Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Siku zote huwa nasema kwamba ajidhaniaye kasimama aangalie asianguke. Wanaodhani sheria hii itawabana wapinzani tu wamekosea sana. Kuna siku itafika wanaofurahia leo watagugumia kwa hasira. Sheria ni msumeno.
 
Duuuh,Mungu mwenye nguvu awalani wote waliopitisha muswada huu,kwan kikokotoo kilikuwaje siwalipitisha halafu wakakipamba kweli kumbe kilikuwa ni kandamizi kwa watumishi.nalaani sana hii
 
Hivi viongozi wa dini waliweza kulisemea hilo swala?
Hata TEC jamani hawakuliona hilo swala?
Na ukute jamaa aliwaita kupima upepo wa hilo mojawapo ,
Sasa kwa kuwa hawakulisema ndo maana sasa hivi ni mwendo wa kufagiliana tu hadi nasikia wengine wanataka kupewa majina ya mitaa !


Sent using Jamii Forums mobile app
 

YAJAYO HAYAKO MBALI, YANAFURAHISHA SANA! ULIPASWA KUFANYIWA MAREKEBISHO NA SIO KUPITISHWA KAMA ULIVYO! TATIZO LETU NI HILI TU KATIKA VYAMA VYETU, UWAJIBIKAJI WETU UMEKUWA DUNI NDANI VYAMA KULIKO NJE YA CHAMA! NDANI YA CHAMA SISI KWA SISI UADUI NDIYO FASHION YA MJINI,
SASA MUSWADA UMEKUJA KUTUKUMBUSHA WAJIBU WETU NDANI YA VYAMA NA SIO NJE.. HATA MAANDIKO MATAKATIFU YALIPATA KUSEMA....................."PINDI PALE MTAKAPO SHINDWA KUJIONGOZA MTALETEWA KIONGOZI MUOVU AMBAYE HATA WAHESHIMU WAKUBWA WENU WALA WA WATOTO WENU!" MUSWADA (KWA SASA SHERIA TAYARI) UTAKUWA KIONGOZI MUOVU KWENYE VYAMA VYETU! MAANA HAUTAMUHESHIMU YEYOTE YULE...TUWEMO KATIKA EPISODE YA PILI INAYOONYESHA WATU KUFUTIWA UWANACHAMA NA VYAMA KUFUTWA......Ila tahadhari tu usije andamana kisa chama chako au mtu anafutwa uwanachama maana utataabishwa sana

Asubuhi njema amani ya bwana iwe nanyi!
 
Duuuh,Mungu mwenye nguvu awalani wote waliopitisha muswada huu,kwan kikokotoo kilikuwaje siwalipitisha halafu wakakipamba kweli kumbe kilikuwa ni kandamizi kwa watumishi.nalaani sana hii

USILAANI ILA NI MATUNDA YA WALE TUNAO WAITA VIONGOZI WETU!
 
muswada huo unalenga pia kuviimarisha zaidi vyama vya siasa...

Sasa upinzani mnacho lalamika ni kitu gani sasa... Kama mswada wenyewe ukipita unaenda kuimarisha vyama vya siasa?


UKIWA NA NYUNDO KILA KITU HUWA KAMA MSUMARI KAKA! TAFAKARI SANA, KINACHOLALAMIKIWA KIPO HAPO HAPO ILA HAYO NI MATUNDA YA MBEGU AMBAZO WALIPANDA KWA MIKONO YAO!
 
Rubbish! Ushahidi mwingine wa Bunge UOZO/DHAIFU udikteta na udhalimu utakithiri nchini chini ya huyu dikteta na dhalimu ambaye ni janga kubwa la Taifa.


NAKUONA NI JASIRI KAMA HERO GBAEK, AU UNA NGUMI NZITO KAMA ZA WANG BAEK SAN MWISHONI ALIUWA KWA NGUMI MOJA TU YA KIJANA MDOGO
 
CCM rudisheni kwanza mali za umma, viwanja, majengo mlojimilikisha baada ya mfumo wa vyama vingi ndo mlete porojo za kuvifanya vyama vingine kujisimamia.
Hivyo unavyosema ni mali ya CCM na vilijengwa na wana CCM, leo ukitoka Chadema huwezi kudai yale magari ya chama kwamba ugawiwe maana najua hakuna kingine mnachomiliki zaidi ya hayo magari tena ya msaada
 
Mambo yanayoendelea nchi hii yanatia kinyaa, hasira mpaka unasikia sukari inapanda
Mshauri mkuu wa mtukufu malaika toka chato ni Naibu Rais ndugu Daud Arbaty Bashite ambaye hana vyeti unategemea nini? Tuendelee kushuhudia vioja zaidi kwanza nasikia wanataka kusajili vyama vingi vya Siasa iwe kama Congo iwe rahisi kuvichonganisha vinanyang’anyana kura huku CCM ikipeta kirahisi, lakini hakuna mabaya yasiyo na mwisho na mwisho wa ubaya ni Aibu
 
Hivyo unavyosema ni mali ya CCM na vilijengwa na wana CCM, leo ukitoka Chadema huwezi kudai yale magari ya chama kwamba ugawiwe maana najua hakuna kingine mnachomiliki zaidi ya hayo magari tena ya msaada

Mfano wa magari hauna uhusiano na jinsi CCM walivyojimilikisha majengo ni vitu viwili tofauti kumbuka CCM ni chama kipenda magumashi
 
Naomba mwenye nakala ya Mswada tajwa afanye kushare tupate kuona ni kipi haswa kiko ndani ya huo muswada.
 
wabunge wa ccm pelekeni muswada ili Magufuli awe rais wa Maisha.
 
