Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Saladi tena ukieka na nazi hatari kabisa, sema inabidi uziandae mapema la sivyo utakula saladi nyama (vikonokono vidogo na vyura) bibi angu alikua mkiandaa saa kumi na mbili jioni hali anahofia asile saladi nyama😂😂😂😂😂
Hiyo mboga ni tamu sana, usipoosha vizuri lazima ukutane na vijikonokono vyeusiiii
 
sema nin, nadhani hapo cha kuhuzunisha ni kupoteza wazazi wako, mali zenu kuuzwa na huyo dingi mkubwa, ndugu kutupiana mpira kwenye kukulea na manyanyaso ya chakula. Lakn kukata majani ya ng'ombe, kuwalisha, kusafisha banda na kuokota kuni sio mateso bali ni wajibu.
Wajibu upi unaambiwa unakata majani na viboko juu
 
Sehemu ya 6

Tulisubiri ishara bila mafanikio ikabidi turudi location yetu tukiwa tumefura hasira ile mbaya. Asubuhi palikucha na Mankah ndo alikuja wa kwanza na kuanza kulalama sana juu ya Warombo kuwa mama huruma na kwamba Adela amesema hatoshiriki na sisi kwenye huo mpango kwa kuwa ameahidiwa kuolewa na Ima pamoja na kujengewa nyumba, hivo tuliambilia hela ya nauli ya kuondokea Mererani. Wote tulitawanyika na kila mtu alishika 50 zake mchongo ulifeli.

Siku ya Jumamosi nikiwa mitaa ya Ngusero napuyanga huku na huko Palangyo alinifata na kuniambia twende Iliboru karibia na shule ya Iliboru ilipo kuna ramani tuliondoka na gari aina ya pegeout504 mpaka Iliboru. Kule tulimkuta Mroso na mimi na Palangyo na Fidee ambaye ndio alikuwa anaendesha hiyo pegeout.

Mchongo tuliusuka vizuri baada ya kupata taarifa kuna Wakenya wamekuja kununua maparachichi Tanzania, na wapo mizani pale back town Ngarenaro.

Tuliondoka na kwenda mpaka mitaa ya kona ya Eso ambapo tulipaki na kwenda kuzengea zengea ili kujua kunaingilika? Na dere naye alienda kuweka full tanka pamoja na mengine kwenye dumu kama dharura. Kweli fuso ile aina ya tandam ilikuwa imeshiba na walikuwa ni Wakenya ambao walikuwa wanasubiri jua lizame waanze safari ya kurudi kwao Kenya kupitia Namanga.

Sisi tuliamua kutangulia na gari ilikuwa ikipepea haswa mpaka tulipofikaOldonyosambu tukapaki pale huku tunachanja gomba na kushtua bangi ili akili zikae sawa tulipoteza kama nusu saa kisha tukaendelea mbele mpaka Longido, pale tulikuta road block tukasimamishwa kwaajili ya ukaguzi kwa kuwa tulikuwa tuna gomba na bangi tukaona tusipotezeane muda tukampooza askari kiasi cha pesa akatabasamu na kututakia kila la kheri.

Tulienda mpaka mbele kuna kamsitu pale tulisimama na kupaki gari barabarani kana kwamba limeharibika tulikaa kama masaa mawili kisha tukaliona gari la wakenya tandam likija lilikuwa kwa juu pale limeandikwa Michelin Naivasha. Gari iliwashwa na kusogezwa katikati ya barabara halafu likazimwa kama limeharibika tena huku tukijaribu kulisukuma.

Dereva alianza kupunguza mwendo mdogo mdogo upande huu mwingine gari za kutoka Namanga zilikuwa zinakuja tukaona hapa ndio penyewe tukalirudisha saiti yetu kuyapisha magari yanayotoka Namanga kwenda Arusha yapite. Palangyo alienda kwa Wakenya yule dereva kuomba msaada yule dereva aligoma ndipo Mroso akaona muda unazidi kupotea akazumguka upande wa abiria siti nyingine hizi akachomoa bunduki ambayo tuliikodi hapo hapo Arusha. Akapiga moja juu na Palangyo naye alichomoa ya kwake kumtisha dereva maana alikuwa ameshaanza kuingiza gia.

Dereva naye wa Pegeout hakuwa mzembe aliirudisha reverse gari mpaka ikaigonga ile tandam kwa mbele kidogo.

Tuliwashusha wote chini na hakukuwa na kupoteza muda kwani tuliwapiga na kuwataka watoe pesa, pesa ilikuwa kwenye mkoba nyuma ya siti maeneo ya cabin. Tuliibeba na kupiga risasi moja juu tena kisha tukatimua vumbi kurudi Longido, kufika Longido tulishika njia moja ya vumbi ya kuelekea Kiserian ili kukwepa polisi ambao wangetufata.

