Kuteswa kwa Kibanda: Ridhiwani na Nape matatani!

Kuteswa kwa Kibanda: Ridhiwani na Nape matatani!

alizungumza kama.1.mtoto wa rais.2.mwana ccm.3.mwananchi wa kawaida.tujadili haya pia


wana jamii tuwe makini,mtu anaweza kuingia kwenye FB kwa ID yoyote,sasa ni kweli tunayemjadili ni mtoto wa mkuu wa kaya?napata shaka sana jinsi tunvyofanya wengine ata wanfikia kumdhiaki mtu mwenye jina la Rizone bila ya kuwa nauhakika.naomba wanajamii nipeni ushahidi kama ridhiwan kikwete wa FB ndiye mtoto wa mkuu na wala sio mtu kajisajili na id iyo ili tu kumchafua muusika
 
TUKIO la kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Absalom Kibanda usiku wa kuamkiaJumatano wiki hii, limechukua sura mpya baada ya mtu aliyejitambulisha kama Ridhiwani Kikwete akitumia ukurasa wake wa mtandao wa facebook kutoa maneno ya kejeli, akihoji kama nae ametekwa na Ikulu.

Mbali na Ridhiwani, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye,naye alitumia mateso ya Kibanda kufanya propaganda chafu, akitoa kauli inayoonesha “anawajua” waliomtesa.

Ridhiwani aliandika: “Je, hii nayo ni kazi ya Rama (Afisa Usalama wa Taifa) wa Ikulu?”

Rama Ighondu ndiye alitajwa na MwanaHALISI kuhusika na mateso ya Dk. Steven Ulimboka mwaka jana.Kauli hii ilichefua kwa kiwango kikubwa viongozi wa juu wa New Habari, kampuni anayofanyia kazi Kibanda, kiasi cha kumfanya Afisa Mtendaji Mkuu, Hussein Bashe,kuhoji chanzo chake.

Bashe ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, alikwenda mbali zaidi na kuandika maneno makali dhidi yaRidhiwani:“Huwezi kuleta kebehi ya namna hii. Inaonyesha namna gani hufahamu nafasi yako katika jamii.

Funga mdomo kabisa kwa sababu unajaribu kutukana hisia za watu.“Futa kauli yako ya kijinga ya namna hii, hatuwezi kuvumiliakebehi ya kiwango kikubwa namna hii; umelewa madaraka ya kuwa mtoto wa rais, na kudanganywa na hayo mageti ya ikulu, na kudhani unaweza kuleta kebehi na dharau zako katika kila jambo…

“Nakuonya iwe mwanzo na mwisho;usilete kebehi katika jambo hili.Nakuonya,nakuonya, nakuonya usijaribu! Tumekaa kimya…”

Tangu Ighondu alipotajwa na MwanaHALISI kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka, serikali haijamkamata wala kumhoji. Kauli ya jana ya Ridhiwani kuuliza kwa kejeli kama Kibanda naye aliteswa na watu wa Ikulu, imeibua upya hisia mchanganyiko kuhusu sakata hilo, huku watu wengine wakisema mtoto huyo wa rais anamponza baba yake kwa kutokujua wapi atoe kauli gani.

Baadhi ya waliozungumza na gazeti hili wakionesha kukerwa na kauli ya Ridhiwani, walisema mtoto huyo wa rais anafurahia mateso ya wananchi kwa sababu hajui shida zao, na amelewa madaraka yasiyo yake.Wengine wanaojua kuwa Kibanda alimfundisha Ridhiwani alipokuwa anasoma Shule ya Sekondari Shaaban Robert, Dar esSalaam,walisema hii ni dharau na kejeli iliyopitiliza, inayofanana na ukatili.

Mmoja wao alisema kauli ya Ridhiwani inatokana na kujua udhaifu au upendeleo wa serikali,na kwamba baba yake (rais) hawezi kumchukulia hatua. Wapo piawaliofikia mahali wakasema: “Mtoto huyu kuna kitu anakijua…au kuna kitu anajaribu kuficha.” Katika hali isiyokuwa ya kawaida.

Nape naye alitumia ukurasa wa facebook kulijadili suala hili katika muktadha wa kipropaganda, akitaka kuwahusisha watu kadhaa bilakuwataja majina.

