Hoja dhaifu yanii huyo Josephine ategemee kirahisi tu hivyo kuwa Slaa atakuwa rais na yeye awe first lady?For the record slaa ndio alishauri lowassa apokelewe Chadema na kwenye mapokezi ya lowasa chadema slaa alikuwepo.
Upepo ulibadilika baada ya mama josephine kuhisi ataukosa u first lady , nadhani ni yale maongezi ya pillow talk usiku kwa wanandoa ndo slaa akabadili msimamo wake juu kwa juu na kupindua meza.
To me, kutenguliwa siyo issue, ISHU NI SABABU YA KUTENGULIWA.
Unafiki sio kitu kizuri.
Mzee slaa aliwasaliti CHADEMA mbele ya JPM kwajili ya tumbo lake, leo hii tena wapo pamoja kwenye jukwaa la kisiasa.
Mbowe na Lema wanapaswa kujitafakari sana, sio kwamba wanachadema wamesahau ila ...
Ni ajabu mzalendo anavuliwa hadhi, wauza nchi wameigeuza Ikulu pango la walanguzi na wapo wanapeta.
The crux of the matter!To me, kutenguliwa siyo issue, ISHU NI SABABU YA KUTENGULIWA.
Slaa aliwasaliti viongozi wa chadema kipindi cha awamu ya 5 na hivyo kupelekea viongozi wa chadema kuwa kwenye kipindi kigumu haijawahi kutokea kwenye maisha yao ya siasa.Kwamba alitakiwa ampigie kampeni Lowassa ili awe rais wa Tanzania kupitia chadema?
Mbona hata kina mbowe waliingia ushirika na ccm na jana wamesema ushirika umevunjika.Always TL apewe heshima yake, ushirika na wachawi huwa haudumu. Dr slaa alikuwa na option moja tu, ya kuendelea kuwaunga mkono milele ama msukosuko wowote unaomtokea hauepukiki.
Viva Tundu A. Lissu.
Mama nchi imemshindaDr Wilbroad Slaa ni mpinzani wa siku nyingi, toka kuanzishwa siasa za vyama vingi. Dr Slaa ni kama yule mchezaji katika timu, si wa kutegemewa sana, lakini anaweza kutokea nyuma na kufunga goli la ufundi.
Tunaikumbuka List of Shame.
Alopoteuliwa kuwa Balozi wengi tulishangaa sana, lakini ndo hivyo, tumikia kafiri upate mradi wako.
Awamu hii ya Sita akiwa Balozi Dr Slaa kaingia na pasi aliyoipata ya mpira wa DP World Akiwa kavaa jezi yenye nembo ya Balozi.
Dr Slaa vyenga kapiga, na alikuwa anaelekeo eneo la hatari box la timu ya serikali.
Sasa serikali ikachanganyikiwa, ikishangaa mbona Dr Slaa anakuja kavaa jezi yetu? Wakamvua jezi, lakini mchezaji ni yule yule, Dr Slaa.
Kwa upande mmoja serikali ya Mama Samia imejiumbua kwa kiasi, haipendi kuumbuliwa, iko vindictive!
Kilichomtokea Job Ndugai tunakikumbuka, serikali iko vindictive.
Tunakumbuka utawala wa mzee wa Chato.
Kuna mtu anaitwa Prof Mark Mwandosya.
Alionyesha hadharani kutoridhishwa kubambikwa kesi mtu, tena mpizani, anaitwa Sugu.
Yaliyotokea ni kama kagusa wire wenye umeme live.
Akafukuzwa uenyekiti wa Bodi za vyuo vikuu viwili, MUST- Mbeya na Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Vindictiveness.
Hii tuliyoiona si dalili njema saana.
Kina Mbowe walisamehewa uhaini na kualikwa siku hiyo hiyo Ikulu.
Tundu Lissu pia.
Sipendi wapinzani wanavyotukana, but you guys have better watch out.
Kwa mama, this is a sobering moment, aendelee kuwavumilia wapinzani, na tusirudi zile siasa za kubambikana kesi.
Mama Samia, stay the moral high ground.
Mwanasiasa akikubeza, chukua yale ya maana kama ushauri, mengine yadharau na yatupilie mbali.
