Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Una ufinyu wa akili wewe! Mmejaribu kuingiza vikaragosi vyenu mmeshindwa, mkatabiri kifo lakini hakikutokea. Sasa huko kwenu kwenye democracy kwanini hamuwapi form wote wanaotaka kugombea uenyekiti wa chama? Kwanini mnamuhofia Membe?

ANALYSIS: Bashiru, Membe and CCM tradition

Kuna dikteta zaidi ya yule alienyofowa kipengele cha ukomo wa uongozi na akaweka kipya hakuna mwanachama kwenda mahakamani kuhoji ukihoji unafukuzwa chama!
 
Bunge limepitisha sheria ya vyama vya siasa ambapo sasa vyama vya siasa vitapaswa kupeleka mahesabu kwa msajili.
Sasa vyama vya siasa vitatakiwa kutoa taarifa ya fedha wanazopewa na wafadhili.

Vyama haviruhusiwi kuwa na vikundi vya ulinzi

Wanafunzi wa vyuo vikuu hawatakiwi kushiriki siasa wawapo chuoni

Msajili wa vyama vya siasa anaruhusiwa kuingia katika mkutano wa chama chochote cha siasa na anaweza kusimamia uchaguzi wa chama chochote cha siasa.

Source ITV habari!
 
Wakoloni wa kingereza walipitisha sheria za ajabu zimbabwe, kua mkoloni anawwza kuua mtu na asishtakiwe.

Zimbabwe ilipopata uhuru weusi wakawa wanaua wazungu na wakienda mahakamani wanashinda kwa kutumia sheria ile ile ya wakoloni.

Tatizo la viongozi wa Afrika ni kupitisha sheria zinazowalinda wao, wakiamini kua watakua madarakani milele. Wanatunga sheria zjnazowalinda wao, sio zinazolimda nchi, ila wao.

Ubinafsi ndio unaiua Afrika.
 
Sheria hutungwa ili kiwabana wanadamu, hakuna sheria nzuri wala mbaya kwa mwanadamu maana mwanadamu anapenda Uhuru na kujiachia. Hata tukiondoa vipengele vyoote kwenye sheria bado malalamiko yatakuwepo. Muswada utapita na maisha yatasonga
 
Unategemea nini Mkuu kutoka kwenye Bunge UOZO na Bunge DHAIFU ambalo limeweka mbele maslahi ya dikteta na dhalimu kuliko yale ya Watazania milioni 55.

A very sad day in our beloved country.

Yani pamoja na serikali kuchapisha jedwali la mambo yote waliyokubaliana na wanakamati bado Vifungu vyote vimepita kwa ndiyooooo!!
CCM mmetisha, Vizazi vijavyo vitawakumbuka..
 
Nawashukuru wabunge wote kwa kupitisha mswada huu.
Baada ya kusainiwa na rais itakuwa sheria.
 
Nitajie nchi yoyote duniani isiyo na sheria ambayo watu wake wapo Huru wanafanya lolote Walitakalo. Nchi moja tu kaka
Wacha UJUHA wewe! Tulipata Uhuru ili tuwe huru na tuwe na haki kama ambavyo katiba inaruhusu. Huyu dikteta anaipeleka nchi kuwa sawa na iliyokuwa Serikali ya Wabaguzi wa Afrika Kusini. Dhuluma na udhalimu kila kona nchini.
 
Nilijua huyu ni bomu kubwa sana lakini haya ya kuminya uhuru na haki za vyama vya upinzani na Watanzania ikiwemo dhuluma na mauaji sikuliona kabisa.

Kibaya zaidi wastaafu wote wamekaa kimya kabisa wakati huyo muuaji akiendelea kuisambaratisha nchi.

Anafikiri atakuwa kwenye hiyo nafasi milele, anafikiri ataishi milele, anafikiri kinga yake atakapoondoka itakuwa ya milele.

Aendelee tu kujimlika miguuni, badala ya kumlika na sehemu ya mbali. Historia huwa haidanganyi.
 
Sawa kaka, wewe mwelevu, nitajie nchi moja tu duniani ambayo watu wake wapo huru, hakuna sheria za kuwabana. Nchi moja tu
Wacha UJUHA wewe! Tulipata Uhuru ili tuwe huru na tuwe na haki kama ambavyo katiba inaruhusu. Huyu dikteta anaipeleka nchi kuwa sawa na iliyokuwa Serikali ya Wabaguzi wa Afrika Kusini. Dhuluma na udhalimu kila kona nchini.
 
Narudia tena acha UJUHA! Huyaoni maovu mbali mbali nchini wewe? Wizi, ufisadi, mauaji, dhuluma, kutoheshimu katiba, bunge, sheria za nchi na mahakama?

Tia akili kichwani badala ya kuendelea kumuunga mkono huyu dikteta na dhalimu

Nitajie nchi yoyote duniani isiyo na sheria ambayo watu wake wapo Huru wanafanya lolote Walitakalo. Nchi moja tu kaka
 
Back
Top Bottom