Kutoana kafara kwenye familia, na Siri ya wazazi wetu

Muhusika Mama mkwe mchawi
 
Sehemu ya kumi.

Katika harakati zangu za kuzunguka huko na huko nilijikuta nafahamiana na kijana mmoja mrefu,mwenye mwili mkubwa wa mazoezi,Mimi ni mrefu,ila kijana alinizidi.

Kijana huyu anatokea kanda ya ziwa,tulifahamiana tukiwa ndani ya boti ndogo tukielekea ukerewe,ilitokea hitilafu ndogo ya boti i huku kila mtu akisali kivyake,lakini baadaye hali ikawa shwari Moses alinitazama huku akicheka,bila shaka alinicheka.
Kiufupi ndiyo mwanzo wa kufahamiana na Moses.

Sasa endelea....................................

Moses alikula chakula kwa pupa,yaani njaa ya muda mrefu ilimsumbua,yote hayo yalitokana na simu aliyopokea toka kwa mkewe Zawadi.
Simu ilileta tumaini,simu ilimpa faraja Moses kubwa zaidi Kwa namna fulani ilimpa ushindi.

Baada ya kumaliza kula alirudi nyumbani huku akishangaa kukuta ugeni wa watu wasiopungua watatu, ambapo mmoja wao alikuwa dada yake wa Zawadi mke wa Moses.

Hivi wewe Moses unajikuta nani, unajiona ni nani haswa ,Una hati miliki ya mdogo wetu? Kwanini unampiga usiku kucha huku ukikosa huruma,mtu anahesabu siku tu aweze kujifungua lakini wewe hukujali!!

Mama yetu unampa presha huko aliko hawezi hata kuongea ,hali chakula kutwa tunambembeleza ,yote hayo ni kwasababu umempiga mwanaye.hivi unajua anampenda kiasi gani?

Sisi wenyewe tunajua,
Watoto wote tunajua zawadi anapendwa na mama kuliko chochote na furaha ya mama yetu ni zawadi , yaani Zawadi akifurahi,akicheka akiwa na wakati mzuri basi mama naye huwa vizuri.hivyo wewe Moses Kwa kumpiga zawadi,umemkosea Sana Mama,umemkwaza mno!!
aliweka kituo dada yake Zawadi ambaye ni Shemeji wa Moses.

Jamani,karibuni ndani,karibuni sana,Kwanza nashukuru mmekuja,Nina malalamiko na Mimi mke wangu alinifanyia,lakini hata hivyo ningependa kusuluhisha matatizo yetu ili Mimi na mke wangu tuishi kama zamani.siwezi kumpoteza mke wangu, nampenda sana zawadi.(Huku akijaribu kuwashawishi wageni wake waingie ndani)

Haingii mtu ndani ,shetani mkubwa wewe ,eti nampenda mke wangu,nini mke,
Unajua Sisi wenye mdogo wetu tuna uchungu gani?
Unajua mama mzazi ana uchungu gani?
Kwahiyo wewe Moses unaweza kuwa na uchungu na Zawadi kuliko sisi?
Huyu unayemuona ni mume wangu (huku jamaa fulani wa makamo akiguswa ambaye ni mume wa Yule Shemeji wa Moses) tangu anioe tuna miaka zaidi ya kumi na tano lakini hajawahi kunipiga hata kofi tu,Kwanza angeanzaje!! Lakini wewe hata miaka miwili hujafikisha lakini mdogo wangu unamgeuza na kumnyanyasa Kwa vipigo visivyoisha unataka kumpa kilema?

Unatafuta jela weee mtoto,Kwanza ukimuua mdogo wangu na wewe unakufa,yaani uniulie mdogo wangu halafu uende jela ukale huku ndugu yangu ukimnyima haki ya kuishi,wewe nitakubali wapi.alibwata Shemeji wa Moses huku mume wake akiwa hatii wala kuongeza neno,ila akawa anamkonyeza Moses asijibu chochote.