Kuna sku aliyetukana kijinga atakuhitaji tu, na lazima ataomba radhi tu.
Vindictive politics no!
Alamsiki.
🤣🤣🤣😂tuna safariiii ndeeefu sanaThe fact kuwa slaa aliamua kuuza utu wake kwa hao ma ccm mwaka 2015 na akapata tangible rewards pamoja na huo ubalozi, wala simhurumii kwa haya ya kudhalilisha yanayomtokea .
Tungekuwa mbali sana kama Dr slaa asingesaliti upinzani mwaka 2015.
Kama ubalozi ni hadhi tu, kuepusha lawama kwenye mgogoro wa bandari Slaa angeachwa tu maana hiyo hadhi sio meno ya kung'atia!Samia ameamua kuwakumbatia wasaliti wanaopigia chapuo ule mkataba wa hovyo wa bandari, na kuwatosa wazalendo wanaoulaani ule mkataba wa hovyo wa bandari kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Hiyo "hadhi ya ubalozi" Dr. Slaa asingeenda nayo kaburini, wala asingeingia nayo peponi kama angefika huko, wala hakuwahi kuwa na mabawa baada ya kupewa hiyo hadhi, kusema ndio akaanza kuruka angani...
Ni hadhi ya kujidanganya tu hapa ulimwenguni, kama ulivyo Urais wenyewe anaoutumia kuwapa wajinga wenzake vyeo, na kuwavua werevu vyeo, watanganyika tunamshangaa tu kiongozi aliyepoteza muelekeo na asiyeona aibu kuzidi kupotea.
Hiki alichokifanya Samia, ndio kinazidi kuthibitisha alivyo na roho mbaya kwa watanganyika, mwanamke dikteta, asiyetaka kuwasikiliza wale anaowaongoza, anayejifanyia mambo yake kwa manufaa ya wajomba zake wakiarabu.
The fact kuwa slaa aliamua kuuza utu wake kwa hao ma ccm mwaka 2015 na akapata tangible rewards pamoja na huo ubalozi, wala simhurumii kwa haya ya kudhalilisha yanayomtokea .
Tungekuwa mbali sana kama Dr slaa asingesaliti upinzani mwaka 2015.
Mkuu niseme hukufutatilia !! lowasa lilikuwa ni stepping stone .kwa siasa za chadema kwa sababu lowasa alikuwa na watu. Mind you hata magu kupata nafasi ya kugombea urais ilikuwa ni sababu lowasa alionekana ni tishio hata huko ccm hasa team msoga.
Kilichokuja kumbadilisha Dr slaa ni kuwa mama josephine aliona kwa ile move anaukosa u first lady akamzingua Dr ,na Dr naye akaja kuizingua Chadema .
Mama alianza vizuri, asiiache tu nchi ikaingia kwenye autopilot na kuwaachia maamuzi magumu washauri wa karibu.Mama nchi imemshinda
Kidata siyo tu kuwa alitenguliwa, baadaye alivuliwa hafhi ya ubaloziHuelewi kitu, Dr Slaa hajatenguliwa kwenye nafasi ya uwakilishi katika nchi fulani, bali kaondolewa hadhi ya kuwa balozi.
Kutokana na muonekano wa suala zima, ni kisasi. There is no way itakuwa kuna jingine.The crux of the matter!
Je ni kisasi au kuna kitu kingine?
Mimi naona kama Mhe Tukijaaliwa nae itakuwa hakubaliani na issue ya bandari ndo mana kachaguliwa msaidizi. Hamjafikiria hilo?Hii inaonyesha Samia hana ngozi ngumu, ana visasi na anadhani mtu akiwahi kuteuliwa na rais basi hiyo ni favor na kwamba mtu huyo hatakiwi kukosoa, kuonya na hata kupinga mambo ya hovyo.
Dr Slaa kanyang'anywa ubalozi kwa sababu kapinga kwa nguvu zote nchi yetu kuuzwa kwa mwarabu, na kwa kuwa kawa kiongozi kwa vitendo kukataa udalali wa nchi yetu.
Tutamrudishia hadhi yake Samia akiondoka madarakani.
Ni ajabu mzalendo anavuliwa hadhi, wauza nchi wameigeuza Ikulu pango la walanguzi na wapo wanapeta.