Aliandika hivi: “Hili la kutekwa na kupigwa na kuumizwa kiasi hichi (hiki) kaka yangu Kibanda, kila nikilitafakari maneno ya waliosemahakutatawalika na makala za Kibanda mbili au tatu za mwisho kabla ya kuhama chombo cha habari kabla ya anachofanyia kazi sasa vinajirudia kichwani mwangu sana!”

Kauli hii inaakisi maoni kadhaa yanayosambazwa tangu juzi katika maeneo na mitandao kadhaa,yakiwanukuu baadhi ya makada namashabiki wa CCM ambao wanasema wanalenga kuinusuru serikali isihusishwe na tukio la kutekwa kwa Kibanda.

Huku wakijua kuwa Kibanda aliacha kazi Free Media na kuhamia New Habari kwa hiari yake, kama mwajiriwa yeyote, kama alivyowahikuacha kazi New Habari, na Mwananchi kabla hajajiunga na gazeti hili, Nape na wenzake wamediriki kupandikiza propaganda kwamba kuteswa kwake kuna mkono wa mwajiri wake wa zamani.

Gazeti linajua, na Kibanda anajua,kwamba hana uhusiano mbaya na mwajiri wake wa zamani, bali amekuwa akiwindwa na kuandamwana watu wenye mamlaka makubwa sana katika nchi hii kwa muda mrefu kwa sababu za msimamo wake wa kisiasa katika masuala
kadhaa.

Amepata kuitwa na kuonywa mara nyingi dhidi ya msimamo wake katika masuala ya kitaifa, na hasa kwa msimamo wake na makalazinazoonekana wazi kumuunga mkono kigogo mmoja anayechuana na wenzie ndani ya CCM katika kinyang’anyiro cha urais 2015.

Gazeti hili linajua pia kwamba hata mawasiliano ya simu ya Kibanda na baadhi ya wahariri wenzake (na wa gazeti hili wamo) yanafuatiliwa kinyume na sheria.

Kauli yake mwenyewe juzi akisimulia mkasa huo kwa waandishi wa habari kabla hajapelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, inadokeza aina ya watuwaliomtesa.

Kibanda alisema kuwa alimsikia mmoja wa watesi wake aliyekuwa na silaha ya moto akikoki risasi na kisha kumuuliza mwenzake, “afande, tummalize?”

Wananchi waliopiga simu chumba cha habari jana baada ya kusoma kauli za Nape na Ridhiwani walisema nukuu hii ya Kibanda ndiyo inawapa kiwewe watu wanaodhani serikali inaweza kuhusishwa na tukio hili dhalimu.

Mmoja wa waliojibu kauli za Nape na Ridhiwani pale pale mtandaoni,aliandika kwa hasira: “Mna dola na all machineries (taasisi zote)mnashindwa nini kuwakamata na kuwachukulia hatua? Lini mtaacha propaganda za kimisukule? “Mwigulu (anadai) anao mkanda,wewe pia unataka kutuaminisha kuwajua wahaini wa Kibanda. Kama kweli acha upuuzi, peleka maelezopolisi.

Mmeanzisha propaganda za udini, na bado tu hamtuonei huruma tusio na pa kukimbilia?”

Source. Tanzania daima.

SAA ZA UTAWALA WA Ccc meu UNAESABIKA BILA WASIWASI.NAAMINI 2015 UTAKUWA MWISHO,KAMA MUNGU AISHIE MILELE ASIVYO BADILIKA BASI Ndivyo awezi kuwaacha wanyonge wakiangamia.Nape na Ridh1 SI WAKWELI.TUNAAMINI SAA YA UKOMBOZI Inakalibia.
 
wana jamii tuwe makini,mtu anaweza kuingia kwenye FB kwa ID yoyote,sasa ni kweli tunayemjadili ni mtoto wa mkuu wa kaya?napata shaka sana jinsi tunvyofanya wengine ata wanfikia kumdhiaki mtu mwenye jina la Rizone bila ya kuwa nauhakika.naomba wanajamii nipeni ushahidi kama ridhiwan kikwete wa FB ndiye mtoto wa mkuu na wala sio mtu kajisajili na id iyo ili tu kumchafua muusika

Ww cjui vp,do u think wa2 wamekurupuka 2?
Halafu ww u dont knw rizmoko eeh!?
 
