Kila mtu anajua Kila kitu. Watanzania inabidi tujifunze kuheshimu kazi za kitaalamu. Mkuu unataka Prof. asikufundushe theory za research bali akufundishe softwares kama hiyo software ndio inayofanya research!!!!
Hivi ukienda field ukatumia hiyo software kwenye data analysis ikakupa r=0.5 utafanya nini? Unataka ufundishwe software atafundisha ngapi sababu karibu Kila mtu atatumia software tofauti na mwingine kuanzia kwenye kudesign study na kufanya data analysis.
Halafu pia software zinakuja mpya Kila siku je ukihitimu nani atakufundisha software mpya huko makazini?
Software zinakuja na user manual na Kuna video kibao you tube kwa Kila software unaweza kuangalia ukajifunza ina haja gani kufundisha?
Assumption ni kwamba ukienda field utakuta watu kwenye research group watakufundisha kwa hiyo si kitu kigumu sana kama unajua kufanya research.
Pia software nyingi zina customer contacts email yaani ukiandika tu hapo hapo mtu anakujibu kukusaidia mpk kukusaidia kurepair software yako Kama haifanyi kazi vizuri. Sasa hapo Kuna haja ya kufundisha software badala ya kufundisha namna ya kufanya research?
Halafu kwa Sasa Kuna vyuo vingi kwa nini unakomaa udsm wabadili standards zao na usiende kwenye vyuo ambavyo vina standard unayoitaka?
 
Halafu Kuna wale wanalalamika supervisor hawasomi kazi kwa wakati nao hawaelewi tu mzigo uliopo kwenye kuisimamia wanafunzi.
Unakuta mtu ana wanafunzi 15 wa PhD wakati standard ni watano ongeza na wa masters, bado vipindi kufundisha hapo unataka asome kazi kwa muda unataka wewe wakati hata wew hutaki kazi ya kufundisha unataka kwenda UN, TRA, TBS, bungeni au hata wizarani.
Maprof. wazee wazoefu wote wamekimbilia siasa na green pastures kwingineko halafu unataka mtu ajipinde eti wewe umalize shule muda unataka wewe wakati hata ukimaliza hiyo masters yako hutaki kubaki kufundisha tulijichimbia kaburi wenyewe ngoja itajulika tu...washaurini baba na mama zenu warudi kufundisha wasime kazi zenu kwa muda sio watu wanajazana wizarani tu kuattend mafile halafu eti mtu mwingine ajipinde.
 
Mkuu umeandika Kwa uchungu sana na makasiriko mengi... nimecheka sana neno KUJIPINDA😀😊
 
Sasa kama Wana mzigo kwanini wanapokea postgraduate pia wao hawajali mda uzembe wao mwanafunzi unakuwa unapata fine ya extension fee wakati kosa si lako. Hafu kwahyo wahadhiri watanzania tu ndio wanakazi wa nchi za nje ndio hawana kazi eeeh.
Hafu postgraduate udsm Huwa ni Wachache mno masters waweza Kuta watano, wengine hawazidi 30 ni wako Wachache huo wingi unaosema ni upi?
Usipende kutetea uzembe na madaktari wa hospitalini wasemeje sasa
 
Mkuu watu
Mkuu umeandika Kwa uchungu sana na makasiriko mengi... nimecheka sana neno KUJIPINDA😀😊
watu hawaelewi tu vile wanataaluma wametelekezwa mpk wengine wameamua kuhamia kada nyingine kutafuta fursa....kwa load iliyopo vyuoni hakuna siku seriali itakuwajibisha supervisor kwa nini mwanafunzi hatoki kwa wakati...tusikwepe tatizo tulitatue.
 
