Kuteua watu kabla ya kuwajulisha: Wapi kwingine duniani wanafanya hivyo?

Exactly. Hayo👆👆 ni Mawazo na Fikra zilizosheheni Hekima na Busara. Ubarikiwe sana kiongozi.
 
Huoni katika utawala huu machawa wamekua wengi kupita kiasi na katika utawala huu ndio mapambio yana imbwa kwa wingi sana
Ninashangaa kumeibuka hata misamiati mipya ya "Kuupiga mwingi",....Machawa....etc.....
 
Shule ikikushinda unasoma mzumbe na stanford university,au unasikiliza wanasiasa ?Wanasiasa wapo kazini kwao.
Mzumbe umeona ndio benchmark?

Mbona hata Nape naye kasoma Mzumbe hahaha!

Na baadaye tukaambiwa kaenda Bengaluru!

Ila elimu zao halisi zinajulikana.

Leo hii ukiniambia academic background labda ya Professor Mark Mwandosya na Samia ipi ina mashaka naamini jibu utakuwa nalo.
 
Kuna theories kwenye spin coding zinatumika, ubunifu mzuri ndio msingi wa ufanisi kwenye kazi.

Ligi imesimama, raia wajuvi na international media zimeripoti kuhusu baadhi ya matukio ya kiongozi wa nchi, wengineo wakaanza kuhoji kwanini imekuwa hivi na vile, mara nyingi mpira ulitumika kuwaondoa kwenye reli ya majadiliano ya kisiasa na utendaji wa serikali, binadamu nyinyi mkaanza kufuatilia alichokisema ahmed ally na ally kamwe, sasa jamaa wako likizo ya muda, ko kuna mbinu nyingine mpya imetumika kuwazubaisha kutoka kwenye pointi yenu ya korea, ndio mnaanza kujadili kuhusu mfu na kurugenzi ya mawasiliano, hivi inawezakana vipi kwa taasisi kubwa ya teuzi isifahamu kuwa mteuliwa amefariki au yu hai, inaingia akilini kweli,,,,???? hapa na haiwezekani, kilichofanyika ni agenda setting au framing ili msiendelee kujadili na wasiyoyataka muyajadili au kuhoji.

Ila hayo ni mawazo yangu sio ukweli au uhalisia wa mambo yalivyo.
 
Jamaa vyeo vinamfuata hadi peponi. Bahati iliyoje
 
Kama shida ni wasaidizi nashauri kwenye hili wajiuzulu
 
Na uhamisho ulikuwa unasaidia nini na kwa nini siku hizi haupo? Tuliozoea kufanyakazi private sector tunashangaa unachokisema eti fatigue etc etc! Tatizo la utumishi wa umma Tanzania na nchi nyingi za Afrika ni kutokuwa na malengo endelevu na upimaji wa utekelezaji wa malengo hayo na ufanisi wa kazi kwa nia ya kujua changamoto na namna ya kuzikabili ikiwa ni pamoja haya uliyoyataja.
 
Wakipigwa spana na kina Tundu Lissu huko kwenye majukwaa ya kisiasa mbele ya wananchi, kina chiembe na Lucas Mwashambwa na chawa wenzao wanaanza kulialia na kuzusha kuwa 'ooh, Rais na wananchi wanatukanwa.!', really?

Hivi unaweza vipi kumtukana mtu ambaye yeye mwenyewe tayari keshajitukana na hawa wengine wanakwoti matusi yake mwenyewe?
 
Hii 👇👇👇 ndo ingekuwa major criterion halafu mengine yakawe ni kama
chachandu tuu.
"Uzoefu wa muda mrefu na uwezo mkubwa wa kiutendaji kila siku ndo vinatakiwa kuwa vigezo vya mtu kushika nafasi fulani."
Halafu sasa ndo ujumlishepo/Uongezeemo na Elimu. Hili huja kwa kuzingatia kwamba mteuliwa atakwenda kuwaongoza wenye kuanzia darasa 0 hadi PhD
Kwa mantiki hiyo, ni lazima naye awe na walau Salio la kutosha kielimu.
 
