Kutana na fundi rangi, kuna mengi ya kujifunza

Kazi iko poa.
 
Swali.
Kuna maeneo Yana magadi mengi na hivyo nyumba ikipakwa rangi,hiyo rangi hubanduka au kuwa na mabakamabaka,Nini chaweza kufanyika ili nyumba hiyo iwe nzuri rangi isiharibike?
 
Swali.
Kuna maeneo Yana magadi mengi na hivyo nyumba ikipakwa rangi,hiyo rangi hubanduka au kuwa na mabakamabaka,Nini chaweza kufanyika ili nyumba hiyo iwe nzuri rangi isiharibike?
Hapa tiba ni Ant nchunvi na yenye water proofing ndani japo mafundi wengi hawaelewi tiba na hii ni elimu adimu kwenye ujenzi. Ikiwa ukuta uneisha tafunwa hati plaster kupukutika au ukigonga ukuta unalia ngoma ni lazima utindue ukutane na tofali kisha unapiga plaster yenye Aunt chunvi na water proofing. Na ikiwa plaster bado ni imara tunapiga msasa sehemu zilizo athirika nakupaka hiyo dawa.

Kifupi ukanda wa pwani kama vile Dar, Lindi, Zanzibar, bagamoyo na Tanga kitaalam kiwango cha maji kwenye Ardhi kipo juu yaani water Table iko juu mno, na sehemu kubwa msingi na tofali kuanzia kazi ya kwanza pengine mpaka ya 4 zote zinakuwa na unyevunyevu, hivyo huo unyevunyevu unakuwa na kiwango kikubwa cha chunvi ambayo inakuja kutafuna Cement ambayo ndiyo kiunganishi.

Na maeneo ya mikoani hao wana tatizo la magadi yaani chunvi ambayo ipo kwenye hali ya hewa. Maumivu yakizidi muone Daktari 0766111212.
 
Tupo pamoja,hivi kabla ya kupiga rangi kwa kuta zilizoliwa na fungus unatumia nini kuzuia maji kutoharibu kuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…