Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Huku kusali kwenye mikutano ya Kisiasa ni kupotezeana time tu, mbona wenzetu haya huwa hatuyaoni?
 
Ninaamini Nchemba anajua fika hawezi kuupita msitu wa Lowasa, Membe, Wasira, Mwandosya, Pinda, na wengineo ambao ni wakongwe wa siasa. Ila anafanya investment ya mwaka 2025. Ni kama tu Kikwete alivyojitupa kwenye kuwania nafasi hiyo mwaka 1995.

Unadhani 2025 hamna watu wanataka urais? Kuna akina January, Nchimbi, Mtoto wa mwinyi, na yule wa mkwere! Kaa chonjo Sana! Halafu usimsahau Kigwanocs
 
Naona hii sasa imekuwa ndio fashion na utamaduni kwa wana-CCM wanaosaka uraisi.

Muda huu ninapoandika kuna magari aina ya coaster yamekodishwa ili kubeba wanafunzi wa chuo kikuu na kuwapeleka Chuo cha Mipango Dodoma kwenye tukio la Mwigulu kutangaza nia.

Nasikitika kuona hata wanafunzi wa vyuo vikuu nao hawajitambua!

Binafsi nimebaki naangali tu tukio hili nikiwa kwenye gate kubwa la kuingilia na kutoka hapa chuoni.
Ingekuwa ni Chadema ungethubutu kuongea maneno haya? Mnavokemea suala la wanafunzi kutumika kisiasa mnabidi mkemee kotekote na siyo kuwa na double standards. Kwingine mnasifia, kwingine mnakemea.
 
Wanaanza na maombi safi sana.Wassira kulikuwa hamna sala

MC kama kalewa pombe vile! Ona wewe wale Mabahai walisali mchana kutwa mungu wao ashushe moto ila ziiii na Gideon alifanya nn unakumbuka? Haturembi sisi
 
Jamaa anaweka long term plan.Nadhani baadae yeye na January watapokezana kama Lowasa anavyotarajia kupokezana na JK
 
Tunampongeza Mh Mwigulu Nchemba kuamua kuomba ridhaa ya wanachuo wa vyuo vikuu Dodoma kutangaza nia yake ya kuwania mbio za urais hapo October. Nipo hapa wanafunzi ni wengi ajabu haijawahi kutokea. Hongera sana Mhe.
 
Vyama vya upinzani vijifunze demokrasia toka ccm sasa
 
Back
Top Bottom