Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Wenyewe wanadhani wanawakomoa upinzani.
Mungu tupe uhai mrefu ili tuone watu wakijutia maamuzi yao
Shida yao Mbowe ang'ooke....

Zitto ang'ooke...

Lowassa na Sumaye warudi Ccm..

Then we remain eating their filthy stinky politics for years..

Yote haya inabidi yatimie mwaka huu before 2020.
 
Kwa ajili ya yule bundi wa bungeni au?....... Chadema haina ubavu wa kuvuruga amani!
Kumbe unatambua Tanzania ni nchi ya utulivu,tulia hapohapo.Kwa hiyo Mbowe akiondoka "nchi haitatawalika?"

Sent using Jamii Forums mobile app
Sheria zinazopitishwa kwa nia ya kukomoa au ku favour kundi fulani, haziisaidii nchi bali kujifurahisha nafsi.

Siku tutakapoongozwa na hekima tutaisaidia mama Tanganyika. Mengine haya ni usanii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mujibu wa mwakilishi wa TLS aliyehojiwa na ITV amesema sasa vyama vinavyoishi bila kufanya uchaguzi wa viongozi wake na wale viongozi wa maisha siku zao zinahesabika kwani sasa msajili wa vyama vya siasa amepewa rungu na sheria mpya.

My take
Chadema na Mbowe jiandaeni kisaikolojia
Maendeleo hayana vyama!
Chadema hii ife tu. Ni janga la taifa.
Majanga:
1. Ujinga
2. Umasikini
3. Maradhi
4. Chadema.
 
CCM mtaukumbuka huu Mswada wa Vyama vya Siasa!!.
 
Spika Ndugai ameipongeza Serikali kwa kazi nzuri na Muswada umepita kwa kura za Ndiyo

======
BAADHI YA NUKUU (KUTOKA UPINZANI)

Kambi ya rasmi ya upinzani bungeni imekosoa muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa wa mwaka 2018 ikisema ni uonevu mkubwa dhidi ya vyama hivyo.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo bungeni leo, msemaji wa kambi hiyo, Ester Bulaya amesema wabunge wana uwezo mkubwa wa kuzuia uonevu huo ikiwa watapenda kufanya hivyo.

Bulaya ametoa mfano wa vifungu vinavyoonea katika muswada huo kuwa ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama akisema kutapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka ofisi ya msajili.

Kingine amekitaja ni kinachotoa masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia kuwa masharti hayakutilia maanani kuwa vyama vya siasa vina mahusiano ya kiitikadi na vyama rafiki toka nje ya nchi.

“Ni haki yao ya msingi ya kueneza itikadi za vyama vyao bila kujali mipaka ya nchi…huu ni upungufu mkubwa kwani msajili anaweza kukataa tu kutokana na maslahi yake bila kuongozwa na sheria inayopendekezwa,” amesema.

Halima Mdee:

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amesema baadhi ya vipengele vya muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018 vinavunja Katiba.

Akichangia muswada huo bungeni leo, Mdee amesema miongoni mwa kinachovunja Katiba ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama ambacho kitashindwa kuwa na kumbukumbu za wanachama wake.

“Muswada huu unataka vyama vya siasa viweke rejista kila ngazi. Kuna wanachama wanaingia na wanatoka kila siku na kununuliwa kila leo. Sasa chama kitakuwa hakina kazi nyingine zaidi ya kuweka kumbukumbu,” amesema.

Amesema muswada huo unasema kuwa chama kitakachoshindwa kufanya hivyo msajili atakifuta lakini Katiba inasema mazingira ambayo inaweza kukinyima chama usajili ama kukifuta.

Mdee amependekeza kifungu hicho cha 8 (C) kifungu kidogo cha 3 kifutwe kwa kuwa kinakwenda kinyume na Katiba.

Amesema ibara ya 13 ya Katiba inasema ni marufuku kufanya ubaguzi lakini baadhi ya vifungu vya muswada huo vinakwenda kinyume.

“Uvunjwaji wa Katiba si jambo dogo. Tunataka ufanye marekebisho utakapokuja hapa (Waziri katika ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, vijana, kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama)” amesema.

Mdee amesema kifungu kingine wanachokitaka kifutwe ni kinachohusu zuio la vikundi vya ulinzi: “Hakuna asiyefahamu kuwa vikosi vya ulinzi wakati wa uchaguzi vimekuwa vikifanya kazi ya CCM. Polisi wanalinda maboksi ya kura. Kusingekuwa na shida kama majeshi yangesimama katikati.”

