Kutojua umuhimu wa talaka kumenigharimu zaidi ya M10

Wewe ndio umechemka, kama ulifunga ndoa na mwanamke wako wa kwanza, ukitakiwa uachane nae kwa taraka. Hapo bado siku ukifa atachukua mgao huo. Na bado anaweza kuomba mgawane hizo mali (kama zipo) hata ukiwa hai. Wewe endelea kuvuna mali, ila fahamu bado yupo kwenye mali hizo sababu hujamtariki, mmetengana kitanda tuu.

Mpe taraka ili mmalizane mbele ya sheria kabla. Huyo kisheria bado yupo "entitled" na wewe kupita hayo makaratasi mliyo sainiana huko kanisani au serikarini.
 
Nimejifunza jipya. Sijui status ya huyo mgonjwa huko NHIF naye amekuwa blacklisted? Kama hajawa blacklisted mfungulie bima yake separate ya hiari wakati mkiwa mnapambania hii ya kwako.
 
Naona leo l hazikai kabisa 😆

Huyu anaonekana anapenda ndoa na hakujua kwamba mifumo sio wino
 
Nimekubali kumalizana nao mkuu. Jamaa walinambia kama nikimalizana nao kesi itakuwa imemalizika kati yangu na wao ila nikishindwa ndo itaenda mbele zaidi
 
Ndio madhara ya kutegemea kila kitu kitaenda sawa bila kufuata matakwa ya kisheria. Na ukiachana na hilo la bima, bado huyo mke wa kwanza anaweza dai mgawanyo wa mali utakazopata baada ya wewe kudai mmeachana.

Serikali haina umbea, haijui kama mmevunja ndoa. Kufunga mmepewa cheti, kuachana unategemea maelezo ya mdomo. Kaa tiyari.
 
Na ikitokea umedondoka sasahivi,huyo mke wako ulofunga nae ndoa ya kiserikali hana haki ya kurithi hata kijiko, mke wako wa kwanza ndo anachukua kila kitu,kuna watu hii imewatokea kimewarambaa.
 
Hata hicho kiasi ni kikubwa, akae na bosi amweleze ukweli wote, atasaidiwa.
 
Huwezi kujua hata hili la Bima mke wa kwanza amemchoma, hakuna mwanamke atakubali kuachwa kienyeji na kumwona mwenzake anakula mema ya nchi
 
Kwahiyo umesubmit vyeti viwili vya ndoa NHIF vya wanawake wawili tofauti si ndio?

Yani ujinga kama huu unamfundisha nani? Huelewi divorce decree ina kazi gani?

Devorce decree ndio ilikuwa unatakiwa usubmit NHIF unarevoke jina mtalaka wako then ndio unafanya endorsement ya mke mpya na cheti kipya cha ndoa.

Halafu utashangaa ukiambiwa huyu naye ana Degree tena labda Masters kabisa.
 
Huwezi kujua hata hili la Bima mke wa kwanza amemchoma, hakuna mwanamke atakubali kuachwa kienyeji na kumwona mwenzake anakula mema ya nchi
Wala hakuna kumchoma, mke wa kwanza ndio anastahili huduma za NHIF, ni mke halali wa ndoa mpaka sasa.

Ndoa inavunjwa Mahakamani peke yake, sielewi shule zetu zinawafundisha nini vijana wa sasa.
 
Mnaingiaga kwemye ndoa mkiwa hamjakomaa akili
 
Hapa ulipigwa mzee.

Inatakiwa kabla ya ndoa, mkapime kila aina ya ugonjwa. Tena urudie hata mara tatu kuhakikisha hakuna magonjwa yaliyo fichwa.

Huyo mwanamke itakuwa alikuwa na gonjwa lake huko, kapiga kimya ili apate boya wa kumhudumia.
Wewe naye umechanganyikiwa ndio maana mimi napendekeza wanandoa kwenye kupima afya zao siyo ukimwi tu, afya ya akili ndio checkup muhimu kuliko vyote, Wabongo wengi akili haziko sawa wake kwa waume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…