Kutoka Butiama: Exclusive news

Kutoka Butiama: Exclusive news

kwa sababu tukikiweka tutakuwa tunawafanyia watu kazi ambayo wanaweza kuifanya, kama wangesoma Katiba wasingepata hilo shaka. Yawezekana ni kweli ndugu yangu umeisoma lakini nakushauri urudie tena ili uweze kuona lakini ukweli bado uko pale pale kwamba Katiba ya CCM imeweka jukumu kwa CCM kuwa ni kitu cha kwanza kabisa kabla ya nchi na siyo kwa maneno yenye utata ambayo mtu anaweza kuyatafsiri tofauti bali kwa maneno ya wazi kabisa ambayo kwa mtu aliyesoma katiba hiyo hatapata shida ya kuyatambua.

Naomba urudie tena kusoma lakini kama kweli utakuwa umeshindwa kabisa kukiona hicho kipengele (siyo kwa vile hakipo) basi with pleasure nitajitolea kukuonesha kilipo.

Mwanakijiji,

Muda wote huu si ungekuwa umetupunguzia posts zisizo na maana za kuulizia kipengere kwa ku post hicho kipengere? Unataka niisome hiyo katiba mara ngapi?

Mimi nimeisoma na sijakiona na ninaomba mwenzetu uliyekiona basi utuambie. Hivyo si ndivyo tunavyofanya kila siku hapa JF?
 
Mwanakijiji,

Muda wote huu si ungekuwa umetupunguzia posts zisizo na maana za kuulizia kipengere kwa ku post hicho kipengere? Unataka niisome hiyo katiba mara ngapi?

Mimi nimeisoma na sijakiona na ninaomba mwenzetu uliyekiona basi utuambie. Hivyo si ndivyo tunavyofanya kila siku hapa JF?

good point.. wacha na mimi niende kukitafuta..
 
Bubu huwa unaongea lakini kusema bado, kuongea na kusema ni vitu viwili tofauti..

Soma, kwanza....I went through lenghts to explain hypothetical kuwa ingekuwa mazingira ya kawaida, absense ya Mkapa ingeweza kuwa chochote, bubu kasema Mkapa kakimbia, I didnt say that...Point ni tunalishwa habari za hivi hivi sababu ya kiu iliyopo ambayo haiongezi maendeleo.
.Sasa unachojua wewe siyo ndio matatizo yote ya Tanzania, wewe unajua skendo zote, nadhani hata ukiamshwa usiku wa manane, mtiririko huo utautaja kirahisi tu...

Mazingira ya kawaida unayoyasema hayapo. Mwalimu alitwambia kwamba Ikulu ni nyumba takatifu ambayo si nyumba ya biashara. Lakini fisadi Mkapa kwa uroho wa utajiri aliokuwa nao, akaona ni wakati muafaka wa yeye kuanzisha biashara akiwa Ikulu na kuyadharau yale aliyoyasema Mwalimu. Pia siri ikafichuka kwamba alijipatia Kiwira Coal Mining katika mazingira ya kutatanisha na kuhusika kwa karibu zaidi na ununuzi wa rada ambayo pesa yetu $12 millioni ililipwa kama commission kwa wakala mhindi Mtanzania ambaye hajulikani alichaguliwa vipi na yeye huyo huyo alikuwa wakala wa ununuzi wa ndege ya Rais iliyonunuliwa wakati Mkapa kabakisha miezi mitatu ya kumaliza awamu yake, ununuzi wa helikopter na magari ya jeshi.

Kwani kujua skendo zote ni dhambi!? 😕
Zinaandikwa kwenye magazeti yote ambayo yanapatikana mtandaoni , hivyo kila anayetaka kujua nini kinaendelea ana fursa ya kufahamu.

Naam siyajui matatizo yote ya Tanzania maana mimi simo kwenye siri kali ambayo hata kuwataja mafisadi wanaogopa kwa kuwa nchi italipuka. Lakini machache ninayoyajua naamini kwamba yanachangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya Watanzania wengi waishi katika maisha ya dhiki kubwa, kitu ambacho kingeweza kuepukwa.