Shame on all those involved in the torture of Mr. Kibanda., WATU WAKISHA CHOKA, KIONGOZI MWENYE BUSARA HUSIKILIZA NA HUTAMBUA KWAMBA KUACHIA KWA HIARI NIKUTUNZA HESHIMA SIO YAKE TU BALI HATA YA WALE WALIO AMINI JUU YAKE. LAKINI KATIKA YOTE HATUCHOKI KUSEMA ILIYO KWELI, - HATUTA COMPROMISE INTERGRITY YETU KWA HOFU WALA WOGA WA MTU YOYOTE YULE!! SI HATA USALAMA WA TAIFA.

Justice MUST prevail against all it adversaries.
 
.......hii miamala(accounts) ya mitandao ya kijamii nayo ni vema ikawa inasajiliwa (kuhalalishwa).......vinginevyo tutaumiza vichwa vyetu kwa habari zisizothibitishwa......ni wazo tu......
 
Hivi haka kajamaa mnakazungumzia hapa ndio kale kadogo kabrazameni kalikuwa kanatufanyia fujo upanga,masaki hadi disco bills huku kanatembea na maputo yake yale ya block nanihii pale Moroco ambayo mengine siku hizi eti nayo madiwani?aisee uongozi huu siku hizi ni cheap hivi?nnavyokijua kile kichwa sishangai kuona kasababisha tayari!tena kamejitahidi maana kangeachia makucha yote mbona dadi angekuwa impeached saa hizi!dah!jamani,chichiemu hoi,ah nimekosea,chichiemu hoyee!
 
Nape na riz one wote walipata dv 4 unategemea wataandika nini cha maana. ila ninawasifu waliocomment wamewapa ukweli wao hapohapo!

Huyu mtoto kapagawa na hela wanazopiga serikalin,anatoa kauli ambazo hajui impact yake kwenye jamii,mimi namshauri aendelee kushinda pale MAHABA BEACH na wapambe wake pale wanapopanga mikakati ya kuendelea kuwanyomya watz,usifir unavyokuwa kwenye hilo shangingi jeusi ndani tinted hatukujui tena kuna siku utaonja joto ya jiwe,eneo la la wananchi hekari 3 mlizomilkishana na mzee majogo pale baharini tunajua,sasa hivi una nguvu kwa sababu mshua yuko kazini,lkn mambo yako yote yako uchi,usiwaongopee watz,utesaji wote wewe,baba yako na hao wanaowalamba miguu wanajua,Nape katika hili wee ni kunguru tu unasukumwa na tumbo zaidi kuliko hoja...
 
Ni bora tukatawaliwa na kichaa kutoka chama chochote kuliko professor awaye yote ndani ya ccm
 
Huyu mtoto kapagawa na hela wanazopiga serikalin,anatoa kauli ambazo hajui impact yake kwenye jamii,mimi namshauri aendelee kushinda pale MAHABA BEACH na wapambe wake pale wanapopanga mikakati ya kuendelea kuwanyomya watz,usifir unavyokuwa kwenye hilo shangingi jeusi ndani tinted hatukujui tena kuna siku utaonja joto ya jiwe,eneo la la wananchi hekari 3 mlizomilkishana na mzee majogo pale baharini tunajua,sasa hivi una nguvu kwa sababu mshua yuko kazini,lkn mambo yako yote yako uchi,usiwaongopee watz,utesaji wote wewe,baba yako na hao wanaowalamba miguu wanajua,Nape katika hili wee ni kunguru tu unasukumwa na tumbo zaidi kuliko hoja...

He has Presidential Immunity as President's Offspring.

 
Wakuu,
kuna mabandiko kadhaa yaliletwa hapa baada ya Kibanda kupigwa vibaya...
na 1 ni reaction ya riziwan kukashifu kwa kuisemea ikulu...
hiv kuwa mtoto wa rais kunafanya uwe na mamlaka ya kuitamkia ikulu?
ni kwel nch inaongozwa na familia ya j.k?
 
Back
Top Bottom