Magazeti ya Leo yana hii habari ya mgombea urais kupitia ccm Dr John Magufuli kwenye Kampeni zake kutaka ushindi wa asilimia 99 dhidi ya wapinzani wake UKAWA .
Hii isitafsiriwe kama ni propaganda za kumnanga huyu mgombea lakini kwa vile anaomba ridhaa ya kupata nafasi ya kuwa rais, basi kauli na matendo yake lazima vijadiliwe kwa kina.
Pamoja na majigambo ya kisiasa lakini kuna mambo lazima yaashirie uhalisia, kwenye siasa hizi za ushindani ni uendawazimu na ndoto za alinacha kudhani au kujiaminisha au kupaza sauti jukwaani kuwa unataka ushindi wa asilimia 99.
Kuna wakati huwa naona Kama magufuli anapoteza dira mwelekeo na dhamira yake ya kuirudisha chama chake madarakani au anafanya makusudi kukichinjia jukwaani Peupe au elimu yake inamtosha yeye tu kwenye fani yake lakini si kwenye ulingo wa siasa.