Ng'wanamangilingili
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 5,778
- 4,859
Usirembe maneno katumbuliwaHuyu mama wakati mwingine nadhani anasikiliza sana maneno ya mitaani. Chalamila hakutumbuliwa bali uteuzi wake umetenguliwa kulingana na matakwa ya Rais lakini sababu kubwa ilikuwa ni kutengeza nafasi ya mama Buriani ambaye alipoteuliwa kuwa RAS mitaani watu walisema kuwa amepewa cheo kidogo kulingana na hadhi yake hasa ukizingatia aliwahi kuwa waziri na balozi. Sasa ilikuwa ama Hapi au Chalamila aachie ngazi ndipo mpira ukamwangukia Chalamila. majina hayo mawili ni yale yaliyokuwa yanazungumzwa sana mitaani, na hhapi alikuwa na bahati sana kwani yeye bado ni target namba moja hasa ukizingatia jinsi alivyomchambua sana Membe wakati ule simu ya membe ilipowekwa hadharani.
Kutumbua ni neno tuliloletewa kuwa kiongozi akifanya makosa kazini linakuwa kama ni jipu ambalo lazima litumbuliwe; Magufuli alitumbua wengi sana wa namna hiyo. Utenguzi ni kuondolewa kwenye nafasi fulani kwa sababu yoyote ile isiyotakana na utendaji wa kazi. Hiyo ni pamoja na kumtoa kitengo kimoja na kumpeleka kitengo kingine, analazimika atengua uteuzi kwenye kitengo cha zamani ndipo amteue kwenye kitengo kipya. Kitengo kipya kinaweza kuwa ni jobless!
Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app