Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Duh.... mbwa kala mbwaa
 
Sehemu ya 9

Nikaona Arusha hali ishakuwa mbaya uzulumati ndio jadi na ili uweze kusurvive basi yakupasa uwe mbabe haswa!

Nikarudi Rombo kupumzisha akili ila sikukaa sana nikaenda kwa bibi Marangu ambako ndio nilikaa mwezi mzima huku nikitafakari hatua inayofuata mbele.

Nikaondoka na kwenda kuanza maisha mapya huko Tabora, ambapo nilipanga chumba maeneo ya Isevya.

Kule nilianza kujishughulisha na nguo za mtumba, ambapo nilikuwa naagiza mzigo Dar ukifika mimi nasambaza madukani. Huko nilibahatika kupata mwanamke tukawa tunaishi naye pika pakua.

Niliifanya biashara hiyo ila haikudumu maana ilikuwa ni ya mikopo sana. Hivyo nilifilisika rasmi na back to square one. Nyumbani kule dogo anasumbua maana ndio yuko form 4 na hapa pia mwanamke kazi hataki anajua kupokea tu na umri wangu ulikuwa bado. Kichwa kilikuwa kinawaka moto kurudi nyumbani naona jau. Nikaamua kuingia kwenye biashara ya ganagana( daladala baiskeli).

Nikafainya kwa muda wa kama wiki moja, nilipata ruti ya kutoka mjini kwenda Cheyo kama nne hivi. Sasa huwa kuna kamlima fulani kupandisha, miguu iliuma nikalala ndani siku 2 na kazi hiyo nikasema hainifai.

Nikaingia kupiga vibarua vya kushusha cement na saidia fundi na penyewe pakuwa pagumu sana kwangu.

Siku moja nilienda Mwinyi Mchichani kwenye bar x kufurahi huko nikakutana na Mpoladuhu ambaye tulianza kupeana michongo ya hapa na pale.

Nyakati hizo zilikuwa ni za majira ya asali huko Sikonge na Kaliua. Mpoladuhu akaniambia twende Kaliua, ambako huko tulipanda gari na kuelekea kilomita 90 Ugala huko mpakani mwa Tabora na Katavi.

Shughuli iliyotupeleka huko ni urinaji wa asali kinyemela huko Ugala na kurudi mpaka hifadhi ya Lumbe. Yeye alikuwa ni mtaalam wa urinaji na tulifanikiwa kupata madumu 5. Lakini hayakuzaa matunda kwani tulikamatwa na game na kunyang'anywa yote na kichapo juu!

Tukarudi mjini na tukaamua kuunda genge letu tukamuongeza Kinehe na Madelagawisa ambao tutashirikiana katika maisha. Hivyo kila mmoja hapo ameshawahi kuwa katika matukio kadha wa kadha.

Tuliondoka na kwenda katika milima ya Izimbili ambako huko tulijifua kwa dawa na kula viapo mfano ukidakwa basi kufa mwenyewe, kugawana pasu kwa pasu, kutokuzungukana n.k. Kule mbuzi mnyama alichinjwa na madawa mengine na tulipigwa kila mtu chale mwilini za kinga. Kwasababu wasukumu ukiwaibia mara nyingi wanakimbiliaga kuloga hivyo tuliona tujizaetiti mapema.

Katika kutest mitambo na kujiweka sawia na kazi tukaamua twende tukawatembelee huko Cheyo kwanza.
Tulienda mitaa ya Cheyo A, ila tulighairi na kwenda Uzunguni ambako tulipata taarifa za mstaafu mmoja. Hapo hatukuwa na silaha ni mapanga tu hivyo usiku tulimvamia na kuvunja mlango maana hakukuwa na uzio katika hiyo nyumba. Tulizama ndani na bila kupoteza wakati tulianza kuwapa kichapo, lakini wapi mstaafu mwanaume hataji hela zilipo na mwanamke pia hataji wote wamekaza.

Piga na mabapa ya mapanga mpaka mstaafu akazimia ila mwanamke aligoma katakata kutaja hela zilipo. Walikuwa wawili tu nyumbani mume na mke. Hivyo tukaanza kupekuwa huku na huko pesa hazionekani tukirudi kwa mwanamke anasema hajui zilipo.

Muda unazidi kwenda na hapo uzalendo umeanza kutushinda. Mpoladuhu kwa hasira alinyanyua meza kumpiga nayo yule mke wa mstaafu, na ndipo kila mtu akastaajabu. Meza ya mbao kwa chini imegongewa mbao nyingine na kwa ndani ndipo hela zinapokaa.

Bila kupoteza muda tuliivunja na kutoa maburungutu ya hela na kutia kwenye mfuko wa rambo na kutokomea zetu tukimwacha akiangua kilio kikali sana.

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Niliifanya biashara hiyo ila haikudumu maana ilikuwa ni ya mikopo sana. Hivyo nilifilisika rasmi na back to square one.
Chukua somo hapa ukikopesha mfanyabiashara utafilisika. Nilikuwa na baangu mmoja anadai kuwa Bora kioze atupe kuliko kukopesha.
Namie huwa naongezea Bora upigike ukiwa hudaiwi ama kudai maumivu yake inabidi uyapitie Mana uliambiwa hutoelewa
 
Sehemu ya 10

Tulienda mpaka Ipuli ambako ni nyumbani kwa shemeji yake na Madelagawisa ambaye ndio alituuzia mchongo. Tukazihesabu hela na zilikuwa milioni 40 kasoro.