Haya ni mapungufu makubwa ya kumfanya rais kuteua kila mtendaji. Baada ya ziara ya Korea, na kusainiwa mikataba ambayo imeleta sintofahamu tulitarajia kauli yake ili kurudisha imani kwa wananchi, badala yake anateua marehemu kuongoza. Still kuna chawa wanatetea kwa nguvu zote mfumo wetu wa utawala.
 
Mwandosya kusoma dit hakuna mashaka ,Samia kusoma mzumbe kuna mashaka ,kwa akili hiyo hongera sana.
 
Mkuu, Uhamisho unafaida nyingi;
1. Kumwondolea mtumishi Kuchoka kukaa sehemu moja kwa muda mrefu na kule kuzoeleka na wale anaowatumikia ref.Familiarity breeds contempt. Walio chini yake hawaoni tena jipya kutoka kwake-wamemzoea.
2. Kukaa eneo moja kwa muda mrefu e.g. zaidi ya 3-5yrs, katika hali ya kawaida kibinadamu lazima utakuwa kuna watu wasiokukubali (maadui/wapinzani). Hawa maadui wanaweza kuwa wameshajijenga vya kutosha na hivi kuanza kukuharibia kazi na utu wako.
3.Ukiyazoea mazingira kwa muda mrefu kama kiongozi au hata mtumishi wa kawaida unajikuta umeridhika na hali iliyopo huoni tena Fursa za Maendeleo zilizopo i.e. Unakuwa ni Mwenyeji wa hapo hapo. "When in Rome do as the Romans do" Hili liko wazi mno e.g. maeneo yenye mambo ya Ushirikina. Naturally unajikuta na wewe unaanza kuyaogopa au kutishika nayo kumbe hamna kitu.
4. Kwa baadhi uhamisho ni mojawapo ya Motivation.
Hoja ya kutokuwa na malengo endelevu na Upimaji wa Utekelezaji.....Sio kweli.
Watumishi wengi Serikalini wanajua hilo(kwa kusomea e.g. fani ya Maendelo ya Jamii) au wameshiriki mazoezi ya Kijamii O&OD , Participatory Rural Appraisal -PRA au Wameshiriki Mafunzo ya Muda mfupi (Seminars -e.g. LFA Logical Framework Analysis, Popular Partipatory Approach-PPA n.k.)na wana uzoefu mwingi. Kinachokwamisha hapo ni Uwezeshwaji in Time na Commitment ya Uongozi. Kumbuka Kila kijiji hapa Tz (vijiji 12,317) vimefanyiwa/ vimewezeshwa kufanya mchakato wa kuibua Fursa na Vikwazo ktk maendeleo ya kijiji (O&OD) na kujiwekea Vipaumbele(Priority) vyao na. 1 hadi 3.
 
Kweli hayo ni mapungufu. Kama Rais atateua katika kila nafasi cjui itakuwaje - Hachoki? na hapo ni rahisi makosa kutokea.
Mwanzoni Rais aliteua Mawaziri na Makatibu wakuu. Mawaziri/Makatibu wakuu wakawateua viongozi wengine DED, DC etc. Mifumo ya Kijeshi huko Wanajua wenyewe mie siijui.
Kwani ndani ya Mfumo ule kulikuwa na Mapungufu yapi na kwa nini Usiboreshwe Tukaendelea nao? (Naomba kuelimishwa.)
 
Rais wa tz ni sahihi kuteua marehemu Kwa sababu hiyo nafasi haimfai na hajaipata Kwa kuitafuta yeye binafsi.Alilithishwa urithi.alipata mbeleko ya kurithi na kuanza kutumbua keki ya taifa pasipo utaratibu unaotakiwa.Mtu yeyote anayerithi huwa hana uchungu na kitu alichorithishwa nacho.huwa anakichezea tu hovyo hovyo kama anavyo chezesha huyu mama Yao.
 
Vituko juu ya vituko. Kuna mwingine aliteuliwa nafasi mbili kwa wakati mmoja na cheo ni hicho hicho. Kule znz mgonjwa aliyelazwa icu India huko alipiga kura bungeni la hapo zenj.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…