Kutoka Kenya: Mchakato wa wenzetu kumng'oa Naibu Rais unaumbua ubovu wa katiba yetu

Kutoka Kenya: Mchakato wa wenzetu kumng'oa Naibu Rais unaumbua ubovu wa katiba yetu

Ni lazima nchi ya kenya ikubali kuwa na ustahimilivu wa kisiasa. Kutofautiana kisiasa ni afya ya nchi. Siyo wewe Rais ukitofautiana kisiasa na mwenzako unataka umfukuze mwenzako kazi. 🤣🤣🤣🤣

Rais wa kenya anatakiwa kuwa mstahimilivu. Na kama alimteua Rigathi Gachagua kuwa mgombea wake mwenza na kisha akamsaidia kupata kura kutoka kwa Wakikuyu kisha akamshinda Odinga, anatakiwa kuwa mstahimilivu na wamalize mambo yao kwa mazungumzo, maana wataendeleza na kukuza uhasama wa kikabila. Tunaomba uchaguzi wao wa 2027 yasije yakatokea yale ya Mungiki
Ukiongelea ustahimilivu basi kwetu hapa ndio zero kabisa maana ndugai kusema tu nchi itapigwa mnada aling'olewa Asadi kusema tu huu ni udhaifu wa bunge aling'olewa na watu wakiongea maneno kwa ukali kidogo tu utamsikia kiongozi analalamika wananitukana
Kule kuna uvumilivu mkubwa sana wa kisiasa
 
... katiba nzuri kisiasa lakini iko sambamba na sera mbovu zinazomilikisha raslimali, kama ardhi, kwa wakubwa wachache ni KIINIMACHO TU!
... DON'T COMPARE OUR BONGO WITH SHITHOLE COUNTRIES!
So far hoja yangu kubwa ilikuwa namna wenzetu zile check and balance zimekaa vizuri yaani dp anaenda mahakamani akiamini kabisa kuwa hakuna maelekezo kutoka juu.
 
Ingekua nchi ya kusadikika, na mkuu wa hyo nchi hamtaki Naibu wake, Anafuata na gari la wazee wa baka baka, analazimishwa kuandika barua ya kujiuzulu, anapewa lockup ya nyumbani kwake yeye na familia zake ikiwa ni kunyimwa access ya mawasiliano kwa mwezi mzima mpaka watu wana msahau kua alikuepo.
Hahahaha 😂 😂 😂 nmecheka kinoma
 
Mkuu 'Mufupi', nimekusoma na nimekuelewa vizuri.

Hakika, kama usemavyo, Tanzania yetu hii sasa mtu kuonekana kuwa "mzalendo" ni kuwa chawa wa kiongozi. Hata kama huyo kiongozi akiwa mbovu kiasi gani, lakini chawa wanao ishi kwa kutumia uchafu wake, hao ndio wanaojipambanua kuwa wazalendo wa taifa hili.
 
Kwa kadri nilivyofuatilia Mchakato wa kumng'oa Naibu Rais wa Kenya nimejifunza kwamba tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili kupata katiba inayolinda maslahi ya wananchi.

Yaani hapa kwetu ukiwa wewe ni Mbunge Rais hata Diwani ukikosana na mwenyekiti wako wa chama akakufukuza uanachama basi wananchi walioridhishwa na wewe wakakupigia kura kama ulivyo kama mwakilishi wao sahihi, hawana cha kufanya ili kukupata tena wewe kama mwakilishi wao.

Kwa Kenya haipo hivyo katiba inalinda sana uamuzi wa wananchi.
Huku hatuendeshwi na katiba tunaendeshwa na maono ya Rais
 
Lazima katiba itengeneze mazingira rahisi ya kumwajibisha kiongozi wao lakini pia lazima mihimuli ya mahakama ifanye kazi yake bila kuegemea upande wowote
Katiba inayotengeneza mazingira marahisi na kuacha vacuum ya uwajibikaji na kuodoa haki ya kusikilizwa na security ya viongozi hiyo ni katiba ya kijinga.

What is the security of Deputy President? Kama anaweza kuondolewa kihuni kihuni tu hivyo? Yaani President akichoka tu anakuondoa wakati wewe ni sehemu ya kuchaguliwa kwake? Deputy President siyo waziri.
 
Ukiongelea ustahimilivu basi kwetu hapa ndio zero kabisa maana ndugai kusema tu nchi itapigwa mnada aling'olewa Asadi kusema tu huu ni udhaifu wa bunge aling'olewa na watu wakiongea maneno kwa ukali kidogo tu utamsikia kiongozi analalamika wananitukana
Kule kuna uvumilivu mkubwa sana wa kisiasa
Mzee unaazisha uzi kisha unachanganaya madesa. Ndugai alichaguliwa na wananchi? 🤣 🤣 🤣 🤣 Ndugai alichaguliwa na wabunge tu? Ndugai alikuwa anawajibika kwa Wabunge. Mzee unasafari ndefu sana ya kujifunza issue za Katiba na Republic.

