Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Kama kiongozi ni mshirikina, na anaamini asingeupata uongozi alionao bila msaada wa mganga, basi maisha yake yote atawashukuru waganga, sababu siku zote ataamini kwamba, hata wapiga kura wasingempigia bila msaada wa mganga.
 
Ishakuwa hivyo. Mpumbavu ashakuwa.

Mshauri mkuu wa mtukufu malaika toka chato ni Naibu Rais ndugu Daud Arbaty Bashite hana vyeti na mtukufu mwenyewe ile PhD yake ilichambuliwa na Ben Sanane akapotezwa na Bashite na kikundi chake, jiulize sasa mshauri wake mkuu hana vyeti na yy mwenyewe PhD yake full utata unategemea nini hapo?
 
Huyu chawene ni bure kabisa. Ina maana hajui maisha yalikuwaje kabla 1992. Ngoja ni mdokezee kama alikuwa bado mtoto. Kabla 1992 kulikuwa na hamisha hamisha ya watu toka vijiji vya asili na kupelekwa uhamishoni vijiji vya ujamaa. Watu wengi walipata njaa na wengine kuliwa na wanyama kama simba.
Miaka ile ya mwanzoni mwa 1980 na kuendelea kulikuwa na shida kubwa ya mahitaji muhimu watu walikuwa wana amka alfajiri saa kumi kuwahi foleni ya bidhaa muhimu madukani na kuishia patupu kwa bidhaa hizo kuto pelekwa kama ilivyo tarajiwa.
Moja ya sababu ya kuanzisha vyama vingi ni kukubali mabadiliko baada ya kuona chama kimoja sera zake ni pofu na zinakosa chama cha kukikosoa. Chawema ulikuwa unavalishwa napi wakati huo kwani unakoelekea ni kutafuta huruma ya mkuu akurudishe kwenye neema.
Tulikuwa tunavaa suruali vitambaa vya mpira toka Msumbiiji no choice na mashati juliana toka Burundi. Yote haya yalitokea kabla ya vyama vingi na sijui kama unaelewa kwani tuliweza kuwa na mzee ruksa. Hii ilitokana na shida na umasikini kukithiri kwa sababu ya ukiritimba wa chama kimoja hadi pale huyu babu aliposema kama mbwai naiwe mbwai na kutoa ruksa ya kuagizia na kufanya biashara kwa mapana. Nakujuza haya uwache kupotosha watu kuwa vyama vingi vimeleta shida. Hivi ubinafsishaji wa viwanda na kugawana nyumba za serikali ulifanywa na vyama vingi au serikali iliyoko madarakani toka uhuru. Acha uwongo ndio maana mkuu anachukua madokta na maprofesa ninyi wengine ni bure mlichangia kumrubuni mzee wa Msoga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*Kutoka katika chanzo changu cha kuaminika (Kimada wangu anayefanya moja ya kazi ndani ya Mjengo)

Taarifa ni kuwa kuna Onyo lilitolewa na mmoja wa Maafisa wakubwa wa Chama (Jina Ninalihifadhi) kwenye kikao cha siri cha dakika 15-20 na baadhi ya Wabunge kama 17 wa Chama Tawala ambao pia kwa namna moja ama nyingine hawakuwa wakikubaliana na baadhi ya Vipengele vya Muswada ule uliopitishwa.

"Nimeambiwa niwaite niwape ujumbe, Yule atakayesaliti na kukiuka makubaliano yetu ya kupitisha Muswada huu, atashughulikiwa, siku zake pamoja nasi zitahesabika na Tusilaumiane kitakachomkuta"

ilikuwa ni moja ya kauli ya Afisa huyo kwenye kikao hicho kilichofanyika ndani ya moja ya vyumba vya mkutano bungeni Mapema Asubuhi siku ya Jumatatu.

Chanzo changu kinaendelea kusema kuwa Suala la Bundi kuonekana ndani ya Ukumbi wa Bunge lilipotokea lilizidi kuwatia Hofu na kuhusishwa na masuala ya Kishirikina hivyo kila mmoja wao kutepeta na kuunga mkono kukubaliana na kilichokuwepo ili tu kunusuru Maisha yao kwa kuogopa kurogwa na kutolewa Kafara kwa kuzingatia Ujumbe waliopewa na kuoanisha maana tuliyozoea ya Bundi kuonekana kuhusishwa na Bahati mbaya, Ugonjwa, au Kifo.