Sasa kama Wana mzigo kwanini wanapokea postgraduate pia wao hawajali mda uzembe wao mwanafunzi unakuwa unapata fine ya extension fee wakati kosa si lako. Hafu kwahyo wahadhiri watanzania tu ndio wanakazi wa nchi za nje ndio hawana kazi eeeh.
Hafu postgraduate udsm Huwa ni Wachache mno masters waweza Kuta watano, wengine hawazidi 30 ni wako Wachache huo wingi unaosema ni upi?
Usipende kutetea uzembe na madaktari wa hospitalini wasemeje sasa
Niletee student teacher ratio ya udms nikuwekee ya Stanford unajua kazi ya mhadhiri ni kusoma kazi yako tu wakati ana wanafunzi mia tano wa undergraduate anafundisha unazungumzia nini mkuu.
 
Hyo inanihusu Nini Mimi mwanafunzi na kuweka kisingizio kutimiza wajibu wenu wa kazi taasisi niliyosoma tu darasa letu master's tulikuwa sita, PhD hata watano hawafiki Sasa hyo kuwa wazembe wa kazi na mzigo waache kazi ka ngumu kuliko kutokutimiza wajibu wao si ndio Huwa Wana gpa kubwa. Kwanza mhadhiri Huwa Wana share topics na Kuna tutorial assistance so usije singizia ugumu wa kazi hapa bana. That's why imekuja system ya kuwafatilia both. Hata postgraduate student ana haki ya kupata equal treatment ka undergraduate.
 
Kwahiyo Mkuu unataka na sisi tusote kama mlivyosota😆

Kumbe wewe Engineer kabisa 😊
Lisu akiwa Rais tutakupa Uwaziri wa teknolojia😂.

Hebu tuma voicenote ya kimalkia tuone., lazima kalafudhi ka kimachame kamo ndani yake.
Hahahaaa

Mama la mama leo unanipanga jamani

...Kuraaaa chuma hicho mpenzi mtazamaji..... 😂 😂 😂 😂 😂
 
Hyo inanihusu Nini Mimi mwanafunzi na kuweka kisingizio kutimiza wajibu wenu wa kazi taasisi niliyosoma tu darasa letu master's tulikuwa sita, PhD hata watano hawafiki Sasa hyo kuwa wazembe wa kazi na mzigo waache kazi ka ngumu kuliko kutokutimiza wajibu wao si ndio Huwa Wana gpa kubwa. Kwanza mhadhiri Huwa Wana share topics na Kuna tutorial assistance so usije singizia ugumu wa kazi hapa bana. That's why imekuja system ya kuwafatilia both. Hata postgraduate student ana haki ya kupata equal treatment ka undergraduate.
Kwa hiyo inamhusu nini mhadhiri ambaye naye anawakuta tu wanafunzi darasani?...nimekupa kazi uniletee ratio hujaleta unaanza leta hoja nyingine...tuache ujanja ujanja watanzania tunawekeza kwenye siasa halafu tunataka kuvuna kwingineko...wewe baada ya kuhitimu MSc kwa nini hukubaki idarani kwako utatue hizo changamoto ukakimbia. Ungeongea na superior wako angekuambia yanayowasibu wanataaluma.
Kama mwajiri anaona mwajiriwa hafanyi kazi vizuri kwa nini hamfukuzi kazi? Iulize serikali yako hilo swali sio yule unayemtuhumu kutotenda kazi vyema.
 
Hyo inanihusu Nini Mimi mwanafunzi na kuweka kisingizio kutimiza wajibu wenu wa kazi taasisi niliyosoma tu darasa letu master's tulikuwa sita, PhD hata watano hawafiki Sasa hyo kuwa wazembe wa kazi na mzigo waache kazi ka ngumu kuliko kutokutimiza wajibu wao si ndio Huwa Wana gpa kubwa. Kwanza mhadhiri Huwa Wana share topics na Kuna tutorial assistance so usije singizia ugumu wa kazi hapa bana. That's why imekuja system ya kuwafatilia both. Hata postgraduate student ana haki ya kupata equal treatment ka undergraduate.
Hiyo inamhusu nini mhadhiri ambaye naye anawakuta tu wanafunzi darasani? Nimekuambia ulete ratio hujaleta unaanza leta hoja nyingine....kaam mwajiriwa hafanyi kazi vizuri kwa nini Sasa mwajiri asimfukuze kazi? Iulize serikali yako hilo swali...tunawekeza kwenye siasa halafu tunataka kuvuna kwingineko umeona wapi hiyo? Wewe baada ya kuhitimu MSc kwa nini hukubaki idarani kwako utatue hizo changamoto ukakimbia? Ni rahisi kusema lakini kutenda Sasa...
 