Salome Makamba:

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Salome Makamba amesema Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 ukipitishwa kuwa sheria, itawachinja walioitunga.

“Dua la kuku halimpati mwewe. Leo mnaitazama kesi ya CUF mnaitazama Chadema. Sheria itakuja kuwachinja walioitunga kwa kumpa mamlaka makubwa msajili ya kufuta vyama vya siasa,” amesema Salome akibainisha kuwa kazi ya Msajili wa vyama ni ulezi kwa vyama.

=====

NUKUU KUTOKA CCM:

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji amesema Muswada wa Marekebisho ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018, unalenga kuondoa uhuni na kuvifanya vyama vya siasa kufanya kazi kwa ukomavu.

Akichangia muswada huo bungeni leo Januari 29, 2019 Lusinde amesema muswada huo unalenga pia kuviimarisha zaidi vyama vya siasa.

“Tukomae tufanye kazi za ukomavu, siyo kuzunguka kwenye corridor (viambaza) za mabalozi. Sheria zinatungwa ndani ya Bunge, viatu vinaisha soli,” amesema.

Amesema muswada huo unakwenda kuvitaka vyama vya siasa kutambua tunu za Taifa ikiwamo Mwenge na Mapinduzi ya Zanzibar.

“Msajili alikuwa akihudhuria kama mualikwa sasa anasimamia na kuangalia demokrasia kama inatekelezwa ndani ya chama,”amesema.

Amesema muswada haukatazwi kulindwa kwa chama chochote cha siasa na hakuna chama ambacho kimekatazwa kuwa na mlinzi wa kukilinda.

UPDATES

"Bunge limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa utakaoongeza uwajibikaji miongoni mwa vyama vya siasa na kukuza demokrasia nchini" Dkt Hassan Abbasi, MsemajiMkuu wa Serikali

Hapa ndo inabidi Zitto & Company aende mahakamani kupinga vifungu ambavyo vinapingana na katika.
 
Na, Mwl, Osunga Pasaka Jr.
ZITTO KABWE ULITAKA HITLER AFANYEJE??
Nimepitia mitandao ya kijamii nikaona tweet ya huyu kijana akidai haya yalifanywa na Hitler?

Hivi kweli unamjua Hitler?

Mara baada ya vita vya kwanza vya dunia 1914-1918, Hitler pamoja na rafiki yake Austria walishindwa vibaya, hali iliyosababishwa na usaliti wa rafiki yao wa karibu Italy aliyeamua kuondoka kwenye vita kwa zawadi nono aliyoahidiwa.
Baada ya vita hivyo kilifuatia kikao cha amani pale Versaille, mji uliojirani na Paris Ufaransa.
Katika kikao hicho kilichokuwa cha upande mmoja (Tripple entete) kilichoshutumu ujeruman kama waanzilishi wa vita kiliweza kuja na maazimio yafuatayo:

a) Ujerumani kulipa uharibifu uliojitokeza zaidi ya dollar milioni 6.5
b) kurejesha Alsace na Lorraine kwa Ufaransa( kumbuka wakati wa Franco Prussian war)
c) Kutojihusisha na utengenezaji wa silaha za aina yoyote.
d) Kutokuwa mwanachama wa league of national (Ingawa alikubaliwa baadae).
Nk.

Baada ya vita hivyo Ujerumani ilikuwa chini ya Kaizer ambaye aliisababisha kuingia tena kwenye mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 1929-1933.
Hali hii ikasababisha mwanaume Hitler kuibuka na kusema Ujerumani imeshindwa vita vya dunia kwa sababu ya unafiki wa Wayahudi( kumbuka Wewe Zitto Ujeruman ndo nchi iliyokuwa ikitumia he badala ya she kama nyingine za dunia)
Aliibuka kuitangazia dunia kuwa Ujerumani bado ni strong state ( sense of nationalism) na kwa kuwa kulikuwa na vibaraka wa kiingereza na mataifa mengine ya mlengo wa kibepari aliamua kupitisha sheria hiyo kwa maslahi mapana ya nchi?

Nakuuliza ingekuwa Wewe ungeendelea kuwaacha akina Kaizer waharibu nchi?

Kipindi watu wako bungeni mnatembea Ulaya kuhubiri ushoga, na kulitukana taifa, Ingekuwa Hitler angewaacha????
Acha kusahau mapema Hitler unayemzungumzia ameipata Ujerumani iliyo imara baada ya kutengenezwa na mtu aliyeitwa Chancellor Ottoman Bismarck, ambaye aliamua kufuta kabisa bunge kwa sababu walikuwepo akina Zitto waliopinga Muungano wa Ujerumani nae alisema
"The great question of the day cannot reached by majority resolution but by blood and iron" akalifuta bunge na akafanikiwa 1870's kutengeneza Ujerumani ya Leo.

