Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Ninatamani kuona nape akiishi milele bila kufa!! Ninatamani moses nnauye angekuwa hai akamsikia mtu anaejinasibu kuwa mwanae anavyosema... Ninatamani siasa hizi za maji taka nione mwisho wake. Ninatamani zaidi matusi yaruhusiwe kikatiba. Ninatamani pia hawa wanaotukana leo wasife bila kuyapata yoote wanayotapika hivi sasa kwa jina la siasa.
 
Zipo nyingi sana tu tatizo wengi wanaompenda sio wa vijiweni wala wapiga kelele,

I wish ungejua vzr iringa, mi mkazi wa ir, hao wapiga kelele ndo walimchagua Kipindi kilichoisha, na kwa maendeleo haya mwakalebela hachomoki mark my words
 
mwakalebela hali ni mbaya sana. pamoja na polis kutumika kumnyanyasa mchungaji msigwa na wana mabadiliko hali ni mbaya sana kwa mwakalebela.
 
Tff aliiba akafukuzwa sasa iringa ndio watakubali kuibiwa? Sio wajinga atasubiri miaka mia
 
Hii sio nyomi kumbe wewe huijui iringa,tafuta picha za lowasa alipokuwa iringa uone
 
Magazeti ya Leo yana hii habari ya mgombea urais kupitia ccm Dr John Magufuli kwenye Kampeni zake kutaka ushindi wa asilimia 99 dhidi ya wapinzani wake UKAWA .

Hii isitafsiriwe kama ni propaganda za kumnanga huyu mgombea lakini kwa vile anaomba ridhaa ya kupata nafasi ya kuwa rais, basi kauli na matendo yake lazima vijadiliwe kwa kina.

Pamoja na majigambo ya kisiasa lakini kuna mambo lazima yaashirie uhalisia, kwenye siasa hizi za ushindani ni uendawazimu na ndoto za alinacha kudhani au kujiaminisha au kupaza sauti jukwaani kuwa unataka ushindi wa asilimia 99.

Kuna wakati huwa naona Kama magufuli anapoteza dira mwelekeo na dhamira yake ya kuirudisha chama chake madarakani au anafanya makusudi kukichinjia jukwaani Peupe au elimu yake inamtosha yeye tu kwenye fani yake lakini si kwenye ulingo wa siasa.
 
Miye nilikuwepo uwanjan samola sijaona umakin Wa magufuli maana anazungumzia is hu ya national milling atairudisha na kuifufua hapo hapo anamshika mfanya biashara maarufu hapa mjin kwamba n msafi wakat madudu yake tunayajua na Hawa ndio wamegeuza national miling kuwa store ya bidhaaa zao aende zake huko kura yangu n siri

Ningekuwepo ningemuukiza anajua kilichoua hizo national milling nchi nzima?
 
Exaggeration za kisiasa ni ruksa kipindi hiki cha siasa. Hakuna ubaya kuomba ushindi wa 99% .. swali ni kwamba alikuwa anaongea na sisi wa mjini au wa vijijini maana kule 90% CCM wala hawaoni kuwa ni unrealistic
 
Kuna marafiki zangu ambao wao ni CCM damu...

Mwanzoni walikuwa wana imani sana na Magufuli...

Lakini kampeni zilivyoanza tu, nikawashtua kuwa nina wasiwasi Magufuli hana washauri wazuri...

Na kadiri siku zitavyokuwa zikisogea maneno yangu yatadhihirika...

Guess what, sasa hivi hata hao makada wamechoshwa kw kuyatazama mambo ya ajabu ayafanyayo bwana Pombe...
 
Ni mambo ya kawaida katika siasa, japo ukweli ni kuwa hakuna mwenye uwezo wa kushinda kwa 99% katika medani za ushindani miaka hii. Lakini hizo ni propaganda za kisiasa na ni kitu cha kawaida sana. Niwashangae nyie mnaoshangaa.
 
DSC00851.jpg
 
Ametumia muda wote wakampeni kutukana. Kwa kweli mungu atamlipa
 
Back
Top Bottom