Kusoma sana sio kigezo cha utendaji: Nehemiah Mchechu ana degree moja

 
Poleni sana
 
Scheme ya Serikali sidhan kama inaruhusu mtu kuwa MD,DG, CEO wa Sehemu flani hali ya kuwa hauna MASTERS.

Labda kama alipewa favor..
Mimi mwenyewe nimeshangaa lakini hiyo ni kauli yake mwenyewe na akiwa Live kuwa nina degree moja na sina mpango wa kuongeza nyingine kwa sasa msije mkanikamata bure (to VC's) , alipozungumzia kuhusiana na vyuo kuwa na ukata
 


Mimi nina degree moja na sioni sababu ya kuwa na degree nyingine kwasababu hizi. Masters nyingi ni kwa wale ambao degree zao zilikuwa sio za kazi mfano degree ya sociology haiwezi kukupa kazi ya bank . Lakini kwa wale wenye degreee nzuri hauna sababu ya masters. Masters na PHD ni tafiti tu ambazo kwa mara nyingi hazina kabisa uhusiano na kazi. Hivyo degree moja ni kusoma sana!
 
Yule ana Degree moja na kipawa cha uongozi.Kipawa hakisomewi mahala popote bali unatunukiwa na Mungu!
 
JPM alimtumbua KWANINI?
Mama alimtumbua KWANINI?
 
Wa vivu ni wengi zaidi, mchukue mtu mwenye diploma muweke na mwenye degree uone kama wanaweza fanya kazi sawa
 
Wewe unamuona ni mtendaji mzuri? Mie naona kama anapita tu njia tofauti na iliyozoeleka maana uzuriwake sijauona. NHC alipandisha tu kodi akapata hela nyingi kuliko yule aliyekuwa anatoza kodi ya kawaida. Ila nyumba ziliendelea kubaki cvhafu tena chafu sana
 
Huyu yuko vizuri namkubali sana ni role model kwa utendqji mzuri na ubunifu mwenyezi mungu aendelee kumbariki. Japo pia ni vema tuendelee kuencourage watu kusoma zaidi na pia tumshawishi na yeye aandike hata kitabu ili yale mazuri yake yaendelee kwa vizazi na vizazi.
 
Na hasa anaposoma ili kupata heshima ktk jamii na sio kusolve matatatizo yao.. Mfano katibu wa maji alietenguliwa😂😂😂
Dah hii nchi ngumu sana, sasa mheshimiwa Katibu Mkuu wa Maji mstaafu ana baya gani? Si masuala ya siasa tu😂
 
Yaani senior officer tena msajili wa hazina awe na bachelor uyu jamaa inawezekana haelewi kilichokua kinazungumzwa
Itakuwa huelewi kinachozungumzwa au hujasoma kwa makini nilichoandika, nimeweka wazi kilichokuwa kinaongelewa na scenario husika na mhusika kataja live, maana hata ukisoma andiko langu nimebainisha wazi kushtushwa na kitu hiki. Unaweza pia kufuatilia historia yake unaweza kuja na kitu cha ziada ila mi nimemnukuu mhusika akiwa live kabisa.
 
Ni wazo zuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…