GE2025 Kususia Uchaguzi ni Bora kuliko kuandamana hasa kipindi tukiendeacho sababu ni hizi

GE2025 Kususia Uchaguzi ni Bora kuliko kuandamana hasa kipindi tukiendeacho sababu ni hizi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
16,583
Reaction score
42,992
1. Pamoja na kwamba uchaguzi wetu umekuwa haramu siku zote ila kuandamana Kwa wakati huu inaweza leta matatizo makubwa.

A. Nguvu itatumika kubwa kuyazima hivyo kupelekea watu kuumizwa sana.

B. Kuna matukio ya kitaifa yatakayofwatana mfululizo kwenye wiki la mwisho la October na wiki la mwanzo la November.
I. Uchaguzi mkuu.
II. Mtihani wa upimaji FTNA.
III. Mtihani wa KIDATO Cha NNE.
Matukio yote hayo yatahitaji nchi iwe imetulia na wenye jukumu lao ni hao hao askari na Tiss.
Hivyo serikali haiwezi kukubali mazoezi yote haya ya kitaifa yaharibike hasa yanayowahusu wanafunzi ambao ni innocent. Hivyo nguvu kubwa itatumika at first glimpse of an eye. Nashauri kama maandamano ni lazima basi yangesubiri haya matukio ya kitaifa yapite. Nchi itulie hata serikali itaona tumeiheshimu lakini yakilazimishwa muda huu wakati serikali haijatulia na Iko kwenye panic mode inaweza Fanya yasiyotarajiwa na mwisho wa siku serikali ni serikali tu. Kila mchuma janga atakula na wa kwao mmoja mmoja.
 
Kuna muda nyumba Ili iwe borq inabidi uibomoe na kuijenga upya
 

Attachments

  • sativa255_-20251003-0001.jpg
    sativa255_-20251003-0001.jpg
    143 KB · Views: 29
Tuiheshimu serikali , yenyewe inatuheshimu ? Wangekuwa wanataka amani wangekubali reforms zifanyike. Kama kuandamana ni kufa basi tulishakufa zamani hata kabla ya kuandamana.
Watanzania wangapi wametekwa na kuuawa, familia ngapi zinalia zimepoteza ndugu zao?
 
1:wanaoweza kuhamasisha maandamano 90%

2: Wenye nia ya kushiriki maandamano 50%

3:Watakao andamana 3%😄
 
Mbona nasikia maandamano ni ya amani? Fujo na watu Kuumizwa vyatoka wapi tena?
Maandamano ya amani huku mnachochea vurugu?Lugha kama tutakinukisha vitafanya wajinga walete vurugu.
 
Kususia uchaguzi sijui kuandamana, vyote viko mjini tu tena nadhani ni Dar. Nilikua village last weekend, watu hawana hata habari. Wanasubiri siku ya kupiga kura. So kazi bado kubwa sana inahitaji kufanyika, yaani shida ni kwamba hii nchi ni kubwa sana, wewe utasema hufanyi wenzio wanafanya.
 
Back
Top Bottom