Kutana na fundi rangi, kuna mengi ya kujifunza

Hv nikipiga hii kuna ulazima tena wa kupiga rangi ya kawaida?
Asante
 
Hv nikipiga hii kuna ulazima tena wa kupiga rangi ya kawaida?
Asante
Ndg hili ni swali zuri. Sababu kubwa ya msingi kutumia Rough Decor ni kwasababu ya uimara wa gamba lake ukishaipaka kwenye jengo, hii ninayoitangaza ina rangi moja tu, hivyo nashauri mtu kupaka rangi juu anayoitaka, japo wengine wanapenda jinsi ilivyo.
 
Asante kwa muongozo wako. Je kwa ramani kama hii inaweza kutumia ndoo ngapi hz zako?
Picha kwa hisani y mtandao
 
Pia tumepata Neema ya kufanya Mradi mkubwa kisiwani Zanzibar kuna Hotel kubwa inaitwa Marijani Hotel, majengo yote nje yamenakshiwa na Mimina Plaster. Na tumepewa Certificate of Appreciation.
 
Mkuu kwa nyumba ambazo zinaathiriwa na magadi hasa kwenye msingi ambapo unakuta rangi zinababuka na nyumba kumomonyoka hyo rough plasta n suluhisho?

Hii changamoto inanikabili. Natafuta namna ya kupambana nayo. Ukuta juu uko safi kabisa, imara, skimming imekaa vizuri, Ile rangi ya awali Iko sawa kabisa, shida baadhi ya maeneo Kwa chini ni kama ukuta au plaster inapukuchuka.



 
Ndg wewe upo Dar? Kama ni Dar water table ipo juu. Naomba tuwasiliane nikupe tiba,niliwahi kuweka mabandiko yanayohusu hilo tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…