Kutoka kuwa Mkurugenzi wa TISS na kuwa IGP hii imekaaje?

Huwa navyoona wakikaa kiprotokali;

1. Mkuu wa majeshi. CDF

2. IGP.

3. Usalama wa Taifa.

4. Kamishna Uhamiaji.

5. Kamishna Magereza.

6. Kamishna Fire.

7. Kamishna madawa wa kulevya.
 
Mimi nakuunga mkono wewe, hata mishahara wanayopata ni ya mambo ya ndani ya nchi japo kuna ka upendeleo fulani hivi wanapata kutoka ikulu ila hawana tofauti na Polisi .
Sent using Jamii Forums mobile app
 
hata Polisi pia wanafanya kazi mpaka nje ya nchi ya Tanzania, ndio maana kuna Polisi wa kimataifa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mnamfananisha Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na watu ambao anawachunguza yy na kuwatolea mapendekezo kama wanafaa kuwa nafasi walizo nazo!

Usalama wa Taifa c watu wa kawaida na hawafananishwii
 
hata Polisi pia wanafanya kazi mpaka nje ya nchi ya Tanzania, ndio maana kuna Polisi wa kimataifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe tatizo ni kubwa kuliko nilivyokua nafikiria, kwa hiyo polisi wa kimataifa Interpol iko chini ya wizara ya mambo ya ndani ya Tz
 
Mimi nakuunga mkono wewe, hata mishahara wanayopata ni ya mambo ya ndani ya nchi japo kuna ka upendeleo fulani hivi wanapata kutoka ikulu ila hawana tofauti na Polisi .
Kabla ya mwaka 1996 TISS (UWT) kuanzishwa ilikuwa chini ya Wizara ya Mambo ya ndani na mpaka leo wengi wa maafisa waliokuwa huko ni POLISI mishahara na masurufu yako huko,
kuna mdau kaelezea vizuri lkn uelewa wa member
Pale Ikulu kwenye ulinzi wa Rais kuna aina tatu za Walinzi, wengi wanawaita TISS lkn kuna JWTZ makomandoo, inner circle wakifuatiwa na TISS na POLISI na hata mavazi silaha na escort vinajionesha kabisa,
cc Evarist Chahali
 
Mgambo wana mafunzo ya kivita,wako chini ya JWTZ.Ndio maana kila mkoa kuna mshauri wa mgambo ambaye ni afisa wa jeshi
Sawa lakini Ni kweli kuwa wakati wa amani wanakua chini ya Mambo ya ndani wakati wa Vita wanakua chini ya W Ulinzi.
 
Sawa lakini Ni kweli kuwa wakati wa amani wanakua chini ya Mambo ya ndani wakati wa Vita wanakua chini ya W Ulinzi.
Ni kweli wakati wa Vita ni wote wanakuwa Wanajeshi hata kama wapo Mambo ya ndani, ndio maana Darfur POLISI walikwenda wengi, zipo kazi huko
 
Kitu kizuri humu ndani kila mtu mjuaji, kuna wanaojua wamekaa kimya na kuna wasiojua wanaonesha kujua. Sitaki kubishana ila nataka kuwasaidia kidogo. TISS ndicho chombo kikuu cha kukusanya taarifa,kuzichambua na kushauri. Taarifa zote kutoka kila sehemu iwe ni jeshini, bungeni, nje ya nchi, sokoni nk. Narudia tena taarifa zote wanatakiwa kuwa aware nazo baadaye wanazifanyia screening na kuchukua za maana tu.

Kwa mantiki hiyo TISS wanashauri uteuzi wa nafasi nyeti ndani ya serikali, from no where mtu hawezi kupewa cheo cha CDF aongoze jeshi bila kufanyiwa vetting. No lazima wajiridhishe then wampitishe. Vivyo hivyo kwa IGP nk

TISS wapo kila mahali, iwe kanisani (kapilimba alikua mchungaji) msikitini, ikulu, shuleni nk. Kila penye watu wapo!

TISS imegawanyika sehemu kuu mbili. Kurugenzi ya mambo ya nje na ndani. Huko nje tuna mawakala kibao kamwe hatutowajua kwa macho!

TISS members wanapatikana kwa ujuzi wa hali ya juu sana, vetting huchukua hadi mwaka mzima. Nilipokua chuo yalinikuta haya... Kama isingekua.... Leo hii ningekua huko.
TISS ndo wanaratibu hata aina ya siasa na uongozi wa nchi, ndio wanaochezesha hata michezo michafu kama ile ya kina Zit...
TISS wanacheza sana na saikolojia za watu, propaganda kwao ni somo kule chuoni, kuna watu maalumu wapo kwenye vyombo vya habari, mitandaoni nk wakileta habari wanazotaka tusikie kwa malengo yao... Amini nakuambia!

TISS ni dubwana kubwa! Usidanganywe na neno 'idara' kisheria hawaruhusiwi kuendesha any operation lakini.... Pia wao kwa wao hawajuani maana kule unafanya kazi kwa amri na maelekezo kama utapewa kazi ya udukuzi utaifanya tu hata kama kwa mke wa rais

Sitaki nilinganishe vyeo vyao... Nataka ujue majukumu ya kazi zao.. Wengi hatumjui rais ajaye Ila miongoni mwao wanajua mda mrefu. Pia depo yao ile ya Siri pale ba... Sio mchezo! Pale ndo wanatoka PSU kwa ajili ya ulinzi wa viongozi, snipers wa kazi maalumu na wale wasiojul...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gavana alimteua mwanasheria kwa sababu amesoma Economic Law na ni Profesa. By the way, Gavana aliyepita alikuwa mchumi kweli?
 
Hivi watu wanabishana hivi kwa nini? Katiba imeenda wapi? Huu mjadala kwa upande mwingine unaonyesha kuwa watu tulitamani sana kuwa sehemu ya taasisi hizi ila kwa bahati mbaya hatukubahatika. Mimi mwenyewe hapa nilipo, nilitamani sana kuwa JW au Polisi lakini sikubahatika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…