Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.

'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.

Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.

Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni

Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.

Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu

Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa

Dr Kilawa the Iron

Huna hata aibu kutamka haya
 
1 & 4 is event related hazina maana kabisa

..kwangu mimi hayo yanatoa picha fulani kwa mtangaza nia.

..huyu Mwigulu anaandikwa mpaka kwenye mawe makubwa kwenye njia zote kuu hapa nchini.

..sasa tunataka kuona kama kweli anaungwa mkono anapojitokeza hadharani.

..mkutano ambao uko well organized na kila mtu anazingatia muda na jukumu alilopewa unanipa confidence kwa mtangaza nia mtu wa aina gani kwamba anapenda shughuli zake ziendeshwe kwa mipangilio na nidhamu.

NB:

..nakubali kwamba umati wa Lowassa ni nguvu ya pesa. Sasa nataka mtu ajaze umati bila kutumia pesa; kwasababu watu wanamuamini.

cc Kimweri
 
Last edited by a moderator:
TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.

'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.

Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.

Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni

Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.

Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu

Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa

Dr Kilawa the Iron
Unajua please serikali in posh indwelling inasingizia taasisi binafsi kuwaibia au watumishi wa umma kuihujumu! Ndini gia anayo kuja nayo Mwigulu!
 
mwigulu simwamini hata kidogo yupo kama babake hapo magogoni kila siku nitawafunga wauza unga, waliokula hela za epa, escow inaishia hewani maccm ndivyo yalivyo yanafanana.
 
Dah! okei, ni hivi,
anamaanisha yeye akiwa rais!

kama ameshindwa kulisema ndani ya bunge kwa nini mikataba bado ni siri, anataka atuaminishe akiwa rais ndio ataanza yeye kufanya haya? ccm wote walewale tu.
 
kutangaza nia kwa style hii kunaipa kamati za uteuzi nafasi nzuri ya kufanya maamuzi mazuri badala ya kununua mbuzi kwenye gunia maana watakuwa wameshapima mwelekeo wa upepo. Binafsi kwa kuangalia tukio la jana la Lowassa na leo la Mwigulu nimeondokwa na woga niliokuwa nao kuhusu nguvu ya Lowassa. Si lolote, si chochote. CCM wakiamua kufanya maamuzi magumu ya busara wanaweza kabisa kumuuza kapuku kama mwigulu na akanunuliwa na wapiga kura.

Mkuu ngoja kwanza kesho tumsikilize wa Mwitongo naye ndipo hoja yako inaweza kuwa na mashiko. Ila the bottomline ni kwamba ni rahisi kumuuza Makongoro kwa wananchi kuliko Mwigulu. Maana yangu ni kwamba kesho Makongoro akionyesha vision inayokubalika, ni bora yeye kuliko Mwigulu. Nasema hivi kutokana na hizi kashfa zinazonyong'oneza CCM na serikali yake
 
Nimeitoa paala

Leo taifa letu linapita katika historia nyingine , historia hiyo ni ile ambayo wengi wetu tunaisubiri hatma yake 25.October , pale Tanzania itakapo apisha Rais MPYA wa awamu ya5 kuelekea miaka 50 NYINGINE

Na katika mchakato huu kwa sasa tupo katika hatua muhimu , hatua ya kuwapima viongozi wanao jitokeza kuomba ridhaa hiyo

Kwa sasa tumeanza Na ccm Na tunazidi kuwaona wale wenye nia ya kutaka kuliongoza taifa wakijitokeza na kujinadi

Kwa sababu ni taifa langu Na Rais anayetafutwa ni Rais wa nchi yangu siwezi kujitenga nyuma juu ya kuwaongelea wale wanao ongelewa kuwa marais wetu

Jana nimesikia Mh Lowassa Leo nimemsikia Mh Mwigulu Na bahati mbaya sikimsikia Mh Wasira

Nasimama hapa kwanza kuwapongeza wote ambao wanajitokeza kulibeba hili gudulila la Tanzania .Make nikikiria ni sio swala la MTU kukurupuka .

Kwa namna nilivyo Pima wote ambao wamejitokeza wanaonesha wanao uwezo tena uwezo mkubwa kuwaza kuluongoza taifa letu nawapongeza

Nasimama kidogo kuchambua kidogo iliyokuwa hotuba ya Mwigulu Leo

Mwigulu ni kijana aliyo Na maono na moyo juu ya kuisaidia Tanzania ,

Lakini katika hotuba YAKE ya Leo sivyo nilivyo tarajia , haijanigusa niseme ukweli hata mkunipiga mawe

Hotuba ya Leo ya Mh Mwigulu sio ya "presidential material " ilikuwa ni hotuba ya kawaida mno na ya mambo Yale Yale yanayozungumzwaga na watu Hawa wale wale yasoyotendeke

Hotubu ya Mh Mwigulu ilikuwa na mapungufu haya niliyouaona Mimi
Ukizingatia ukubwa na unyeti wa nafasi aliyokuwa akiomba kwa chama chake

1.Hotuba yake haikuwa na kipa umbele au vipa umbele .... Mh Hamisi kigwangwala yeye amejitanabaisha Kama kipa umbele chake ni ajira kwa vijana