Usijichanganye kusoma Masters au PhD UDSM utajuta hizo course za Research sijui Methodology walimu wanabahatisha.

Dunia ya Leo imejaa Statistical analysis tools/software Ila mtu kutwa kakomaza fuvu kuelezea historia ya Standard Deviation by Kothari (2004).

NB Postgraduate office wao wanajua kugawa majoho tu.
🤣🤣🤣🤣 ...natunako enda ndio kabisaa technology itawafuta kazi watu wengi . Mfano ile chart gpt
 
Hiyo inamhusu nini mhadhiri ambaye naye anawakuta tu wanafunzi darasani? Nimekuambia ulete ratio hujaleta unaanza leta hoja nyingine....kaam mwajiriwa hafanyi kazi vizuri kwa nini Sasa mwajiri asimfukuze kazi? Iulize serikali yako hilo swali...tunawekeza kwenye siasa halafu tunataka kuvuna kwingineko umeona wapi hiyo? Wewe baada ya kuhitimu MSc kwa nini hukubaki idarani kwako utatue hizo changamoto ukakimbia? Ni rahisi kusema lakini kutenda Sasa...
Inatosha mkuu umeeleweka. Unaongea kwa uchungu mno. Utakua mhadhiri bila shaka.
 
Unaweza kuwa na point ila umegusia juu juu kiasi kwamba nashindwa kukupata kuwa changamoto ni ipi, maana hiko chuo kina wageni wengi kutoka nje na wamepata shahada za izamili na uzamivu hapo na walisifia u ora wa epimu, je kipengele kipo kwenye baadhi ya college au ni mfumo wa chuo kizima??, Maana kuna taasisi nyingi hapo ni ngumu kujua specific wapi kwenye mapengo yanayohitaji kuzibwa.
Ulicho andika hapa kinaonyesha kiasi gani una high level of maturity. 👏👏
 
Utakuwa lecturer mbaya na hapa ndipo Tanzania tunapoangukia! Tunafikiri kuwa lecturer hapaswi kuwafundisha wanafunzi wake jinsi ya kutumia statistical softwares?!

Wanafunzi wanafanya practicals za statistics kivipi kama lecturer haingii lab nao na kuwaongoza? Kwanini unafikiri kazi ya lecturer ni kutoa nadharia tu? Unajua kwanini Tanzania wasomi wetu hawawezi kujiajiri na wana elimu za nadharia pekee? Ni kwasababu wanafanya kama unavyofikiri.

University of Glasgow in Scotland wana policy kwamba kila mwanafunzi ajue na atumie R statistical software katika kazi zake hasa wanafunzi wa science. Software hiyo inafundishwa kwa 90% practicals na 10% ndio theory. Huku kwetu ni kinyume. Ujinga una gharama kubwa!
Mkuu hiyo R unaweza kufundishwa lakini usije kutuma Maisha yako yote..mfano mtu wa molecular dynamics naye unataka atumie R kwenye kazi zake? Huoni Kama inategemea na field ya mtu?
 
Hata Mimi nilikua na wazo la kufundishwa software nikiwa pale jalalani 😂. Lakini nilivyohitimu nikaja kushtuka aiseee, unaweza fundishwa software toka module ya kwanza mpaka unavaa joho maana software ni nyingi na zote za muhimu kwenye field Yako. Just imagine kwenye topic Moja Kuna kama software 5. Nadhan wanafunzi pana haja ya kujibidisha mbali na kile anachokupa mwalimu.
 
Back
Top Bottom