Mimi ni Mtanzania napenda kufuatilia yote yanayoendelea Tanzania yawe mabaya au mazuri, je kuna kosa gani ya kujua mabaya na mazuri ndani ya nchi yetu? 😕
 
Topiki zote kuhusiana na mkutano wa CCM kijijini alikozaliwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zimepoteza mwelekeo na zimezuka na kunganishwa unganishwa mpaka zimepoteza dira kama CCM yenyewe.
Ni kweli kwamba hakuna hata moja lililozungumzwa ambalo linahusiana na matarajio ya wengi kuliona ,hata wale waliokuwa wakitupa matumaini kwamba wao wapo karibu na wengine kujisifu kama inzi wa kijani nao wameingia mitini ,na kutuacha gizani.
Inasemekana matokeo ya Uchaguzi wa Zimbabwe ni Jumatatu je habari hizi za mkutano wa Butiama ni lini zitajulikana ,hivi hakuna hata mmoja aliepata dondoo ,wale makomandoo wa habari wamekwenda wapi ,jamani waulizieni isije kuwa wametiwa mikononi ?
 
mkuu samahani lakini si tulishatoa report ya ndani ya CC?? Therefore NEC won't have any news since they will just deal with what was decided during CC meeting ie CUF/CCM and blah blah rhetoric nyingi tu kuhusu hali ya siasa na uchumi.

Molex, kamati kuu haiko juu ya Halmashauri Kuu ya Taifa; HKT wanaweza kutengua jambo lolote lililoamuriwa na Kamati Kuu.. tafadhali soma Katiba.
 
Mimi nilishabet my bottom dollar and I am willing to put my name on the line saying there is nothing new coming.

Apart from the usual spinning of course.

Kama ripoti za alichofanya Mwinyi ni kweli I have a new found respect for this Mzee ambayo ina reverse vitu vingi vibaya alivyofanya while in power.
 
nasikia wajumbe bado wana hammer maazimio yao na pindi tukiyapata tutawaletea moja kwa moja kupitia broadcast.com na kupitia bongoradio.com
 
As expected, Watanzania wamepigwa bao la tobo! Ushahidi hautoshi hauna maana, tutaongea tena Mwezi wa Tano.

Sasa kikao cha Bunge kinakuja mwezi huu wa April, tusikie sokomoko la Bungeni tujuemkao wa kikao maalumu cha NEC kitakuwaje!
 
jamani kuna mambo ambayo wasingeweza kuyatolea maoni kwa mujibu wa vyanzo vyetu Butiama na wahusika hao wameshangaa kuona watu wanasubiri watolee maoni au maamuzi mambo hayo. Chanzo kimoja cha kuaminika kimeishangaa JF kwa kutegemea mambo makuu wakati hapa ndipo kisima cha fikara mamboleo.

a. Suala la EPA wasingeweza kulitolea maamuzi kwani ripoti yenyewe Rais bado hajapewa hadi kina mwanyika wamalize kazi zao na wana miezi sita kufanya hivyo.

b. Suala la kuwashughulikia waliotajwa kwenye Kamati ya Mwakyembe ni vile vile. Bunge lilishatoa mapendekezo yake. Ofisi ya Waziri Mkuu akaunda tume kuona jinsi mambo hayo yatatekelezwa ripoti ambayo amekabidhiwa siku chache zilizopita na baada ya hapo kwenye kikao kijacho Waziri Mkuu atatakiwa kutoa maelezo ya jinsi serikali imeshughulikia mapendekezo ya Bunge.

Hivyo katika masuala hayo mawili wasingeweza kuchukua uamuzi wowote ambao ungeonekana kuingilia uchunguzi au mchakato unaoendelea maana walioleta suala la Richmond Bungenni ni CCM, kamati iliyofuatilia majority ni CCM na Bunge lililosababisha waziri Mkuu ajiuzulu ni la CCM sasa kwanini NEC ya CCM iingilie kati?

So, naamini hapa ni subira inayotakiwa.
 
MMJJ,

Au ndo agenda yenyewe ya siri ya mwezi May kwenye Kikao Maalumu?
 
Mkjj ahsante kwa yote unayofanya lakini mkuu husiwawekee rehani hao waigizaji sinema.

Ajenda ya siri najua umeshaisikia so unajua wazi usanii umevuka mpaka.
 
kuhakikisha yatakayoandikwa hapa kuhusiana na kikao cha butiama yanakuwa sahihi, najitolea mimi kama kada kuwa makini zaidi na kitakachoandikwa maana kuna wapishi wa habari humu !

Sasa wapishi ingieni kazini huku nikisafisha kope zangu !
 
Wenyewe walidhani wamefukuza waandishi wote.... kumbe yule nzi anayepenya kwenye kuta zao alikuwemo.. na wiki hii nzima habari za kile kilichofanywa "sirini" zitaanza kuandikwa..
 
na baada ya hapo wiki inayofuata nitaandika wizi unaofanywa na mwenyekiti taifa wa chama fulani kwa kutumia falsafa ya muasisi wa chama cha mapinduzi !

Mwenyewe anadai chama kipya, lakini falsafa anayotumia ni ya ccm !
what a sad story !
 
 

Attachments

  • mizengo pinda.JPG
    mizengo pinda.JPG
    17.4 KB · Views: 83
Back
Top Bottom