Sisi Kama wasomi unapo taja vipa umbele vyako ndipo unapo tupa nafasi ya kujadili kuwezekana na kutokuwezekana kwa vipa umbele hivyo

Taifa letu tumekwama kwa kuwa ni taifa lisilo na vipa umbele na taifa lilo na vipa umbele visivyojadilika na mwisho haviwezi kutendeka

Mh Hamisi katika ajenda yake hiyo tunamuuliza utatekelezaje ajira katika taifa ambalo 56% ya vijana na watu wazima hawana Elimu? Kigwanomics amejikita kusema mfumo wake wa ajira utalenga formal education na informal Education ambapo ataongeza nguvu kwenye mfumo wa ajira rasimi na zisizo rasimi

Mh Lowassa yeye amejielekeza kwa kusema vipa umbele vyake Vya kwanza mpaka cha NNE ni "Elimu"

Kosa la pili

2.Hotuba ya Ndugu Mwigulu Nchemba haijazungumzia kabisa mambo ambayo ni national core Mfn hajazungumizia muungano in content and contest, hajazungumzia amani umoja na mshikamano wa watanzania in content and contest as a presidential contests, hajazungumzia Tanzania na nchi za nje Sera Zake ambalo ni muhimu Sana kwa diplomasia ya nje na ambalo nadhani mataifa mengi kwa sasa yatakuwa yanaliangazia hilo

Kosa la 3

3.Ametulimia mda mwingi kuilamu serikali iliyopo as if yeye sio sehem ya serikali hii! Analaumu makampuni makubwa na matajiri wakubwa kukwepa kulipa kodi wakati yeye ndo ndo mkusanya kodi na mtunga Sera
..sasa Kama yeye analalamika nani ni responsible? .Mambo haya angeyazungumza Dr Slaa au Lipumba ni sawa ila sio Waziri

4.kuna wakati amesema yeye ni mjumbe wa kamati ya ushauri ya uchumi Na Sera hivyo wizara hiyo anaijua Sana ,lakini akashindwa kuja Na njia mbadala juu ya mporomoko wa shilingi yetu unao simamiwa na idara hiyo ambayo yeye ni mjumbe Na umekuwa akifanya hapo kabla ya naibu Waziri wa wizara

Pamoja na hyo machache niliyo yataja Mh Mwigulu anaweza kuwa hazina na president material kwa Siku zijazo...!
 
Yap ulikuwa mbaya na kwake yeye umekuwa mbaya zaidi na zaidi, si mwanauchumi yeye atleast ningetegemea angeokoa jahazi lisizame kabisa lakini kwake yeye tunaona ndo tunazidi kuzama kabisa, yeye ni msafi sawa unakumbuka majibu yake ya Escrow account pale bungeni zaidi ya kutupiga changa LA macho? yeye si mpiganaji wa rushwa mbona ameshindwa kushughulikia hayo machache kny utawala wake mdogo wa uwaziri ndo seuze nchi ataiweza?? Analalamika na mfumo mbovu wakati naye yumo ndani? Basi kifupi naye ni mbovu.......... Sera hizi hizi ndo zilimuingiza Kikwete matokeo yake leo tunalia tu....... Hakuna jipya kabisa wote ni wale wale.........

Tatizo watanzania mmeumwa na nyoka, mnakuwa wagumu kuamini mnapoona majani yanatingishisha.

Lakini there is something on him. Ila yuko wrong place at wrong time. Place kwa maana ya serikali ya ccm, time kwa maana ya awamu ya nne.
 
Ww na mbwembwe zote nikadhani unataja hata moja unayoifaham kumbe umerudi kule kule unakodai alichemkia?
 
Alafu utakuw ujamsikia vizuri pia utakuwa mmoja wapo wa kuuza dawa Za serikali
 
anajieleza kama vile yeye si ccm.

Wanataka kufanya nchi hii ya
majaribio....kila mtu anataka uongozi tena uraisi.... Ivi uraisi umekua rahisi kiasi iki??

Uko nyuma bado kuna wenzake kibao wanafata. Eti nia... Uuuuuiiiii tutakoma safari hii
 
Tone ya kuwafunga mafisadi na kuwafilisi inapaswa kuwa juu kuliko tone ya kuzungumzia jambo lingine lolote.
 
Tusiwe wajinga wa kufikri yeye alikuwa anazungumzia wizi wa dawa mahospitalini na kwamba dawa hizo hupelekwa kuuzwa kwe maduka ya nje hivyo amewalenga wale wanaoiba dawa na si wengine.
Mwigulu ni muongo mkubwa! serikali haipeleki fedha za kununulia dawa! msd imekopwa mpaka basi, sasa hizo dawa za kuibiwa zinatoka wapi?
 
Hahaaa...... kamanda Mbowe twende,hawa wajinga nao wanatuunga mkono kwani hakuna tofauti na mtu ambaye anamcheka mkewe au mumewe kwa majirani kuwa anakojoa kitandani na huku akiendelea kulala naye! Pumbavu sana.
 
Back
Top Bottom