Ila hili la Bundi Pengine pia inaweza kuwa ni janja tu ya kuchezeana akili kwa kumkamata ndege huyu na kumtupia ndani ya Bunge ili kuwaogofya wahusika na kuwaaminisha juu ya ujumbe waliopewa.

Vinara wa Tunguli na Ulozi Bungeni hakyanani tena Hamuendi Mbinguni!


Bunge la Walozi, Vigagula na Misukule ya Magufuli....!!
Nchi iko kwente Ze Laiti tlaki.....!!Tunajenga Flaiova, EsjiR,Stigla Joji na Mabalabala ya kiuongo cha Lami.
Msema kweli ni mpanzi wa mungu...!!
 
Ila we jamaa kuna wakati ata kidogo ujaribu kuwaza future ya nchi na kizazi chako kijacho. Usiwe ni mtu wa kutukuza tu kisa unalipwa buku 7.

Siku wajukuu zako wakifahamu wewe ni mmoja ya waliolipeleka hili taifa shimoni unadhani watajisikiaje.

Sent from my Hisense F31 using JamiiForums mobile app
Nchi inaelekea kuzuri sema akili zenu ndo zinaenda shimoni.
Siku nyingine tumia akili mimi silipwi hiyo buku 7 na hauwezi kuthibitisha kazi kuropoka tu.
 
Ila we jamaa kuna wakati ata kidogo ujaribu kuwaza future ya nchi na kizazi chako kijacho. Usiwe ni mtu wa kutukuza tu kisa unalipwa buku 7.

Siku wajukuu zako wakifahamu wewe ni mmoja ya waliolipeleka hili taifa shimoni unadhani watajisikiaje.

Sent from my Hisense F31 using JamiiForums mobile app
Nchi inaelekea kuzuri sema akili zenu ndo zinaenda shimoni.
Siku nyingine tumia akili mimi silipwi hiyo buku 7 na hauwezi kuthibitisha kazi kuropoka tu.
 
Tanzania imekuwa nchi ya chama kimoja, now and then ........ asilete sababu za kushindwa!!

Rais kishatuahidi kuwa ataifanya Tanzania kuwa kama Ulaya ............!!
 
Nimesikiliza angalau kipande cha mchango wa Ndugu George Simbachawene kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa,nilichokigundua sasa ipo hoja inapazwa kwa kasi kuwa.....

1.Kufa kwa viwanda nchini Tanzania ni sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama vingi nchini.

2.Kufa kwa Mashamba makubwa yaliyotoa ajora za kutosha ni kwa sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama Vingi nchini.

3.Uwekezaji ambao haukuwa na tija kwa taifa letu kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu Vyama vingi.

4.Tatizo la ajira nchini ambalo linakuwa siku baada ya siku limesababishwa na mfumo wa Vyama vingi nchini.

5.Kashfa kubwa za Rushwa kama EPA,Escrow,Richmond,Meremeta,Dowans n.k zilisababishwa na nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

6.Kufa kwa Shirika la Reli,Shirika la Ndege/Anga kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuanzisha mfumo wa Vyama vingi.

Ndiyo maana George Simbachawene anasema nchi kama China ina chama kimoja tu na uchumi wake sasa ni imara.

Simbachawene anatamani Tanzania tubaki na chama kimoja ili tujenge taifa lenye nguvu duniani.Sijui kwa nini George hajatumia mifano ya mataifa ambayo yameendelea na yana mfumo wa vyama Vingi?

George Simbachawene ambaye kama sikosei aliondoshwa kwenye Wizara ya Madini na Mh Rais kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Mh Rais ile ya Makanikia,anasema huko nyuma nchi ilikuwa kwenye presha muda wote na akataja harakati kama..

1.Movement for Change
2.Oparesheni Sangara n.k

Kwa mtazamo wa Ndugu Simbachawene,harakati hizi zilichangia kuchelewesha maendeleo nchini.

