Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Mbona humtaji Cheyo "aliyejimilikisha" UDP yake??

Wala humtaji Mrema anayeiendesha TLP kama Chama chake binafsi??

Wewe kada wa Lumumba umemuona Mbowe tuu??
Usimsahau Lipumba ambaye alisaidiwa kabisa kutwaa uongozi tena kinyume cha taratibu za chaa chake.
 
Kwa mujibu wa mwakilishi wa TLS wakili msomi Jebra Kambole aliyehojiwa na ITV amesema sasa vyama vinavyoishi bila kufanya uchaguzi wa viongozi wake na wale viongozi wa maisha siku zao zinahesabika kwani sasa msajili wa vyama vya siasa amepewa rungu na sheria mpya.

My take
Chadema na Mbowe jiandaeni kisaikolojia
Maendeleo hayana vyama!
Yaani Tanzania tumekuwa watu wa ajabu sana!!. Tunashangilia kuchukuliwa madaraka kutoka kwa wananchi walioamua kuanzisha chama chao kisheria na kupelekwa kwa mtu ambaye kachaguliwa na wanasiasa ambao sio wanachama. Halafu watu haohao wanakuja kujiuliza baadae kwanini upinzani hauna nguvu au kwanini hatuna mawazo mapya ya maendeleo? ukiangalia vizuri adui wa maendeleo yetu kwa asilimia kubwa ni sisi wenyewe.
 
Spika Ndugai ameipongeza Serikali kwa kazi nzuri na Muswada umepita kwa kura za Ndiyo



======
BAADHI YA NUKUU (KUTOKA UPINZANI)

Kambi ya rasmi ya upinzani bungeni imekosoa muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa wa mwaka 2018 ikisema ni uonevu mkubwa dhidi ya vyama hivyo.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo bungeni leo, msemaji wa kambi hiyo, Ester Bulaya amesema wabunge wana uwezo mkubwa wa kuzuia uonevu huo ikiwa watapenda kufanya hivyo.

Bulaya ametoa mfano wa vifungu vinavyoonea katika muswada huo kuwa ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama akisema kutapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka ofisi ya msajili.

Kingine amekitaja ni kinachotoa masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia kuwa masharti hayakutilia maanani kuwa vyama vya siasa vina mahusiano ya kiitikadi na vyama rafiki toka nje ya nchi.

“Ni haki yao ya msingi ya kueneza itikadi za vyama vyao bila kujali mipaka ya nchi…huu ni upungufu mkubwa kwani msajili anaweza kukataa tu kutokana na maslahi yake bila kuongozwa na sheria inayopendekezwa,” amesema.

Halima Mdee:

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amesema baadhi ya vipengele vya muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018 vinavunja Katiba.

Akichangia muswada huo bungeni leo, Mdee amesema miongoni mwa kinachovunja Katiba ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama ambacho kitashindwa kuwa na kumbukumbu za wanachama wake.

“Muswada huu unataka vyama vya siasa viweke rejista kila ngazi. Kuna wanachama wanaingia na wanatoka kila siku na kununuliwa kila leo. Sasa chama kitakuwa hakina kazi nyingine zaidi ya kuweka kumbukumbu,” amesema.

Amesema muswada huo unasema kuwa chama kitakachoshindwa kufanya hivyo msajili atakifuta lakini Katiba inasema mazingira ambayo inaweza kukinyima chama usajili ama kukifuta.

Mdee amependekeza kifungu hicho cha 8 (C) kifungu kidogo cha 3 kifutwe kwa kuwa kinakwenda kinyume na Katiba.

Amesema ibara ya 13 ya Katiba inasema ni marufuku kufanya ubaguzi lakini baadhi ya vifungu vya muswada huo vinakwenda kinyume.

“Uvunjwaji wa Katiba si jambo dogo. Tunataka ufanye marekebisho utakapokuja hapa (Waziri katika ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, vijana, kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama)” amesema.

Mdee amesema kifungu kingine wanachokitaka kifutwe ni kinachohusu zuio la vikundi vya ulinzi: “Hakuna asiyefahamu kuwa vikosi vya ulinzi wakati wa uchaguzi vimekuwa vikifanya kazi ya CCM. Polisi wanalinda maboksi ya kura. Kusingekuwa na shida kama majeshi yangesimama katikati.”

Salome Makamba:

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Salome Makamba amesema Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 ukipitishwa kuwa sheria, itawachinja walioitunga.

“Dua la kuku halimpati mwewe. Leo mnaitazama kesi ya CUF mnaitazama Chadema. Sheria itakuja kuwachinja walioitunga kwa kumpa mamlaka makubwa msajili ya kufuta vyama vya siasa,” amesema Salome akibainisha kuwa kazi ya Msajili wa vyama ni ulezi kwa vyama.

