Kuteua Waziri mwanamke Wizara ya ulinzi ni sawa?

Ubaguzi ni kitu kibaya sana.

yaani leo mtoa mada hamtaki waziri wa ulinzi kwa sababu tu ni mwanamke, kesho atateuliwa waziri mwanaume lakini mzaramo, jamaa atapinga tena kwa sababu wakurya na wasukuma wa jeshini "wanawadharau sana wazaramo".

Yaani jamaa anataka waziri hadi awe mwanaume, ana misuli mikubwa na mingi, mwili jumba, alafu mweusi "tiii", na ikibidi awe na macho mekunduuuu, na aitwe Sarakikya, Waitara, Matiko et al.

Tuna safari ndefu sana kama taifa.
kavulata
 
Tumia simu yako muangalie Mwana Mama Florence Parly,ana cheo gani huko France,kisha njoo uedit thd yako kua haijawahi kutokea Duniani Mwanamke kuongoza wizara ya Ulinzi.
 
Commander in chief ni mwanamke..... halafu unauliza kama Wizara ya Ulinzi ni sawa kuongozwa na mwanamke!
 
Binafsi sihoji uwezo wake wa kitaaluma na uzoefu wake kwenye nyanja mbalimbali. Mimi naongelea taasisi ambayo 98% ya wafanyakazi wake ni WA jinsia moja utapelekaje kiongozi wa jinsia ingine? Yaani shule ya wasichana watupu halafu mkuu wake wa shule ni mwanaume hata kama ni professor ni sawa?
 
Binafsi sihoji uwezo wake wa kitaaluma na uzoefu wake kwenye nyanja mbalimbali. Mimi naongelea taasisi ambayo 98% ya wafanyakazi wake ni WA jinsia moja utapelekaje kiongozi wa jinsia ingine? Yaani shule ya wasichana watupu halafu mkuu wake wa shule ni mwanaume ni sawa?
Kwani tatizo lipo wapi wewe mwenye akili fupi kama ya babu yako wa kisukuma. Acha ushamba, mmesomeshwa hadi darasa la saba na form four lakini akili hazikuwi.
Jibu hoja, shule ya wasichana mwalimu mkuu akiwa mwanaume ni sawa?
 
Nyie mnaoona ubaguzi ni kitu kibaya ndio nyie nyie huwa tunaungana hapa kubagua mashoga,kama mnafikiri ubaguzi ni kitu kibaya kabisa na kila mtu ana haki basi hata mashoga tusingewabagua nao tuwachukulie kama sisi tu.
 
Utakuja mleta hoja una familia
 
Wewe inaonekana umezaliwa kilabuni, tena kwenye pombe za kimpumu kama si wanzuki. Yaani mtu mzima na akili zako unaongea pumba, kweli wewe ni fala kweli.
Hizo ni dalili za mtu mwenye woga na hofu ya alichokifanya.
 
Kwani wanaume walishindwa nini kwenye hiyo Wizara hadi tuwajaribu wanawake? Usawa hauwezi kuletwa na attitude ya aina hii. Kufanya hivi ni kulipiza kisasi na kulipa kikombozi kwa wanawake. Usawa uhimizwe kwenye maisha ya kawaida kama vile kufanyakazi, kuhudumia familia. Yaani 50 kwa 50 jeshini, kuendesha bodaboda, matumizi ya familia, kulipa mahari, kukwea minazi kuangua madafu, nk. Lakini huu usawa wa bungeni, MaDC, RC, Mawaziri ni usawa bandia usiokuwa na uhalisia.
 
Naona watu mnaumauma maneno kwa kifupi tu achilia mbali kuwa na Waziri wa ulinzi mwanamke kitendo tu cha kuwa Rais wa nchi mwanamke kwa Tanzania yetu bado sana.
Hata wanawake wenzake wengi hawakubaliani kabisa na hili.
Ngoja tuone 2025
 
Sio kuwa Malkia wa Uingereza anaweza kuamrisha uvamizi wa vita katika nchi nyingine tu bali ni yeye pekee ndio mwenye mamlaka hayo

Soma historia ya Dunia ni wanawake wangapi walipata hayo majukumu ya kuwa kwenye Ulinzi

Akina Bandaranaike (late) Na Indira Gandhi (late) ni baadhi ya waliwahi kuwa na hiyo title

Waziri wakuu huwa Ulinzi pia
Wala haishangazi kabisa labda kama hupendi kuona wao pia wana haki ya kushika madaraka
 
Kuna kale ka msemo kwamba wanwake nao wanwaweza...
 
Jamii Yao hao Iko hivyo na ilikuwa hivyo kutokana na historia Yao na mazingira Yao. Historia/background yetu ni tofauti sana na Yao. Huwezi kufanya copy and paste eti kwakuwa fursa imetokea na imepatikana basi ni Chuki Chuki Chuki dhidi ya wanaume. Yaani inawezekana Yuko mwanamke aliyetendwa vibaya na mwanaume wake basi wanachukiwa wanaume wote bila sababu
kuwa wanawake Wana nguvu
 
Kwani wanawake wameshindwa nini kwenye hiyo wizara na hata tusiwaamini ?
 

Ila kuna wanawake pia ni wabora kuliko baadhi ya wanaume na wanaweza kufanya kazi kwa ueledi na ufanisi zaidi

Kweli sio kila mmoja au nchi zinakubaliana na hili ndio binadamu tulivyo
Na hata hao wanawake waliofika ngazi za juu walifika kwa bidii zao na Vyama vyao kuwainua na kuwakubali

La kwetu linaweza kuwa ndio mwanzo na mwisho ila limeingia kwenye historia pia
 
Hata mama yangu ni mwanamke hivyo sina Chuki na wanawake hata kidogo, ila wasichaguliwe watu kwakuwa ni wanawake na unataka TU kubadikisha historia TU juu ya kwanini miaka yote wawe ni wanaume TU wizara hii, kwani wanaume wamewafanya nini wanawake walivyokuwa mawaziri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…