Nakumbuka harakati hizi zlikuwa zinapiga kelele dhidi ya hiki anacholia nacho Mh Rais Magufuli kila kukicha,wizi,Rushwa,kujilimbikizia mali,Uwekezaji wa hasara.

Je Simbachawene anataka kusema Vyama vya upinzani vingekaa kimya wakati Buzwagi wanawasainisha mawaziri wetu mikataba mibovu hotelini?

Je Simbachawene anasema Vyama vya Upinzani vingekaa kimya wakati baadhi ya Mawaziri,wafanyabiasha na watumishi wa Umma wanagawana pesa za Escrow kwenye sandarusi?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya Siasa vikae kimya wakati wakazinwa Nyamongo wanateseka na maji yenye sumu kutoka mgodi wa North Mara,wanapigwa Risasi na wawekezaji?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji kwenye migodi walipojigeuza miungu watu(wasiguswe),walipokuwa wanawahakisha wenyeji kinyama tena usiku wa manane bila fidia?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji hawa walipokuwa wanachimba madini bila kulipa kodi?huku suala la mapato wakilifanya kuwa ni Siri kati yao na Serikali

Je Simbachawene alitaka vyama ya upinzani vikae kimya wakati Twiga wanahamishwa kwenda nje kwa ndege?wanyama wanauwa na wawindaji haramu?

Je Simbachawene alitaka watu wakae kimya huku kuna watumishi wa Umma walikuwa wanakula mishahara hewa?

Je Simbachawene alitaka wapinzani wakae kimya wakati baadhi ya Viongozi wetu wakuu walipoamua kujiuzia mpaka migodi ya madini?

Yaani haya yote,adhabu yake ni kuwazuia wanasiasa wasiseme chochote mpaka wakati wa uchaguzi na wakikaidi Msajili anawafuta katika wigo wa Siasa?

Kwa nini tusitunge Sheria ambazo zitakuja kuwafanya Watanzania wazidi kuwa wamoja zaidi bila kujali tofauti zao za kisiasa,kidini,kikabila na hata kimtazamo?

Kwa nini baadhi yetu kila siku tunawaza kutunga Sheria ambazo zinalenga kubinya haki za wengine?

Kwa nini tufikirie kutunga Sheria ambazo zinatengeneza hofu badala ya Ujasiri?

Mambo haya yanatafakarisha sana sana.
Kuna tatizo kwa wasomi wetu, kuna tatizo kwa viongozi wetu, kuna tatizo kwa wananchi yetu. Wasomi wetu wameshinda mitihani yao lakini utadhani waliiba mitihani. Viongozi wetu wamechaguliwa na kutangazwa washindi lakini utadhani aliyetangazwa sie huyo aliyeshinda. wananchi wetu wanayohaki ya kugombea na kuchagua viongozi wao lakini utadhani wamezuiwa. Haya ndiyo matokeo.
Unapomsikia kiongozi mwenye degree, tena ya sheria anatamani mfumo wa chama kimoja, unajiuliza, yeye sheria alisomea wapi? Unapomsikia kiongozi na msomi wetu anaamini uchumi wa china umekuwa kwa sababu ya chama kimoja, unajiuliza alisomea wapi?

China wana wasomi wanaojitabua, china wanaweza kuuza madawa ya kulya kwenye nchi za watu wengine lakini kwao hapana, china wamefungua mipaka yao kwa uwekezaji wa nchi za magharibi lakini wanatumia bidhaa walizozalisha wenyewe. China wanaweza kuwatumikisha watu wao kama punda kwa ujira mdogo na sehemu kubwa ya mapato yatokanayo na mtu huyo yakaimarisha chama cha kikomunist cha china!

Halafu mtu anaamini kukua kwa uchumi wa china ni kwa sababu ya kuwa na chama kimoja! Uchumi wa china ni uchumi mdogo sana ukilinganisha na chumi kubwa duniani. Ukuangalia GDP ya china na Mrekani unazidiana kidogo. Ukiangalia per capita GDP ya china na Marekani au Japani tofauti yao ni mbingu na dunia. Kiongozi anabwatuka chama kimoja ndicho kimefanya uchumi wa china ukue. Hii sio sawa.
 
Back
Top Bottom