Zitto Kabwe:

Mwaka 1933, Adolf Hitler alipeleka Muswada wa Sheria Bungeni (enabling act), wabunge wa chama chake wakaupitisha kwa mbwembwe. Miezi 6 baada ya kuanza kutumika Ujerumani haikuwa na chama cha siasa. Hitler aliitumia sheria ileile ilopitishwa na Bunge kuhakikisha vyama vinafutwa na hata wanasiasa wanaikimbia nchi

Madhara ya Muswada huu yanakwenda zaidi ya Ushindani wa chama tawala, CCM dhidi ya Upinzani. Msajili anapewa mamlaka makubwa na muswada huu yatakayoleta hali ngumu huko mbeleni. Mwalimu Nyerere alijaribiwa kupinduliwa takribani mara 8 sababu ya kudhibiti uhuru wa wananchi na uhuru wa kufanya siasa lakini tangu tumekuwa na vyama vingi hakuna jaribio lolote la wananchi kuipindua serikali.

Katiba ya Tanzania ya sasa inaruhusu Uhuru wa Kukutana lakini Sheria hii inaenda kuua Uhuru huo. Msajili alitakiwa anapoona chama kinafanya makosa basi watu wangepelekwa kwenye jopo (Tribunal) ili watu wahukumiwe kwa haki.

Demokrasia si uadui!

Kati ya 2007 - 2012, data zinaonyesha kuwa watanzania takribani 1,000,000 waliondolewa ktk umasikini na ndo wakati demokrasia ilishamiri nchini. Kwa takwimu za karibuni za Benki ya Dunia, tangu Magufuli aingie madarakani 2015, watanzania takribani 2,000,000 wamekuwa masikini

=====

NUKUU KUTOKA CCM:

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji amesema Muswada wa Marekebisho ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018, unalenga kuondoa uhuni na kuvifanya vyama vya siasa kufanya kazi kwa ukomavu.

Akichangia muswada huo bungeni leo Januari 29, 2019 Lusinde amesema muswada huo unalenga pia kuviimarisha zaidi vyama vya siasa.

“Tukomae tufanye kazi za ukomavu, siyo kuzunguka kwenye corridor (viambaza) za mabalozi. Sheria zinatungwa ndani ya Bunge, viatu vinaisha soli,” amesema.

Amesema muswada huo unakwenda kuvitaka vyama vya siasa kutambua tunu za Taifa ikiwamo Mwenge na Mapinduzi ya Zanzibar.

“Msajili alikuwa akihudhuria kama mualikwa sasa anasimamia na kuangalia demokrasia kama inatekelezwa ndani ya chama,”amesema.

Amesema muswada haukatazwi kulindwa kwa chama chochote cha siasa na hakuna chama ambacho kimekatazwa kuwa na mlinzi wa kukilinda.

UPDATES:

"Bunge limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa utakaoongeza uwajibikaji miongoni mwa vyama vya siasa na kukuza demokrasia nchini" Dkt Hassan Abbasi, MsemajiMkuu wa Serikali

Mungu sasa muda umefika umuondoe jiwe toka madarakani
 
Kwa hiyo kwa kiherehere chako umeona chadema tuu..
Hakuna vyama vingine?
Kwa mujibu wa mwakilishi wa TLS wakili msomi Jebra Kambole aliyehojiwa na ITV amesema sasa vyama vinavyoishi bila kufanya uchaguzi wa viongozi wake na wale viongozi wa maisha siku zao zinahesabika kwani sasa msajili wa vyama vya siasa amepewa rungu na sheria mpya.

My take
Chadema na Mbowe jiandaeni kisaikolojia
Maendeleo hayana vyama!
 
Unaua vyama vya siasa. Dikteta aimarishe vyama asivyotaka vifanye kazi zao hadi 2020?



muswada huo unalenga pia kuviimarisha zaidi vyama vya siasa...

Sasa upinzani mnacho lalamika ni kitu gani sasa... Kama mswada wenyewe ukipita unaenda kuimarisha vyama vya siasa?
 
Mswaada wa hovyo kabisa kuwahi kutokea katika nchi hii, yaani hata ule wa kutoa takrima ni nafuu
unajuwa hawa ccm hawana watu makini kabisa walio baki ccm ni wachumia tumbo tu. ndio maana wanatunga sheria za kugandamiza wananchi huku wakisahau kuwa wananchi hao hao ndio wanalipa kodi zinazo wapa kiburi. sasa ni wakati wa wananchi kuugana na kuwakataa hawa wezi na mafisadi waisio kuwa na haya wanao jiita ccm.
 
Ccm ina nafasi ya kutawala mda mrefu sana. Itatawala mda mrefu zaidi endapo hakutaibuka upinzani wa ndani usiodhibitika.
 
CCM lini Mlichagua Mwenyekiti?
Kama ni chaguzi Sasa hata CCM mtauona Moto wake Kina Salim mliwaita si Raia,
Amani na Bilal Chiligati akaokoa Jahazi Dodoma.. 😂
Hawajawai chagua lakini bora yao hazidi miaka 10 ndugu
 
Dah! Hii nchi! Sijui nini kinachoenda kutokea baada ya hili.
 
Mkifanikiwa kuua upinzani wa nje, itakuwa ndio mwanzo wa kuwa na upinzani wa ndani ambao ni mbaya zaidi kuliko wa nje. Kumbukeni, you are united now because you have common enemies out there.

Hawalijuwi hilo kuwa baada ya hapo wataanza kupinduana wenyewe kwa wenyewe, wakati utasema tusubiri
 
Back
Top Bottom