Zitto tafadhali brother usipende kutumia mifano ya nje ukifikiri Watanzania wrote hatusomi,
Nenda kajipange Upya, Spika ndugai leteni sheria ya kufuta wazururaji walioko huko ulaya muwafute kabisa........
Tunataka maendeleo siyo uzindaki.
Mwl.Osunga Jr.
0756231744
 
Kwa mujibu wa mwakilishi wa TLS wakili msomi Jebra Kambole aliyehojiwa na ITV amesema sasa vyama vinavyoishi bila kufanya uchaguzi wa viongozi wake na wale viongozi wa maisha siku zao zinahesabika kwani sasa msajili wa vyama vya siasa amepewa rungu na sheria mpya.

My take
Chadema na Mbowe jiandaeni kisaikolojia
Maendeleo hayana vyama!
Kweli wahenga walinena, mfadhili Punda Binadamu hana shukrani; yaani leo hii Lipumba anaandikwa hivi kwa kazi yote hiyo...
 
Kwa mujibu wa mwakilishi wa TLS wakili msomi Jebra Kambole aliyehojiwa na ITV amesema sasa vyama vinavyoishi bila kufanya uchaguzi wa viongozi wake na wale viongozi wa maisha siku zao zinahesabika kwani sasa msajili wa vyama vya siasa amepewa rungu na sheria mpya.

My take
Chadema na Mbowe jiandaeni kisaikolojia
Maendeleo hayana vyama!
Mbona humtaji Cheyo "aliyejimilikisha" UDP yake??

Wala humtaji Mrema anayeiendesha TLP kama Chama chake binafsi??

Wewe kada wa Lumumba umemuona Mbowe tuu??
 
Lusinde na Msukuma ni kati ya wanafunzi waliokuwa wanapenda vipibdi vya michezo, kutumwana walimu kwenda kusaga mahindiashineni, kwenda kujenga vyoo vya walimu na ndiyo image ya wabunge wa CCM! Wote wawili they feel inferior kuishia standard 7, sio standard 7 tu ni standard 7 wasiojitambua.
 
Mswaada wa kuuwa upinzani nao utafail tu sawa na mengine mfano manunuzi ya Malaya wa kisiasa, kuzuia bunge live,kuzuia local channel, kuwatumia wajasiliadini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika Ndugai ameipongeza Serikali kwa kazi nzuri na Muswada umepita kwa kura za Ndiyo

======
BAADHI YA NUKUU (KUTOKA UPINZANI)

Kambi ya rasmi ya upinzani bungeni imekosoa muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa wa mwaka 2018 ikisema ni uonevu mkubwa dhidi ya vyama hivyo.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo bungeni leo, msemaji wa kambi hiyo, Ester Bulaya amesema wabunge wana uwezo mkubwa wa kuzuia uonevu huo ikiwa watapenda kufanya hivyo.

Bulaya ametoa mfano wa vifungu vinavyoonea katika muswada huo kuwa ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama akisema kutapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka ofisi ya msajili.

Kingine amekitaja ni kinachotoa masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia kuwa masharti hayakutilia maanani kuwa vyama vya siasa vina mahusiano ya kiitikadi na vyama rafiki toka nje ya nchi.

“Ni haki yao ya msingi ya kueneza itikadi za vyama vyao bila kujali mipaka ya nchi…huu ni upungufu mkubwa kwani msajili anaweza kukataa tu kutokana na maslahi yake bila kuongozwa na sheria inayopendekezwa,” amesema.

Halima Mdee:

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amesema baadhi ya vipengele vya muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018 vinavunja Katiba.

Akichangia muswada huo bungeni leo, Mdee amesema miongoni mwa kinachovunja Katiba ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama ambacho kitashindwa kuwa na kumbukumbu za wanachama wake.

“Muswada huu unataka vyama vya siasa viweke rejista kila ngazi. Kuna wanachama wanaingia na wanatoka kila siku na kununuliwa kila leo. Sasa chama kitakuwa hakina kazi nyingine zaidi ya kuweka kumbukumbu,” amesema.

Amesema muswada huo unasema kuwa chama kitakachoshindwa kufanya hivyo msajili atakifuta lakini Katiba inasema mazingira ambayo inaweza kukinyima chama usajili ama kukifuta.

Mdee amependekeza kifungu hicho cha 8 (C) kifungu kidogo cha 3 kifutwe kwa kuwa kinakwenda kinyume na Katiba.