Mpoladuhu akasema maisha yanaitaji roho ngumu sana, kama tungekata tamaa tungezipata wapi hizi hela?
Tuligawana pale watu wanne na yule muuza ramani wa 5, ila yeye hakupata sawa na sisi.

Kesho yake nilirudi home nikiwa nimejaa tele nikaamua kupanga chumba kingine siku hiyo hiyo maeneo ya Kanyenye jirani na Mwika. Na kile pia nilibaki nacho hivyo nilikuwa navyo viwili.

Nyakati hizi nikasema hakuna kufeli tena, nilimdanganya mwanamke nimetoka machimbo hivyo nikampa hela ya biashara namimi narudi machimbo.

Nilikaa wiki nikarudi Rombo nyumbani kwenda kuweka mambo sawa. Baada ya hapo nikapitia Arusha kuwasilimu kina Mroso na Palangyo, ambako nilipata taarifa ya kuwa wote waliuawa kule stendi ya Mboya Moshi. Ilinishtua sana na mdogo wake na Palangyo akazidi kuniambia Arusha sasa hivi hapafai kabisa polisi wamechachamaa sana.

Na mimi nikaamua nijirudie zangu Tabora. Ile kufika tu Mpoladuhu ananiambia hatulali tunaunganisha Usinge kuna ramani. Nilikuwa najihisi mchovu lakini hamna namna. Safari ya Usinge ilianza, tulifika Kaliua na kulala pale tukiwa na gari Hilux double cabin nyeusi.

Kesho yake asubuhi tukaondoka na kuelekea Usinge, ambako tulikutana na wadau wawili ambao walikuwa wanatupa mchongo wa hela. Kwa muhtasari mchongo ulikuwa kwenda kumwibia Mwarabu mmoja hapo Mwanga ana mabiashara na mabasi hivyo tulitakiwa kuwa timu ya kutosha maana hautakuwa mchongo rahisi hata kidogo.

Tuliondoka Usinge na kwenda mpaka Nguruka ambako huko tuliungana na genge lingine na kuwa jumla yetu 8. Hapo hapo usinge tulilala siku mbili kwaajili ya kujiboost kwa wazee.

Hatukuwa na silaha yoyote ila tayari location ya kwenda kupata silaha ilikuwepo. Gari mbili ziliongozana hilux na hiyo nyingine rav4 nyeusi. Tuliingia Kigoma na kwenda kuweka kambi yetu maeneo ya Mwanga Kilimahewa.

Mpango ulifanyika wa kupata silaha maeneo ya Kitongoni, ambapo zilipatikana bunduki 8 yaani kila mtu ya kwake, kati ya hizo kuna pistol na hizi smg pamoja na risasi zake. Wale ambao walitukodisha walikuwa sharti lao nao wawe sehemu ya tukio maana wao pia wanataka hela. Hivyo tukawaunga jumla yetu 10 mwarabu kazi anayo.

Tuliondoka na kwenda location kwaajili ya kuhifadhi zana za kazi na kisha kuondoka na kwenda kuoga tena dawa kwa wataalam kwaajili ya kujilinda.

Siku ya tukio ilifika na kulikuwa na mvua na radi za mngurumo balaa, tukajongea site kuendelea kuangalia hali ikoje tukaona ni mizigo inaingia na kutoka maana walikuwa na sheli pia.

Ilipofika mida ya kukaribia kufunga gari moja iliangalia uelekeo wa Magharibi na nyingine Mashariki pale tulishuka maana tulikuwa tushajipanga 5 waliingia site na sisi 5 tulibaki nje, hapo ni milio ya risasi na kwakweli wale tuliokuwa nao walikuwa majambazi haswa hakuna maswali mengi unakula chuma ni hela zitolewe waarabu nao hawakuwa nyuma kuna wawili walianza kurudisha mapigo na hapo mji ukachangamka sasa wawili waliongezeka ndani kutoa msaada na hela zilianzwa kukusanywa vizuri, polisi nao tayari walikuwa alert na hilo tukio kutokana na milio heavy hawakusogea eneo la tukio tulivyoanza kuondoka kila gari ilishika uelekeo wake mimi nilikuwa kwenye rav4 tulienda kuwakuta Mapai lake Tanganyika tukarushiana risasi kidogo, dereva akaenda mitaa ya Buzeba ili polisi wasirushe risasi. Ila mpaka hapo roho mkononi, tukaendelea kufukuzana huku nao wakitufukuza kuelekea road block zao.

Shughuli yetu ilienda kukwamia Bangwe na ndipo tulianza mashambulizi tena. Katika rusha nikurushie tunazidi kupunguwa huku polisi wakisisitiza tujisalimishe.

Tukaambizana sasa kila akimbie ashike njia yake kujinusuru. Mimi nikakimbilia kule makaburini na ndio ikawa pona yangu giza lishaingia wale niliokuwa nao wote waliuwawa onspot pale na mapolisi wote 4.

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Sa kama.alikuwa mwanafamilia kwa nini Alalame kufanya hizo kazi ..alitaka alelewe kama yai asifanye kazi yyte
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…