Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
659
Reaction score
1,101
Niende tu kwenye mada kwani kichwa imevurugika hata sielewi.
Nilifunga ndoa ya kanisani miaka kadhaa nyuma. Baada ya kama miaka mitatu yandoa tukashindwana kila mtu akawa na maisha yake. Mwaka jana nikafunga ndoa ya serikali na mke mwingine bila kuvunja ile ndoa ya kwanza.
Tatizo limekuja baada ya kumkatia huyu mwanamke bima ya NHIF na kuanza kupokea huduma za matibabu.Ugonjwa wake unatumia garama kubwa sana nadhani hilo ndo lilichangia watu wa bima kuniita.
Nimeitwa nikaambiwa wamechunguza nakugundua kuwa nina ndoa ya kanisani ambayo haijavunjwa na ndoa hiyo ni ya mke mmoja hivyo hii ndoa ya pili ni batili na nimefunga kwa malengo ya kunufaika na bima.
Nimejaribu kuwaelewesha kuwa ndoa ya kwanza imebaki tu kwenye cheti ila hawajataka kuelewa hadi niwaoneshe hati ya talaka.
Mwisho wamenambia watanitumia utaratibu wakulipa gharama zote zilizotumiwa na huyu mwanamke ambazo sio chini ya milioni10.Pamoja na hilo wamesema watafungia kadi za wategemezi wangu wote ikiwemo mimi mwenyewe hadi hilo deni ltakapolipwa lote ndo watazifungulia isipokuwa ile ya mke.
Wamesema nikishindwa kulipa shauri hili litaenda kwa mwajiri na hatimaye mahakamani.
Hapa nilipo napata shida kwani pamoja na kulipa hilo deni bado natakiwa kugharamia matibabu ya mke kwa cash kwani bado hajapona.

Wakuu,kama kuna namna naweza kutoka kwenye hili nisaidieni, ila kama haiwezekani napenda kuwashauri kuwa kilichonipata kikawe funzo kwa kila mwenye kesi inayofanana nahii ya kwangu.
 
Mkuu, usitake mambo yawe mengi kuwa mpole, huna cha kujitetea.
1. Serikali ndo inasajili na kutoa vyeti vyote vya ndoa haijalishi ni ndoa ya wapi.
2. Ndoa ya kikristo ni ndoa ya mke mmoja, huwezi kufunga ndoa moja juu ya ndoa nyingine bila kutoa talaka ya ndoa ya kwanza.
3. Kufunga ndoa ya kiserikali ni jaribio la udanganyifu maana unajua kabisa una ndoa nyingine tena unaongeza nyingine.
Wakikupeleka mahakamani hutoboi, malizana nao kabla hujapata hasara zaidi.
 
Bwana mdogo, unateseka sana na utelezi😄😄😄

Anyway inaonekana wewe ni mpole sana alafu hupendi discussion na wandewa.

Rudi tena huko BIMA, omba kuonana na maneja.Mpange mpe kifuta jasho hata M4 akulainishie mambo huduma zako zirudi kama awali.Maisha hayana formula na hayahitaji ucomplicate sana.

Kama wewe ni MZALENDO kalipe 10M kiroho safi.Ila kwa majanga uliyo nayo kaza watakufilisi, msala mdogo huo upo ndani ya uwezo wako ongea lugha ya kimataifa(NUMBERS💰).

#EVERYONE HAS A PRICE,MAKE SURE UNALIKUMBUKA HILI KILA WAKATI!!
 
Back
Top Bottom