Kutenguliwa ubalozi Dr W Slaa: Mnaliona tatizo ninaloliona?

Wanasiasa kwa visasi acha tu
 
Wala sishangai, sikuwahi kuutambua huo ubalozi, alipewa ubalozi "KIHUNI" kavuliwa ubalozi "KIHUNI"
 

Umenena lililojema.

Ubinafsi unaendelea kutukwamisha watanzania na wana wa Afrika.



Ubinafsi ulisababisha ukoloni ukafanikiwa kwa asilimia 2000 kiasi kwamba mpaka sasa bado tunaendelea kuteseka nao japo umebadiri sura ila mbinu ni zile zile na matokeo ni yale yale.





Unity should be our priority and all else shall fall into place.
 
The crux of the matter!
Je ni kisasi au kuna kitu kingine?

Lakini…..Doctor Slaa yupo nje kwa dhamana sindio?

Kama ni ndio, bado ni mtuhumiwa wa Uhaini na kama ni mtuhumiwa wa Uhaini turudi nyuma tuangalie sheria za public service zinasemaje? Na sheria zinazoiongoza mamlaka ya Urais zinasemaje?


Ama ile kesi iliyomuweka ndani majuzi imefutwa na Jamuhuri?
 

“Huyu mzee hafai kusamehewa milele”

Kwa sababu wewe ni Mungu ama mshauri wa karibu wa Mungu?


Siasa tu hizi, husivuke mipaka.
 
Toka tupate uhuru ni huu ndio mna Rais mwenye akili nyepesi kumzidi hata kipepeo, mwanamke ni kiumbe sifuri na huyo Rais wenu anadhihiri na ataishia 2025, yeye ni wa mpito tu

“Mwanamke ni kiumbe sifuri…..”

Mama yako aliekuzaa yumo kwenye kundi hilo?



“Rais mwenye akili nyepesi kumzidi hata kipepeo…”

Ndio Rais wako wewe, nchi na watu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka pale utakapotaarifiwa tofauti.
 
Dr Slaa wakati vinaanzishwa vyama vingi alikuwa Ccm.

Dr Slaa amepokelewa Chadema akitokea Ccm na sasa anarudi Ccm.

Unafki ndio unaomsumbuwa huyu Mzee, nadhani Josephine ndiye anayemjuwa vizuri.
 
Tunachoheshimu ni mfumo wa chama pamoja na Katiba yake na siyo mtu.
 
 
Aliwageuka kwa sababu ya issue ya Lowassa?
 
VIENNA CONVENTION 1961 inaanza kumlinda mtu huyo, yaani anapata upendeleo & kinga (privileges & immunity) za KIDIPLOMASIA.

Lakini, KINGA hii inaweza kuondolewa kwa muda, na wakati wowote na nchi yake (sending state) – inaitwa "WAVER"; Article 32 ya VIENNA CONVENTION, 1961. Isipokuwa, "WAVER" hutokea tu pale ambapo "receiving state" inapeleka maombi kwa "sending state" kwamba Balozi aondolewe KINGA ili atoe ushahidi mahakamani, akamatwe au ashtakiwe kwa kosa la jinai (under the local criminal jurisdiction). Nchi ya kituo cha kazi cha Balozi haiwezi kumnyang'anya Balozi kinga au haki hizo za KIDIPLOMASIA kama Balozi huyo si raia wake.

Hata hivyo, Balozi akimaliza muda wake wa utumishi nje ya nchi yake, au kama amerudishwa nyumbani (recall), pale tu anapoondoka kwenye nchi ya kituo chake cha kazi, anapoteza KINGA hiyo; Article 39(2) ya VC. Lakini, bado mtu huyo ataendelea kutambulika na hadhi ya Kibalozi anaporudi nyumbani. Ataitwa "Balozi mstaafu", kama anavyoitwa Rais au Waziri au Jaji mstaafu.

Under common law jurisdiction & Diplomatic law, Rais Samia ana MAMLAKA ya kumwondolea mtu "immunity" ili ashtakiwe kwa kosa la jinai, lakini Rais hana mamlaka ya kufuta "HADHI YA UBALOZI" wake kwa sababu hadhi hiyo inatokana na sheria za Kimataifa na Rais Samia hajapewa UWEZO wa kuingilia sheria hizo, isipokuwa tu kama sheria hizo zingetamka wazi! Kwa VIENNA CONVENTION ya 1961, au sheria zingine hazijatoa mamlaka hayo kwa Rais wa nchi yoyote.

Hakuna, kwenye sheria zetu za ndani au za Kimataifa umewekwa utaratibu wa kunyang'anya hadhi ya Ubalozi ya mtu, isipokuwa tu kumwondolea kinga ili ashtakiwe kwenye mahakama za nchi ya kituo chake cha utumishi. Hili suala hapa nyumbani, linafanyika KISIASA tu.

Hivyo, kwa msimamo huu wa kisheria, Dr. Willibrod Peter Slaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…