Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Tunaishi Tanzania na sio huko kwenye kampuni za Benz na Apple,na tunaishi kulingana na mazingira yanavyituhitaji.Kama wewe ni majiriwa na takwa kuwa na degree ya pili basi lazima utafanya hivyo vilvile kama umejiriwa private basi kuna ushindani na sofa za ziada zitakuwezesha kukabiliana na ushindani wowote utakaojitokeza.Kwani elimu kubwa sana ina umuhimu kufika ngazi hizo? Taasisi au kampuni zote duniani zinazofanya vizuri vyeti vyako watu wataviangalia ngazi ya entry level ila kuanzia hapo hamna atayetaka kujua umesoma mpaka ngazi ipi. Kitu cha muhimu watu watataka waone kazi ulizowahi kufanya na sio elimu yako.
Unafikiri kampuni kama Benz au Apple wakitaka chief designer watataka kujua umesoma mpaka Master's /Ph.D? Wao kitu cha msingi ni kazi zipi umewahi kufanya. Hata hapa hapa bongo maeneo wanayojielewa elimu sio hoja. Vodacom waliwahi kuwa na CEO mwenye umri chini ya miaka 30 na alikuwa na shahada moja tu. Baada ya yeye kuondoka walikosa mtu hapa wakatafuta kutoka nje.