Reactions: BAK


MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Mwaka 2018, umesomwa kwa mara ya pili bungeni huku vyama vya siasa vinavyopata ruzuku ya serikali, vikitakiwa kuwa na akaunti maalumu ya benki kwa matumizi ya fedha hizo, ambazo vyama vitakavyoshindwa kuzisimamia vitafutiwa. Aidha, muswada huo ambao uliwasha moto nje ya Bunge, umempa nguvu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu wa mapato na matumizi ya fedha za vyama vya siasa.

Akiwasilisha muswada huo jana bungeni, Waziri wa Nchi, Osi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama alisema lengo la akaunti hiyo maalumu ya ruzuku ni kuhakikisha fedha za ruzuku zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sheria.

“Lengo ni kuhakikisha chama cha siasa kinachopata ruzuku hakichanganyi mapato na matumizi ya fedha za ruzuku na fedha kutoka katika vyanzo vingine,” alisema Jenista. Alisema Kifungu cha 24 cha muswada kinakusudia kurekebisha Kifungu cha 18 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ili kumpa msajili mamlaka ya kusitisha ruzuku kwa chama cha siasa, kinachoshindwa kusimamia matumizi ya fedha hizo, kwa lengo la kulinda fedha za umma zisitumike vibaya. Vile vile, kifungu hicho kinataka kumpa msajili mamlaka ya kumuomba CAG, kufanya ukaguzi maalumu mapato na matumizi ya chama cha siasa, ili kumwezesha msajili kubaini .

upungufu uliopo katika mapato ya matumizi ya chama cha siasa. Alisema Kifungu cha 21 cha muswada huo, kinakusudia kuweka Kifungu kipya cha 12 C cha Sheria ya Vyama vya Siasa ili kuvitaka vyama hivyo kutoa tamko la mapato na matumizi katika chama cha siasa.

Jenista alisema Kifungu cha 22 cha muswada kinakusudia kurekebisha Kifungu cha 13 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ili kujumuisha vyanzo vya mapato vya chama cha siasa ya ndani ya nchi katika vyanzo vya mapato, vinavyopaswa kuwekwa wazi kwa msajili, lengo nikuwezesha msajili kuratibu vyema mapato na matumizi ya vyama vya siasa.

“Lengo pia ni kuvitaka vyama vya siasa kuteua Asa Msuhuli atakayesimamia mali za chama, lengo ni kuwezesha kila chama cha siasa kuwa na mtu anayewajibika katika mapato na matumizi ya chama, ili kudhibiti mfumo wa uwajibikaji katika utunzaji wa mali za taasisi,” alisema.

Alisema Kifungu cha 25 cha muswada kinakusudia kufuta na kuweka kifungu kipya cha 18A cha sheria ili kuweka sharti kwamba mwaka wa fedha wa kila chama, unapaswa kuwa sawa na mwaka wa serikali, kwa kukitaka chama kuwasilisha taarifa za hesabu zake kwa CAG kwa ukaguzi na kutoa taarifa ya hesabu zilizokaguliwa kwa msajili. Alisema Kifungu cha 11 cha muswada kinakusudia kuongeza vifungu vipya 8C, D, na E katika sheria, ambapo Kifungu cha 8E kinaweka katazo kwa chama cha siasa kuanzisha kikundi cha ulinzi na usalama au kuendesha mafunzo ya kutumia nguvu au silaha ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote.

“Kifungu cha 7 cha Muswada kinaongeza sehemu mpya IIA na kifungu 6A, B na C ambapo katika sehemu IIA inahusika na uundwaji wa vyama vya siasa ambapo Kifungu 6B kinaweka sifa za mtu anayeomba kusajili cha awe raia wa Tanzania na kifungu 6C kinataka mwanachama awe raia na kinakataza raia wa nje kushiriki katika kufanya uamuzi ya chama,” alifafanua waziri
 
Sheria hizi kandamizi zitafutwa ikija serikali nyingine isoyo ccm
 
Wabanwe kila kona,hatuwezi kulipa kodi halafu mtu anaenda kutanulia huko kwa mabeberu na selfie juu.
 
Mfano wa magari hauna uhusiano na jinsi CCM walivyojimilikisha majengo ni vitu viwili tofauti kumbuka CCM ni chama kipenda magumashi
Nasemea magari kwa vile Chadema hawana asset yoyote bali wanapiga hela tu. Naomba nikufundishe jambo utanishukuru. Baada ya CCM kuanzishwa mwaka 1977, walianzisha miradi mingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mashule,majengo,viwanja vya michezo nk. Ni jinsi gani miradi hiyo ilifanikiwa,ni kutokana na wanachama wake kujitolea kuijenga na umiliki ulikuwa ni wa CCM na siyo Serikali, Ndo maana nikakupa mfano,leo hii wanachama wa Chadema wakijitolea kujenga ofisi ya Chama kwa usajili halali wa chama basi jengo hilo ni mali ya chama na si mali ya Serikali. Ila ukiona kwamba mali za wananchi zimeporwa na CCM ni vizuri ukaenda Mahakamani ili upate tafsiri nzuri ya umiliki huo ili ujiridhishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…