Also Asadi huyo ni mteuliwa yeye siyo mwanasiasa 🤣🤣🤣🤣 Mzee mahaba yako na kenya yanakufanya uwe kichaa. Hapa tunaongelea Deputy President mtu ambaye alikuwa kwenye ballot paper moja na President. Huyo amechaguliwa na wananchi wote wa kenya. Kuwezi kumuondoa kihuni huni tu.
 
Si angalau huyo rais kahangaika kutafuta njia za kumwondoa kwa kutokwa jasho? Na bado haijulikani huyo rais mwenyewe atakuwa amepoteza kiasi gani kwa sakata hili. Utamlinganisha vipi huyo na mwingine ambaye yeye kwake "katiba ya nchi ni mkusanyiko wa makaratasi tu"!
Hapa tunaongea facts mzee hatuongelei mihemko. Tunajadiliana kisomi. Leta facts acha kuongea misemo miiiiiiiiiiiiiiiiiiiiigi

Kwanini Deputy President aliyechaguliwa pamoja na Rais kwa kupigiwa kura na wananchi wote wa Kenya anaondolewa kihuni na watu wachahce?
 
Wewe hunijui, utaanza vipi kunihoji?
Ndiyo maana watu wa aina yako nawachukulia kama takataka tu zilizojaa ndani ya nchi hii. Sijui mmeokotwa wapi nyinyi?

Kwa taarifa yako, ninaifahamu Kenya zaidi ya ushabiki wa kijinga unao uleta wewe hapa.

Sasa unataka tusemeje hapa; kwamba Tanzania inao mfumo mzuri wa uwajibikaji wa serikali yake kuishinda Kenya ilivyo kwa sasa, chini ya Katiba yao?
Acha kushabulia watu na kujifanya mjuaji wa kijinga. Kenya ni pale tu watu wanaenda kwa miguu. Tuongelee hoja iliyo po mezani. Kujivibisha kama chura ni ujinga wa hali ya juu. Hapa JF tunaongea kisomi na tunalazimika kutoa facts na sio kuoleta kiburi cha kijinga.

Tueleze kwanini Deputy president anawekwa kwenye ballot paper moja na President?
 
'Actually', nilikuwa sijaangalia hata jina lako bandia humu JF ni nani? Nilikuwa nikijibu nikidhani ni katika wale majuha wa CCM ambao kutwa nzima wamejazana humu wakiandika takataka.
"Jay One', sidhani kuwa nilisha wahi kukusoma popote humu jukwaani.

Basi ni hivi:
Wewe ni hovyo zaidi hata zaidi ya yale matakataka mengine ambayo mara nyingi huwa sijisubui kujibu maandishi yao.

Kwa hiyo chukulia kuwa nimekosea kujibu chochote ulicho kuwa umebandika hapo nilipo ku'quote'.

Kenya ninaifahamu vizuri sana, na ukitaka kujua, angalia michango yangu kuhusu nchi hiyo humu humu JF. Historia yangu haijifichi, na sijawahi kuififu nchi hiyo hadi haya yanayo tokea sasa hivi. Wamepiga hatua nzuri, pamoja na kwamba bado wanayo matatizo mengi.
Sisi tumeporomoka zaidi, na nahofia sijui tutaishia wapi na kuporomoka huku.

Sina muda tena na wewe.
Mzee tupo kwenye serious topic halafu wewe unaleta michambo. 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Acha kushabulia watu na kujifanya mjuaji wa kijinga. Kenya ni pale tu watu wanaenda kwa miguu. Tuongelee hoja iliyo po mezani. Kujivibisha kama chura ni ujinga wa hali ya juu. Hapa JF tunaongea kisomi na tunalazimika kutoa facts na sio kuoleta kiburi cha kijinga.

Tueleze kwanini Deputy president anawekwa kwenye ballot paper moja na President?
Kwani kuwekwa kwenye ballot paper Moja na rais ni immune ya kukosea!? Na ukifanya mambo usiwajibishwe!?
So far ninachosifia mimi ni kwamba pamoja na yoote hayo dp anaweza kwenda mahakamani
 
Mzee unaazisha uzi kisha unachanganaya madesa. Ndugai alichaguliwa na wananchi? 🤣 🤣 🤣 🤣 Ndugai alichaguliwa na wabunge tu? Ndugai alikuwa anawajibika kwa Wabunge. Mzee unasafari ndefu sana ya kujifunza issue za Katiba na Republic.

