Nimeitoa paala
Leo taifa letu linapita katika historia nyingine , historia hiyo ni ile ambayo wengi wetu tunaisubiri hatma yake 25.October , pale Tanzania itakapo apisha Rais MPYA wa awamu ya5 kuelekea miaka 50 NYINGINE
Na katika mchakato huu kwa sasa tupo katika hatua muhimu , hatua ya kuwapima viongozi wanao jitokeza kuomba ridhaa hiyo
Kwa sasa tumeanza Na ccm Na tunazidi kuwaona wale wenye nia ya kutaka kuliongoza taifa wakijitokeza na kujinadi
Kwa sababu ni taifa langu Na Rais anayetafutwa ni Rais wa nchi yangu siwezi kujitenga nyuma juu ya kuwaongelea wale wanao ongelewa kuwa marais wetu
Jana nimesikia Mh Lowassa Leo nimemsikia Mh Mwigulu Na bahati mbaya sikimsikia Mh Wasira
Nasimama hapa kwanza kuwapongeza wote ambao wanajitokeza kulibeba hili gudulila la Tanzania .Make nikikiria ni sio swala la MTU kukurupuka .
Kwa namna nilivyo Pima wote ambao wamejitokeza wanaonesha wanao uwezo tena uwezo mkubwa kuwaza kuluongoza taifa letu nawapongeza
Nasimama kidogo kuchambua kidogo iliyokuwa hotuba ya Mwigulu Leo
Mwigulu ni kijana aliyo Na maono na moyo juu ya kuisaidia Tanzania ,
Lakini katika hotuba YAKE ya Leo sivyo nilivyo tarajia , haijanigusa niseme ukweli hata mkunipiga mawe
Hotuba ya Leo ya Mh Mwigulu sio ya "presidential material " ilikuwa ni hotuba ya kawaida mno na ya mambo Yale Yale yanayozungumzwaga na watu Hawa wale wale yasoyotendeke
Hotubu ya Mh Mwigulu ilikuwa na mapungufu haya niliyouaona Mimi
Ukizingatia ukubwa na unyeti wa nafasi aliyokuwa akiomba kwa chama chake
1.Hotuba yake haikuwa na kipa umbele au vipa umbele .... Mh Hamisi kigwangwala yeye amejitanabaisha Kama kipa umbele chake ni ajira kwa vijana
Sisi Kama wasomi unapo taja vipa umbele vyako ndipo unapo tupa nafasi ya kujadili kuwezekana na kutokuwezekana kwa vipa umbele hivyo
Taifa letu tumekwama kwa kuwa ni taifa lisilo na vipa umbele na taifa lilo na vipa umbele visivyojadilika na mwisho haviwezi kutendeka
Mh Hamisi katika ajenda yake hiyo tunamuuliza utatekelezaje ajira katika taifa ambalo 56% ya vijana na watu wazima hawana Elimu? Kigwanomics amejikita kusema mfumo wake wa ajira utalenga formal education na informal Education ambapo ataongeza nguvu kwenye mfumo wa ajira rasimi na zisizo rasimi
Mh Lowassa yeye amejielekeza kwa kusema vipa umbele vyake Vya kwanza mpaka cha NNE ni "Elimu"
Kosa la pili
2.Hotuba ya Ndugu Mwigulu Nchemba haijazungumzia kabisa mambo ambayo ni national core Mfn hajazungumizia muungano in content and contest, hajazungumzia amani umoja na mshikamano wa watanzania in content and contest as a presidential contests, hajazungumzia Tanzania na nchi za nje Sera Zake ambalo ni muhimu Sana kwa diplomasia ya nje na ambalo nadhani mataifa mengi kwa sasa yatakuwa yanaliangazia hilo
Kosa la 3
3.Ametulimia mda mwingi kuilamu serikali iliyopo as if yeye sio sehem ya serikali hii! Analaumu makampuni makubwa na matajiri wakubwa kukwepa kulipa kodi wakati yeye ndo ndo mkusanya kodi na mtunga Sera
..sasa Kama yeye analalamika nani ni responsible? .Mambo haya angeyazungumza Dr Slaa au Lipumba ni sawa ila sio Waziri
4.kuna wakati amesema yeye ni mjumbe wa kamati ya ushauri ya uchumi Na Sera hivyo wizara hiyo anaijua Sana ,lakini akashindwa kuja Na njia mbadala juu ya mporomoko wa shilingi yetu unao simamiwa na idara hiyo ambayo yeye ni mjumbe Na umekuwa akifanya hapo kabla ya naibu Waziri wa wizara
Pamoja na hyo machache niliyo yataja Mh Mwigulu anaweza kuwa hazina na president material kwa Siku zijazo...!