Kuteua watu kabla ya kuwajulisha: Wapi kwingine duniani wanafanya hivyo?

Hii kauli sikubaliani nayo kabisa. Kwani Katiba ya Nchi Haikuzingatiwa? Hebu tuambie bro, mathalan ingelitokea kuwa umepewa walau nafasi moja tu ya Upendeleo ukatakiwa kupendekeza Nafasi ya Rais wa Tz apewe nani; ungemchagua nani?
 
Kifupi nchi inaongozwa kihuni na wahuni
 
Hii kauli sikubaliani nayo kabisa. Kwani Katiba ya Nchi Haikuzingatiwa? Hebu tuambie bro, mathalan ingelitokea kuwa umepewa walau nafasi moja tu ya Upendeleo ukatakiwa kupendekeza Nafasi ya Rais wa Tz apewe nani; ungemchagua nani?
Katiba ni batili.walioitunga hiyo Sheria ya kurithisha ni wa chama kimoja Cha ccm.katiba inatakiwa iseme endapo kutatokea changamoto kama iliyotupata 2021 makamu arithi miezi sita au ikizidi kabisa iwe mwaka mmoja.baada ya hapo unafanyika uchaguzi.Nchi zote duniani hakuna katiba inayomrithisha makamu zaidi ya mwaka mmoja ispokuwa ni i Tanzania pekee
 
Safi mkuu, ila hukutoa pendekezo. Nadhani imekuwia vigumu kutokana na Ukweli kwamba hakuna asiyekuwa na mapungufu.
Ni kweli kama Katiba inamapungufu hayo, basi Katiba hiyo ibadilishwe na ipatikane Katiba Mpya itakayokidhi mahitaji ya sasa 2024+ na sio hiyo tunayoendelea nayo (iliyopo) iliyokidhi mahitaji ya wakati ule 1977.
 
Viongozi wa Africa wanafikiri kila mtu anasubiri kuteuliwa kwa hamu, kumbe kuna wengine ukiwateua umewaharibia maisha na ustaarabu wao. Ni aibu kwelikweli kuteua marehemu kwenye serikali yako!
 
Viongozi wa Africa wanafikiri kila mtu anasubiri kuteuliwa kwa hamu, kumbe kuna wengine ukiwateua umewaharibia maisha na ustaarabu wao. Ni aibu kwelikweli kuteua marehemu kwenye serikali yako!
Hilo limetokea kwa bahati mbaya au unaona ni kwa makusudi au ni la kiMkakati?
 
Yani hii mpaka aibu tumeona sisi hii ni kali haijawahi kutokea kwa kweli!
Mkuu; Hiyo Imewahi kutokea.
Nanukuu: "........Tamar Aaron Mbogho (11), alipojitokeza na kupokea Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD), akimwakilisha mama yake Swai Sophia Faustin ambaye alifariki dunia miezi sita kabla ya kufika siku ya mahafali......"Gazeti la Habari leo Nov.2016
 
Point zako 1 mpaka 4 zinakubaliana na hoja yangu ya uhamisho wa wafanyakazi. Nakubaliana na wewe.
Kuhusu kutokuwa na malengo endelevu na upimaji wa mafanikio hapo nina mawazo tofauti kama nilivyoeleza mwanzo nilipochangia hoja ya awali.
 
Nanukuu: "Kuhusu kutokuwa na malengo endelevu na upimaji wa mafanikio hapo nina mawazo tofauti kama nilivyoeleza mwanzo nilipochangia hoja ya awali." OK Sawa. Hebu tushirikishane uzoefu:-
Ninao uzoefu (12 yrs +) kwa sehemu nilizo-underline na niseme tu kwamba changamoto kubwa hapo ni Upatikanaji wa Fedha za Utekelezaji ndani ya Time frame iliyowekwa na wakati mwingine malengo hayazingatiwi na yanabaki tu kwenye flipcharts ukutani ndani ya Ofisi ya Kijiji. Mengi yamepitwa na wakati au yamechakachuliwa. Ukiuliza Uongozi wa Kijiji imekuwaje wanakujibu kwa furaha kabisa wanakwambia tulifanya Mradi fulani badala ya hiyo iliyopangwa hapo.
Mabadiliko katika uongozi wa Kijiji hilo nalo ni mojawapo ya changamoto.
Huwezi kupima mafanikio ya utekelezaji wa malengo ambayo hayakupangwa kama hujafanya utekelezaji walau hata kidogo i.e. Kilichopangwa ni Tofauti na kilichotekelezwa.
Pia kuna Hoja ya Haphazard Flexibility. Miradi au Malengo yanabadilishwa, kuhamishwa eneo la utekelezaji kiholela kwa interests binafsi za viongozi. Hapo inaweza pia kuwemo agenda ya kisiasa japo kwa kificho.
Ni kwa kutokana na hoja nilizoainisha Mfuatiliaji yeyote binafsi atasema kama ulivyosema wewe hapo kwenye nukuu.
 
Ni kama vile hiyo taasisi haina hata mtu mmoja mwenye common sense!

Sijawahi kabisa kuielewa hii dhana ya kuteua watu bila hata ya kuwajulisha!
Kwsnza ni ukosefu wa utu na heshima dhidi ya kiongozi mwenzako.
Watu wanakuwa na mipango ktk maeneo yao, pengine ukiwapa nafasi itasaidia kujua maono yake zaidi.

Lakin pia ni kupunguza nafasi za uteuzi ili kuwe na ufanisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…