Also Asadi huyo ni mteuliwa yeye siyo mwanasiasa 🤣🤣🤣🤣 Mzee mahaba yako na kenya yanakufanya uwe kichaa. Hapa tunaongelea Deputy President mtu ambaye alikuwa kwenye ballot paper moja na President. Huyo amechaguliwa na wananchi wote wa kenya. Kuwezi kumuondoa kihuni huni tu.
Mi nilikuwa najibu hoja yako kwamba eti Tanzania kuna uvumilivu wa kisiasa kuliko Kenya hilo jambo sii kweli.
Katiba yetu inatoa mianya ya viongozi wa chini kutojiamini sana kwani milango ya kufukuzwa kimagumashi ni mikubwa mno
 
Kwani kuwekwa kwenye ballot paper Moja na rais ni immune ya kukosea!? Na ukifanya mambo usiwajibishwe!?
So far ninachosifia mimi ni kwamba pamoja na yoote hayo dp anaweza kwenda mahakamani
Nimekuuliza swali, Please naomba unijibu. Kwanini Deputy president anawekwa kwenye ballot paper moja na President? Please answer the question
 
Nimekuuliza swali, Please naomba unijibu. Kwanini Deputy president anawekwa kwenye ballot paper moja na President? Please answer the question
Anawekwa kama mgombea mwenza ili afanye kazi kumsaidia rais pindi wakichaguliwa
 
Mi nilikuwa najibu hoja yako kwamba eti Tanzania kuna uvumilivu wa kisiasa kuliko Kenya hilo jambo sii kweli.
Katiba yetu inatoa mianya ya viongozi wa chini kutojiamini sana kwani milango ya kufukuzwa kimagumashi ni mikubwa mno
Mzee jikite kwenye mada. Maana mfano wako huo ulioutoa hauendani na mantik hii iliyopo. Context niliyoiongelea ni tofauti kabisa.

Ruto waliingia makubaliano Gachagua ili Gachagua kuwa Mgombea mwenza ili waweze kuvuna kura nyingi na waweze kumwangusha Raila which walifanikiwa.

Kwanini Ruto anakosa ustahimilivu wa kumvumilia mwenzake na anajua kabisa wametoka vyama tofauti na wanasera tofauti?
 
Anawekwa kama mgombea mwenza ili afanye kazi kumsaidia rais pindi wakichaguliwa
Je, unajua kuwa mgombea mwenza ni part of General Election of the president? Kwanini aondolewe kihuni kihuni tu wakati ni part of president?

Yaani unamtuhumu mtu kisiasa tu, na unataka aondolewe kisheria 🤣 🤣 🤣 🤣 Ruto anatakiwa asubiri 2027.
 
The Phylosopher Ngoja nikupatie somo dogo tu kwa ufupi.

Katiba bora ni ile inayo Protect na Kuwajibisha kwa misingi ya source ya yule kiongozi.

Huwezi kumwajibisha Kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wote eti tu kwasababu mmetofautiana kisiasa. Kwa maana hiyo Rais atakuwa Mungu mtu. Ukitofautinana naye kauli tu anakuondoa wakati hajakuweka yeye hapo madarakani.
 
Mzee jikite kwenye mada. Maana mfano wako huo ulioutoa hauendani na mantik hii iliyopo. Context niliyoiongelea ni tofauti kabisa.

Ruto waliingia makubaliano Gachagua ili Gachagua kuwa Mgombea mwenza ili waweze kuvuna kura nyingi na waweze kumwangusha Raila which walifanikiwa.

Kwanini Ruto anakosa ustahimilivu wa kumvumilia mwenzake na anajua kabisa wametoka vyama tofauti na wanasera tofauti?
Hivi kwa mfano nilikuteua unisaidie kufanikisha jambo fulani, kweli tukafanikiwa lakini nikagundua humo njiani kwamba kuna namna hauniungi mkono unatakanikuchukulie hatua gani!?
 
The Phylosopher Ngoja nikupatie somo dogo tu kwa ufupi.

Katiba bora ni ile inayo Protect na Kuwajibisha kwa misingi ya source ya yule kiongozi.

Huwezi kumwajibisha Kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wote eti tu kwasababu mmetofautiana kisiasa. Kwa maana hiyo Rais atakuwa Mungu mtu. Ukitofautinana naye kauli tu anakuondoa wakati hajakuweka yeye hapo madarakani.
Ile pale sii kutofautiana kisiasa ila ni kuenda kinyume na maadili ya uongozi.
 
Back
Top Bottom