Ishakuwa hivyo. Mpumbavu ashakuwa.Hii nchi hata mpumbavu anaweza kuwa rais
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ishakuwa hivyo. Mpumbavu ashakuwa.Hii nchi hata mpumbavu anaweza kuwa rais
Kama ni nyumba ya CCM lazima uite mafundi wengi kuja kuiokoa kwani CCM hakuna mtu mwenye uchungu na Tanzania wote wapo kwa ajili ya matumbo yaoNyumba ikipata na hitilafu unaifanyaje mkuu?
MAGUFULI4LIFE
NdiyoKwani ile Bar ni yake? si pale relini?
Ishakuwa hivyo. Mpumbavu ashakuwa.
Kitendo cha wao kutishiwa na kuamini ....... kama ni kweli, basi hapo ndipo kwenye tatizo!!Wanaweza kuwa hawajafanya ushirikina ila wamewatisha jamaa kuamini hivyo kwa ujumbe feki na kumuingiza bundi mjengoni ili yao yaende.
Simbachawene ni zuzu mbumbumbu la kitupwaYaani hajui chochote kuhusu SAP's...
Haya ni maendeleo
*Kutoka katika chanzo changu cha kuaminika (Kimada wangu anayefanya moja ya kazi ndani ya Mjengo)
Taarifa ni kuwa kuna Onyo lilitolewa na mmoja wa Maafisa wakubwa wa Chama (Jina Ninalihifadhi) kwenye kikao cha siri cha dakika 15-20 na baadhi ya Wabunge kama 17 wa Chama Tawala ambao pia kwa namna moja ama nyingine hawakuwa wakikubaliana na baadhi ya Vipengele vya Muswada ule uliopitishwa.
"Nimeambiwa niwaite niwape ujumbe, Yule atakayesaliti na kukiuka makubaliano yetu ya kupitisha Muswada huu, atashughulikiwa, siku zake pamoja nasi zitahesabika na Tusilaumiane kitakachomkuta"
ilikuwa ni moja ya kauli ya Afisa huyo kwenye kikao hicho kilichofanyika ndani ya moja ya vyumba vya mkutano bungeni Mapema Asubuhi siku ya Jumatatu.
Chanzo changu kinaendelea kusema kuwa Suala la Bundi kuonekana ndani ya Ukumbi wa Bunge lilipotokea lilizidi kuwatia Hofu na kuhusishwa na masuala ya Kishirikina hivyo kila mmoja wao kutepeta na kuunga mkono kukubaliana na kilichokuwepo ili tu kunusuru Maisha yao kwa kuogopa kurogwa na kutolewa Kafara kwa kuzingatia Ujumbe waliopewa na kuoanisha maana tuliyozoea ya Bundi kuonekana kuhusishwa na Bahati mbaya, Ugonjwa, au Kifo.
Ila hili la Bundi Pengine pia inaweza kuwa ni janja tu ya kuchezeana akili kwa kumkamata ndege huyu na kumtupia ndani ya Bunge ili kuwaogofya wahusika na kuwaaminisha juu ya ujumbe waliopewa.
Vinara wa Tunguli na Ulozi Bungeni hakyanani tena Hamuendi Mbinguni!
Nchi inaelekea kuzuri sema akili zenu ndo zinaenda shimoni.Ila we jamaa kuna wakati ata kidogo ujaribu kuwaza future ya nchi na kizazi chako kijacho. Usiwe ni mtu wa kutukuza tu kisa unalipwa buku 7.
Siku wajukuu zako wakifahamu wewe ni mmoja ya waliolipeleka hili taifa shimoni unadhani watajisikiaje.
Sent from my Hisense F31 using JamiiForums mobile app
Nchi inaelekea kuzuri sema akili zenu ndo zinaenda shimoni.Ila we jamaa kuna wakati ata kidogo ujaribu kuwaza future ya nchi na kizazi chako kijacho. Usiwe ni mtu wa kutukuza tu kisa unalipwa buku 7.
Siku wajukuu zako wakifahamu wewe ni mmoja ya waliolipeleka hili taifa shimoni unadhani watajisikiaje.
