Inaweza kuwa ni ugonjwa mpya wa "hypersexual disorder" ambao baadhi ya wataalamu wa jukwaa hili wanataka uingie kwenye edition ya 13 ya Manual ya Diagnostic and Statistical Mental Disorders itakayochapishwa mwaka huu.
Inadawaiwa kuwa dalili za "ugojwa" huu mpya ni kama ifuatavyo:
- Kutumia muda mwingi kufikiria na kutaka kufanya ngono (sexual fantasies?).
- Kutumia behaviours za ngono kudeal na stress za maisha au anxiety, depression, kuboreka, nk.
- kutojali harm (both physical and emotional) kwa wale wanaokusaidia kwa namna moja au nyingine ku-deal na hilo tatizo.
- Kuwa distressed kwenye maisha yako ya kawaida.
Kwa upande mwingine inawezekana kabisa wala huna ugonjwa wa aina hiyo. In fact, wanaotaka kutengeneza ugonjwa wameupa jina ambalo ni too broad kiasi cha kushindwa kutenganisha ugonjwa upi unahitaji medical treatment na upi hauhitaji. Pia inawezekana ni njia ya makampuni ya madawa kutaka kujitafutua soko jipya maana wamejihusidha sana kwenye hii kampeni.
Unless kutaka kungonoka inaadhiri shughuli zako za kila siku, kuna uwezekano kuwa una high sex drive na unapenda kungonoka. That is good for you na huitaji kuchukua vekesheni ya kutongonoka zaidi ya kuandaa katripu na mpenzio kwenda kwenye kisiwa mtakachokuwa peke yenu na kufanya real au kutimiza imagination zako.
Lakini kama kutaka kungonoka inaathiri shughuli zako za kila siku kama kufanya kazi, kulala, ku-socialise, n.k. hii inaweza kuwa ni "sexual compulsivity". Hii ni tofauti na "sexual addiction" japokuwa baadhi ya madaktari hawazingatii kabisa hizo tofauti. Ukishafika hapo, then kuna umuhimu wa kuonana na mtaalamu wa hayo mambo kwa ushauri wa kitaalamu.
Lakini nadhani mara nyingi mtu anajihisi kuwa ni "sex addict" kutokana na kumhisi mwenzake au mwenzake kujihisi kuwa ni "undersexed." Ni kutokana na hiyo "sexual imbalance" basi mtu anaweza kujihisi au kuhisiwa ni "hypersexual". Tena mara nyingi unawezakuta kuna "power struggle" inaendelea ndani ya mahusiano na inapiganiwa kwenye kitanda.
Pia inategemea wewe na mwenzako mnavyoi-define sex. Unawezakuta defintion yako ya sex ni broad kuliko ile ya mwenzako.
Huu ni ushauri binafsi na na usichukuliwe kama ni ushauri wa kitaalamu. Ukitaka ushauri wa kitaalamu waone "professionals". Maumivu yakizidi, badala ya kusubiri ambulance, mwone "daktari" fasta.