Shemeji wa Moses, mwanamke wa makamo , mwanamke mwenye heshima,mshauri lakini pia alikuwa ni kimbilio la Moses,pindi wakikwazana na mkewe,Yule Shemeji yake ndiye alikuwa mwenye hekima,Busara na maamuzi mazuri kuliko wengine katika familia ya zawadi,lakini siku hiyo Moses alishangaa kuona mtu anayemwamini kageuka mbogo na asiyevumilika.

Waliondoka bila kuaga huku Moses alishangaa,siyo kushangaa kichambo alichopata toka Kwa Shemeji yake,bali ni aina ya maisha yaliyokuja Kwa kipindi kifupi,yaani haheshimiwi,hathaminiwi na hapendwi kama zamani,hasira ziliibuka upya , alijiona mzembe kutukanwa kisha yule Shemeji kuondoka bila ngeu wala kama.

Fu*k yule mjinga katokaje bila ngeu?
Yaani abwate na kujiachia nyumbani kwangu halafu nimwache bure ni ujinga gani nimefanya?

Yule mumewe na Yule mwendesha pikipiki wangenufanya nini?

Kwanza hata kama ningewaumiza si nipo kwangu wangenifanya nini?wangeshitaki wapi?
Si ningewaruka kwakuwa wamenivamia nyumbani kwangu?

Halafuuuuu,,,mbona muda si mrefu mke wangu kipenzi zawadi nimeongea naye kanijibu Kwa upole?
Kama angenichukia kihivyo si angekuwa mkali zaidi ya wengine, kwakuwa yeye ndiye muhusika?

Yule Shemeji m****** (akitoa tusi Moses)
Kwanza Mimi ni handsome, napendwa na wanawake wa rika zote,kila mwanamke hutamani kuwa na Mimi wapo wanaonitamkia wenyewe,wapo ambao nikigusa,wapo kwenye line,aaaaargh Zawadi asinisumbue,ni mjinga mmoja aliyekosa bahati ya kuwa na Mimi.aliwaza kijinga Moses huku usingizi ukimchukua pale kwenye kiti alipokaa.

Alishitushwa na hodi ,ambapo mbishaji alikuwa anapiga kelele baada ya kuona mlango upo wazi lakini mwenyeji haitiki wala kuonesha yupo.

Karibu,ingia tu,alikaribisha Moses.

(Huku akishangaa mume wa Shemeji yake,ambaye ni kama lisaa tu limepita wametoka kumwambia maneno yasiyofaa.

Moses mdogo wangu,usipaniki sijaja na Shemeji yako,hata muda ule nilitamani kuongea na wewe lakini isingewezekana ,sote ni mashahidi namna ambavyo mke wangu alivyokuwa.

Kiufupi Moses umeoa kwenye familia yenye matatizo,wote tuliooa pale ni hivyo tu tunavumilia lakini ndoa zetu si nzuri saaaaana,kama Mimi Yule Shemeji yako,ulivyoshuhudia mdomo wake alivyo ni kwasababu tu,tuna watoto lakini Mimi ningeshaachana naye siku nyingi mno,ila kuhusu wewe Moses,nikupe pole,POLE SANA mdogo wangu,wewe paleeeeee ................(Huku akichukua kitambaa mfukoni na kujifuta jasho) Hivi Moses huwezi kabisa kuachana na Zawadi? aliuliza Yule jamaa aliyeoa Sehemu moja na Moses.

Kaka,kuna nini, niambie.aliuliza Kwa sauti ya upole ila iliyonyooka,huku akiwa active macho na masikio ili asikose hata nukta ya neno.

Lakini badala ya kuongea Yule Jamaa alitikisa kichwa huku akionesha kumuhurumia Moses.

Je ni mambo gani anayotaka kumwambia kijana Moses.
Je Moses atakubali kumwacha Zawadi ikiwa atasikia mabaya kutoka Kwa mkewe?

Next episode ina majibu

Itaendelea....................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…