waziridagaakirumba
Member
- Jul 29, 2023
- 29
- 67
- Thread starter
- #61
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizo za kukaanga siuziNdoo ya litr 20, dagaa waliokaangwa bei gan?
muda mrefu mkuu maana ,mtaji ulikuwa mdogo ,kiasi kwamba ilinibidi kupunguza baadhi ya matumizi ambayo siyo ya lazima ili niendelee kuishi mjiniilichukua kama muda gani Ku rise hiyo capital mkuu??
Hongera sana unao uthubutu kwakweli
UtanipigiaNitahitaji ushauri wako. Mtaji ninao Mimi ni bihawana graduate wa CBA
UtanipigiaNitahitaji ushauri wako. Mtaji ninao Mimi ni bihawana graduate wa CBA
Ok ni SawaUtanipigia
Duh aisee Mungu amsaidieKuna jamaa moja anajuta kuacha biashara ya kuuza mchele kwa magunia baada ya kukimbilia kuajiriwa akakuta anapokea mshahara laki tatu. Alisoma akahitimu chuo akasubiri ajira kwa muda mrefu akaona isiwe taabu akajiingiza kwenye biashara ya kuuza mchele. Kwa vile alikuwa ana kimuhemuhe cha kuajiriwa akitarajia kupata mshahara mnono na pensheni uzeeni hatimaye alipata ajira na kuitosa biashara iliyomtoa kimasomaso na kumpatia mke mzuri kwa vitu vipya alivyojaza chumbani kwake. Sasa anatamani mamilioni ya pesa aliyokuwa anayapata kwenye mchele
Nimejaribu kukucheki whatsApp haupatikaniHabari yako mwanajamii, nina imani ulipo unaendelea vema, kama haupo sawa Mungu akutangulie katika jambo lako.
Leo tena nimepata muda wa ku-share vitu nilivyopitia katika maisha yangu.
Mimi ni mzaliwa wa Nyanda za Juu Kusini (Songwe -Mbozi) nimesoma shule ya primary Songwe Mwaka 2008 na nikajiunga na elimu ya Secondary huko kwetu Songwe, na high level nimesoma BIHAWANA secondary iliyopo kanda ya kati .
Japo nilisoma kwa kuunga unga kwa sababu ya uchumi wa Nyumbani haukuwa sawa,Baadae nikajiunga na Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) kwani nilifurahi sana kujiunga na elimu ya juu sababu ilikuwa Ndoto yangu ,kwa maana hiyo nilijua Ndoto zangu zimetimia na kuwasaidia wazazi wangu ambao walipata shida sana muda wa kunisomesha na muda huo nilikuwa mnufaika wa mkopo.
Maisha ya Chuo yaliendelea ndani ya miaka minne kwani nimesoma fani ya afya(UKUNGA)-MIDWIFERY.
Mungu ni mwema nilifanikiwa kuhitimu masomo yangu ya chuo kikuu na baada hapo nilienda kwenye mafunzo ya vitendo (internship) ndani ya mwaka mmoja katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza(Sekeo Toure).
Baada ya hayo mafunzo hayo kuisha ikanibidi niendelee na maisha ya mtaani ya kawaida ili kujipatia riziki na muda huo naendelea kutuma maombi ya kazi kwenye taasisi mbalimbali japo ilikuwa ngumu sana kupata maana taasisi nyingi zilinipa masharti ambayo niliona kama magumu kwangu,kwani walikuwa wanahitaji wenye uzoefu na mimi nilikuwa naambiwa nifanye kazi bila malipo ndani ya miezi mitatu ili nipate uzoefu kwani ilinipa ugumu kufanya kazi bila malipo nilikuwa sina chanzo chochote cha kujipatia fedha ya kujikimu (chakula na pango),maisha yangu yalikuwa magumu sanaa kwani nilikuwa sina kazi maalumu.
Hatimae nilipata kazi ya kufundisha chuo cha afya huko Rorya sehemu moja inaitwa SHIRATI nilifanya kazi kwa nguvu na moyo wote kwani nilikuwa nimeteseka mtaani kwa kufanya kazi za kuunga unga ili kujipatia kipato lakini bado juhudi zangu hazikuzaa matumaini kwani malipo yalikuwa ya shida sana mpaka ikanibidi nishindwe kujikimu.
Nilishindwa kuendelea na kazi na Kurudi tena MWANZA kwani nilipazoea MWANZA sana kwa sababu niliishi kwa muda mrefu na kuzoea mazingira japo nilikuwa sina kazi maalumu ya kujipatia kipato.
Nilipoona hali yangu ngumu kuna jama yangu alinikopa fedha shilingi laki moja na nusu(150,000/=) ambayo tayari nilikuwa nime-plan kuanza biashara ya dagaa wakavu nilikuwa nanunua na kuuza minada ya karibu Mungu ni mwema niliona maisha yangu yanabadilika na kujikimu kabisa.
Mtaji wangu ulikua mpaka milioni mbili(2,000,000/=) hivyo nilijikuta nachukua mzigo mkubwa zaida na kupata faida zaidi nikaanza kupeleka mikoa ya karibu ,kila hatua Mungu alinisaidia kwani mtaji wangu ulikuwa sana kuliko matarajio yangu nilifikisha zaidi ya million 25 (25,000,000/=) nilitanua wigo zaidi ikanibidi nifungue ofisi soko kuu la dagaa Mwanza(KIRUMBA MWALONI MWANZA)
Namshukuru Mungu biashara yangu ilienda vizuri na kuuza kwa bei ya JUMLA na kuwauzia wateja wa mikoani.
HITIMISHO.
Biashara ya chakula kama dagaa ni bidhaa inayolenga watu wenye kipato cha chini na watu wa chini ndio wengi kwa hiyo ni moja ya biashara inaweza kukutoa kimaisha.
Japo biashara ni nyingi zinazolipa na hii pia inakutoa endapo ukapambana.
Pia vijana waliomaliza vyuo na ambao hawajasoma usikate tamaa maana kila jambo linahitaji umtangulize MUNGU.
KWA AMBAE ATAHITAJI MZIGO/DAGAA/USHAURI KWENYE HII KAZI UNAWEZA KUNITAFUTA WHATTSAPP/PIGA .
0755213580.
AU UNAWEZA KUFIKA KIRUMBA MWALONI MWANZA KWENYE SOKO LA DAGAA
View attachment 2702048