Kusoma sana sio kigezo cha utendaji: Nehemiah Mchechu ana degree moja

Sahihi labda awe alibebwa
Pengine utendaji wake ulimfanya kuaminiwa na kupewa nafasi kitu ambacho alikitumia vizuri,

swali la kujiuliza, je kwa sasa kuna umuhimu wa kuwaamini wahitimu wenye perfomance nzuri kwenye nafasi muhimu na za uongozi pasi na kuwa na elimu kubwa?

Au ndio tubaki kule kule haijalishi una perfom vipi inabidi kwanza ufanye kazi walau miaka kadhaa na uwe na elimu ya postgraduate ndio labda ufikiriwe kuaminiwa??
 
Kusimamia taasisi nakibongo wala hakuhitajiki shule kubwa,kwasababu uko maofisini kuna wasomi kibao lakini mambo ndo kama haya yakushindwa kujisimamia hadi tunaomba msaada kwa wengine kwa mambo ambayo yako ndani ya uwezo wetu.Madarasa mengi ila madudu kila kona.
 
Mkuu

Sijakuelewa

Indicators nzuri za nchi imeendelea ni number of PHDs per capita

Yaani leo unataka ku-play down roles za tertiary education in a nation?

Acha kupalilia ujinga kwa kuangalia exception moja ya Mchechu,hiyo ni exception kati ya watu milioni 60 ndugu!

Usije na ujinga eti PHDs hazina kazi ni ujinga eti kisa Mchechu ana akili?


Hebu kua serious!
 
Ngoja kwanza niwatafsirie vijana maana kwa hivi hawatakuelewa kabisa ndugu mleta uzi

Wakuu anachomaanisha mleta uzi ni kama vile kuwa na ndevu nyingi haimaanishi ndio uwezo wa kuichakata mbususu na kumridhisha demu

Haya kwako ndugu mleta uzi tuendelee na mjadala.
 
PhD isiyo na impact kwenye jamii haina maana hata kidogo.
 
Ukiona mtu anataja elimu yake, ujue ana inferiority complex. Huyo kusema ana kadegrii kamoja anaji console. Hata huyu Ramon Sanchez naona hana shule ni wale wale. Shule ndiyo mpango mzima!
Yes kuna umuhimu wa kuwa na shule, lakini je kuna umuhimu au la wa kuwaamini vijana ambao hawana shule nyingi katika nafasi nyeti za maamuzi ikiwa wanaperform vizuri??
 
Sisi wapambanaji degree moja tu inatosha kabisa lakini ukiona kichwa yako ina bachelor halafu bado unapwaya,hujiamini kaongeze elimu tumetofautiana vichwa wengine walivyomaliza form 4 au 6 wakaona wameshapata vitu vya kutosha kuweza kupambana na maisha na sasa ni matajiri wakubwa

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Aliekwambia PHDs hazina kazi ni nani? Mbona unamlisha mtu maneno ambayo hajayatamka? Ukiangalia vizuri nilichosena hapo je umejibu kile nilichouliza au umekuja na yako mwenyewe?

Nafikiri ingefaa ujibu kile nilichouliza then ungekuja na yako, kutofanya hivyo ni ujinga
 
Yes kuna umuhimu wa kuwa na shule, lakini je kuna umuhimu au la wa kuwaamini vijana ambao hawana shule nyingi katika nafasi nyeti za maamuzi ikiwa wanaperform vizuri??
Of course yes! Kwa vile si wote watakuwa na shule za juu. Shule ni pyramid kumbuka na tunategemea wenye PhD (za ukweli si za Mchongo) katika kila fani na katika kila nchi kuwa wachache!

Nafasi nyeti za maamuzi zinatakiwa watu wenye basic education ila wanaoweza kutumia wenye shule ili kutoa maamuzi. Managerial posts kama Urais si lazima mtu awe na shule kubwa ili a perform. Akiwa na shule akadhani yeye ni Alfa na omega atavurunda kuliko a siye kuwa na shule kubwa na akajitambua mapungufu yake. Shule kiuhalisia inakupa uwezo wa kuchanganua mambo na uwezo wa kujifunza mapya kwa haraka zaidi. Inakufanya uwe na kiu ya kujifunza zaidi katika maisha ya kila siku.

By the way shule huwa si general bali specific kwa fani na kipengele katika fani.
 
Ujuzi mwingi na maarifa tele hupatikana field au wengine husema kwa ground sio darasani !!
 
Mkuu

Acha kujifanya kukwepa unachomaanisha

Wewe unatukana waliosoma sababu tu umeona mwanadamu mmoja mwenye akili nyingi japo hajaenda shule ndio eti uwe mfano wa wanadamu milioni 60 katika nchi inayoitwa Tanzania

Ndio maana nikakupasha huwezi chukue exception ukageuza ndio rule!

Mchechu ni exception,watu kama yeye wapo ila ndio 1%

Na nchi ina watu milioni 60,for the masses the best way ni kusoma na kuelewa haya maarifa na kuweza kua productive nchi iweze kwenda mbele

Shida yako ni kutukana waliosoma sababu tu wana masters na PHDs ambazo Mchechu hana which its his decision,maana angeamua angekua na kama 1000 hivi.

Kujifanya unaepuka maneno yako mwenyewe ni unafiki unaweka hapa
 
Ni vizuri kama mtu atafanya hayo lakini bado haipunguzi umuhimu wa kujiendeleza kimasomo especially Kwa kitu ambacho unakifanyia kazi.....kama una uwezo wa kusoma ni vizuri kusoma Kuna kitu kipya kinaongezeka
Well said....Kwa kuongeza tu ukiona mtu anajifariji Sina elimu na nimefanya hili na lile mara nyingi Huwa ni mtu mwenye inferioty na anataka kuprove Kwa watu especially waliomzidi elimu kuwa yeye ni superior.Angekuwa na shule Inayozidi asingeongea Ivo angejua anafanya kitu ambacho ana uwezo nacho.
 
Kwa hiyo, unataka kusema kuwa na digrii moja ndiyo kuwa na akili? Sijakuelewa.
 
Jibu ni moja tu ndio au hapana, je vijana waaminiwe ikiwa wanaperfomance nzuri bila kuzingatia qualification za elimu?

Sasa unazunguuuuuuuuka, sielewi tabu iko wapi ukiamua kujibu then uje na hayo yako. Ila changamoto naona inakuja attack kwa mtoa mada badala ya hoja. Anyway, asante na nashukuru kwa mchango wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…