kwa sababu tukikiweka tutakuwa tunawafanyia watu kazi ambayo wanaweza kuifanya, kama wangesoma Katiba wasingepata hilo shaka. Yawezekana ni kweli ndugu yangu umeisoma lakini nakushauri urudie tena ili uweze kuona lakini ukweli bado uko pale pale kwamba Katiba ya CCM imeweka jukumu kwa CCM kuwa ni kitu cha kwanza kabisa kabla ya nchi na siyo kwa maneno yenye utata ambayo mtu anaweza kuyatafsiri tofauti bali kwa maneno ya wazi kabisa ambayo kwa mtu aliyesoma katiba hiyo hatapata shida ya kuyatambua.
Naomba urudie tena kusoma lakini kama kweli utakuwa umeshindwa kabisa kukiona hicho kipengele (siyo kwa vile hakipo) basi with pleasure nitajitolea kukuonesha kilipo.
Mwanakijiji,
Muda wote huu si ungekuwa umetupunguzia posts zisizo na maana za kuulizia kipengere kwa ku post hicho kipengere? Unataka niisome hiyo katiba mara ngapi?
Mimi nimeisoma na sijakiona na ninaomba mwenzetu uliyekiona basi utuambie. Hivyo si ndivyo tunavyofanya kila siku hapa JF?