Amesema ibara ya 13 ya Katiba inasema ni marufuku kufanya ubaguzi lakini baadhi ya vifungu vya muswada huo vinakwenda kinyume.

“Uvunjwaji wa Katiba si jambo dogo. Tunataka ufanye marekebisho utakapokuja hapa (Waziri katika ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, vijana, kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama)” amesema.

Mdee amesema kifungu kingine wanachokitaka kifutwe ni kinachohusu zuio la vikundi vya ulinzi: “Hakuna asiyefahamu kuwa vikosi vya ulinzi wakati wa uchaguzi vimekuwa vikifanya kazi ya CCM. Polisi wanalinda maboksi ya kura. Kusingekuwa na shida kama majeshi yangesimama katikati.”

Salome Makamba:

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Salome Makamba amesema Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 ukipitishwa kuwa sheria, itawachinja walioitunga.

“Dua la kuku halimpati mwewe. Leo mnaitazama kesi ya CUF mnaitazama Chadema. Sheria itakuja kuwachinja walioitunga kwa kumpa mamlaka makubwa msajili ya kufuta vyama vya siasa,” amesema Salome akibainisha kuwa kazi ya Msajili wa vyama ni ulezi kwa vyama.

Zitto Kabwe:

Mwaka 1933, Adolf Hitler alipeleka Muswada wa Sheria Bungeni (enabling act), wabunge wa chama chake wakaupitisha kwa mbwembwe. Miezi 6 baada ya kuanza kutumika Ujerumani haikuwa na chama cha siasa. Hitler aliitumia sheria ileile ilopitishwa na Bunge kuhakikisha vyama vinafutwa na hata wanasiasa wanaikimbia nchi

Madhara ya Muswada huu yanakwenda zaidi ya Ushindani wa chama tawala, CCM dhidi ya Upinzani. Msajili anapewa mamlaka makubwa na muswada huu yatakayoleta hali ngumu huko mbeleni. Mwalimu Nyerere alijaribiwa kupinduliwa takribani mara 8 sababu ya kudhibiti uhuru wa wananchi na uhuru wa kufanya siasa lakini tangu tumekuwa na vyama vingi hakuna jaribio lolote la wananchi kuipindua serikali.

Katiba ya Tanzania ya sasa inaruhusu Uhuru wa Kukutana lakini Sheria hii inaenda kuua Uhuru huo. Msajili alitakiwa anapoona chama kinafanya makosa basi watu wangepelekwa kwenye jopo (Tribunal) ili watu wahukumiwe kwa haki.

Demokrasia si uadui!

Kati ya 2007 - 2012, data zinaonyesha kuwa watanzania takribani 1,000,000 waliondolewa ktk umasikini na ndo wakati demokrasia ilishamiri nchini. Kwa takwimu za karibuni za Benki ya Dunia, tangu Magufuli aingie madarakani 2015, watanzania takribani 2,000,000 wamekuwa masikini

=====

NUKUU KUTOKA CCM:

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji amesema Muswada wa Marekebisho ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018, unalenga kuondoa uhuni na kuvifanya vyama vya siasa kufanya kazi kwa ukomavu.

Akichangia muswada huo bungeni leo Januari 29, 2019 Lusinde amesema muswada huo unalenga pia kuviimarisha zaidi vyama vya siasa.

“Tukomae tufanye kazi za ukomavu, siyo kuzunguka kwenye corridor (viambaza) za mabalozi. Sheria zinatungwa ndani ya Bunge, viatu vinaisha soli,” amesema.

Amesema muswada huo unakwenda kuvitaka vyama vya siasa kutambua tunu za Taifa ikiwamo Mwenge na Mapinduzi ya Zanzibar.

“Msajili alikuwa akihudhuria kama mualikwa sasa anasimamia na kuangalia demokrasia kama inatekelezwa ndani ya chama,”amesema.

Amesema muswada haukatazwi kulindwa kwa chama chochote cha siasa na hakuna chama ambacho kimekatazwa kuwa na mlinzi wa kukilinda.

UPDATES:

"Bunge limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa utakaoongeza uwajibikaji miongoni mwa vyama vya siasa na kukuza demokrasia nchini" Dkt Hassan Abbasi, MsemajiMkuu wa Serikali

Nikiwa mwana CCM kwa muswada huu kwa mara ya kwanza sitakipigia chama changu kura kwa uchaguzi wowote. Hata liwekwe jiwe na mwana CCM nitalipigia jiwe. Nakipenda chama changu ila sipendi kwa yanayoendelea
 
Back
Top Bottom