Du! Sasa nimeelewa kwanini taasisi zote za serikali hazina fedha,kumbe
fedha ziko mifukoni mwa watu kwa shughuli ya kujitangaza!
EL tunasema ni fisadi na ananunua watu kwa pesa,
yeye si waziri wala nini,Hivyo uwezekano wa kuwa anatumia fedha ya serikali au gari za serikali ni kidogo.
sasa hawa mawaziri wanaotangaza nia kwa gharama kubwa
fedha wamezipata wapi, wakati serikali haina pesa?
Kwa nini kama wanaielewa hali halisi ya uchumi wa nchi
wasingeitisha mkutano mmoja,wakatangaza nia
ili kuokoa fedha inayotumiwa na kila mmoja kwa wakati wake
huku wote ni chama kimoja,wote wanavaa unifomu moja kijani,
lakini kutangaza wanasambaa mikoa tofauti tofauti na kuhamisha washabiki
kutoka mikoa ya mbali kwa gharama kubwa ya chakula na malazi?
Yangu macho,lkn najifunza kwamba nchi ni masikini
ila watawala ni matajiri.