Sent from my Hisense F31 using JamiiForums mobile app
Kondakta hjyo msishangaeHii nchi hata mpumbavu anaweza kuwa rais
Kuna tatizo kwa wasomi wetu, kuna tatizo kwa viongozi wetu, kuna tatizo kwa wananchi yetu. Wasomi wetu wameshinda mitihani yao lakini utadhani waliiba mitihani. Viongozi wetu wamechaguliwa na kutangazwa washindi lakini utadhani aliyetangazwa sie huyo aliyeshinda. wananchi wetu wanayohaki ya kugombea na kuchagua viongozi wao lakini utadhani wamezuiwa. Haya ndiyo matokeo.Nimesikiliza angalau kipande cha mchango wa Ndugu George Simbachawene kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa,nilichokigundua sasa ipo hoja inapazwa kwa kasi kuwa.....
1.Kufa kwa viwanda nchini Tanzania ni sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama vingi nchini.
2.Kufa kwa Mashamba makubwa yaliyotoa ajora za kutosha ni kwa sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama Vingi nchini.
3.Uwekezaji ambao haukuwa na tija kwa taifa letu kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu Vyama vingi.
4.Tatizo la ajira nchini ambalo linakuwa siku baada ya siku limesababishwa na mfumo wa Vyama vingi nchini.
5.Kashfa kubwa za Rushwa kama EPA,Escrow,Richmond,Meremeta,Dowans n.k zilisababishwa na nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
6.Kufa kwa Shirika la Reli,Shirika la Ndege/Anga kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuanzisha mfumo wa Vyama vingi.
Ndiyo maana George Simbachawene anasema nchi kama China ina chama kimoja tu na uchumi wake sasa ni imara.
Simbachawene anatamani Tanzania tubaki na chama kimoja ili tujenge taifa lenye nguvu duniani.Sijui kwa nini George hajatumia mifano ya mataifa ambayo yameendelea na yana mfumo wa vyama Vingi?
George Simbachawene ambaye kama sikosei aliondoshwa kwenye Wizara ya Madini na Mh Rais kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Mh Rais ile ya Makanikia,anasema huko nyuma nchi ilikuwa kwenye presha muda wote na akataja harakati kama..
1.Movement for Change
2.Oparesheni Sangara n.k
Kwa mtazamo wa Ndugu Simbachawene,harakati hizi zilichangia kuchelewesha maendeleo nchini.
Nakumbuka harakati hizi zlikuwa zinapiga kelele dhidi ya hiki anacholia nacho Mh Rais Magufuli kila kukicha,wizi,Rushwa,kujilimbikizia mali,Uwekezaji wa hasara.
Je Simbachawene anataka kusema Vyama vya upinzani vingekaa kimya wakati Buzwagi wanawasainisha mawaziri wetu mikataba mibovu hotelini?
Je Simbachawene anasema Vyama vya Upinzani vingekaa kimya wakati baadhi ya Mawaziri,wafanyabiasha na watumishi wa Umma wanagawana pesa za Escrow kwenye sandarusi?
Je Simbachawene alitaka Vyama vya Siasa vikae kimya wakati wakazinwa Nyamongo wanateseka na maji yenye sumu kutoka mgodi wa North Mara,wanapigwa Risasi na wawekezaji?
Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji kwenye migodi walipojigeuza miungu watu(wasiguswe),walipokuwa wanawahakisha wenyeji kinyama tena usiku wa manane bila fidia?
Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji hawa walipokuwa wanachimba madini bila kulipa kodi?huku suala la mapato wakilifanya kuwa ni Siri kati yao na Serikali
Je Simbachawene alitaka vyama ya upinzani vikae kimya wakati Twiga wanahamishwa kwenda nje kwa ndege?wanyama wanauwa na wawindaji haramu?
Je Simbachawene alitaka watu wakae kimya huku kuna watumishi wa Umma walikuwa wanakula mishahara hewa?
Je Simbachawene alitaka wapinzani wakae kimya wakati baadhi ya Viongozi wetu wakuu walipoamua kujiuzia mpaka migodi ya madini?
Yaani haya yote,adhabu yake ni kuwazuia wanasiasa wasiseme chochote mpaka wakati wa uchaguzi na wakikaidi Msajili anawafuta katika wigo wa Siasa?
Kwa nini tusitunge Sheria ambazo zitakuja kuwafanya Watanzania wazidi kuwa wamoja zaidi bila kujali tofauti zao za kisiasa,kidini,kikabila na hata kimtazamo?
Kwa nini baadhi yetu kila siku tunawaza kutunga Sheria ambazo zinalenga kubinya haki za wengine?
Kwa nini tufikirie kutunga Sheria ambazo zinatengeneza hofu badala ya Ujasiri?
Mambo haya yanatafakarisha sana sana.