Nimesoma comment zote Mimi kwangu hakuna tunayefanana hata.
Kwangu Iko hivi...!
Ndoto yangu ilikuwa kuwa daktari na sasa nimetimiza baada ya miaka kadhaa kupita sikukata tamaa kamwe niliamini ndoto yangu siku moja itatimia na sasa imetikia.
1.Kidato cha sita nilichaguliwa PCM badala ya PCB na shule nilichaguliwa haikuwa na tahasusi ya PCB baba alifariki nikiwa kidato cha tano nikakosa wa kunipambania nihame shule yenye tahasusi ya PCB .Ikabidi nikubali kuendelea na PCM
Kibwagizo "MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"
2.PCM nikafaulu nikachaguliwa kusoma Electronics Engineering.Nikamaliza miaka minne wakati huo ndoto ya udaktari bado Ipo !
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"
3.Nikapata kazi kama mhandisi wa vifaa tiba (Medical Electronics Engineer) ,wakati naendelea kufanya kazi nakatafu chuo cha diploma in clinical medicine ,Nilisoma huku ninafanya kazi ya uhandisi haikuwa rahisi lakini nilijinyima muda na starehe nyingine zote.
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"
4.Uhandisi pamoja na kuwa ulikuwa unalipa lakini sikuwahi kuufurahi ,.Baada ya kumaliza diploma ya utabibu niliacha kazi ya uhandisi na kwenda serikalini na kuajiliwa kama" CLINICAL OFFICER"
Niliacha mshahara wa TSH 1.0M na kwenda kwenye mshahara wa TSH 0.5M
Wengi walinicheka sana na ndugu wengine waliniona tahira na wakaacha kuongea na Mimi ,.Wakasahau nilivyowalilia iliwanisaidia kuhamia shule yenye PCB wanakataa
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"
5.Nikiwa kazini niliomba ruhusa ya kwenda kusoma MD (5yrs) wakati huo nina mwaka mmoja kazini kama AFISA TABIBU (CLINICAL OFFICER ).Afisa utumishi akaniambia hawezi kuniruhusu kwakuwa sijatimiza vigezo ,nikaambiwa nitoe shilingi milioni 1 aniruhusu .Nikaenda banki kukopa TSH 12M nikachukua TSH 1M nikampa Afisa utumishi .TSH 10M zote nikalipa ada ya miaka 2,miaka mingine iliyobaki nitajua mbele ya safari
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"
6.Kwa shida sana MD nikamaliza ,nikaenda Internship nikarudi kazini nikapewa kwanza kuwa Mganga mfawidhi wa hospitali
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO
7.Kwa sasa ni PhD (candidate) , Neuroanatomy