Gari ilikuwa inatembea haswa tulikuja kutoboa Lariboro na kuelekea mpaka Olmotoni kisha kuelekea Mateves ambapo tulipaki mitaa hiyo na kusikilizia kwanza. Tuliamua kutafta nyumba ya kulala wageni maalum kwaajili ya kuhesabu pesa hizo ambazo zilikuwa milioni 27 na chenchi zake. Mgawanyo ulikuwa 6*6*6*9.

Palangyo ndio alikuwa na mchongo hivo alikuwa anakula cha juu zaidi. Hakukuwa na ubishi sana katika mgawanyo kwani mapatano ya mwanzo ni kuwa mwenye ramani ndio mshika hela na ndiyo atagawa kutokana na ugumu wa kazi.

Je nini kitafata usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Leta vitu baba,natamani kujua kwa Sasa maisha yako na ya wadogo zako kule rombo yanaendeleaje
 
Sehemu ya 3

Baada ya kufika Tarakea kwa shangazi aliniunganisha na mmeru mmoja baba wa makamu wa huko Kenya eneo moja linaitwa Oloitoktok kwa watu wa Rombo na maeneo ya jirani wanapafahamu hapo elimu ndio ilikuwa ishanipiga sandakalawe. Huyo mmeru alikuwa na mke na watoto wawili mke wake ni jamii ya Wakamba maeneo ya Taveta.

Nilianza kuuza duka la mahitaji ya nyumbani biashara kwa kweli ilikuwa nzuri ila kila huyo mwanamke wa Kikamba akija alikuwa na mtindo wa kuchukua pesa na kusema atarudisha ila harudishi, akija mumuwe anakana katakata hajachukua hivyo nakatwa mshahara wangu.

Sa nyingine ananipa nguo nivae yeye alikuwa anauza mitumba ikifika mwisho wa mwezi nakatwa kwenye mshahara wangu hata ukigoma kununua anasema nimekupa bure upendeze mwanangu ila tarehe ya salary ikifika nalimwa panga. Hicho kitu kilikuwa kinaniuma sana. Ikanibidi nimwambie mumewe ambaye ndio bosi wangu, kwa kweli maisha hapo Loitoktok niliyaona machungu sana maana nakumbuka msosi alikuwa hanipi mpaka mumewe arudi jioni ndio nakula, bado nilikuwa nasingiziwa kuwa nasumbua watoto wake nyakati za mchana, ile vita na mwanamke wa Kikamba ilinishinda ikabidi nikubali yaishe nikaomba kuondoka sikupewa hata mia kwani niliambiwa sidai kitu na bado nimesababisha hasara nyingi sana.

Ikanibidi niondoke hapo nakuelekea maeneo ya Taveta ambapo nilikutana na wafanyabiashara wengi sana watanzania ambao walikuwa wakileta maparachichi na ndizi kuja huu upande wa Kenya. Niliwaomba msaada maana hapo sasa nilikuwa nimeshaishiwa nikapandishwa kwenye Beckford ile kama kumbukumbu ziko sawa kwa nyuma kule, gari lilisafiri breki yake moshi mjini nikaambiwa tumefika.

Kwa hapo Moshi nilikuwa mgeni maana ni mjini hivo sio mzoefu. Nilizungaka huku na huku nikadakwa kwa kosa la uzururaji na kuambiwa mimi ni chokoraa, haswa kwa wakati huo machokoraa waliaminika kutenda uhalifu sana kwa Moshi.

Nilikaa ndani, na kila polisi wakinihoji ndugu wakwapi mimi nasema sina. Nilikaa kwa siku 3 nikaachiwa baada ya afande mmoja kusema angenichukua niende Mererani kwenye biashara yake kuuza maji maeneo ya Kazamoyo.

Niliuza maji kwa kutumia punda na hapo kwa kweli nilikuwa na hasira sana na maisha na niliona msaada sina tena maana ndugu wamenitenga na hata wadogo zangu sikuwajulia hali zao. Ile biashara kwa pale Mererani ilikuwa na hela maana nilikuwa nakaa kwa huyo afande na mke wake pia alikuwa askari ila wa magereza.

Nikaja kupata dili la kupeleka maji migodini huko, ila shida ikawa kwenye malipo ya hela mpaka shimo liteme ndio ulipwe na sa nyingine urushwe na bosi haelewi ni mtata sana, kuna muda anakushushia kipigo kizito sana ukichelewesha hela na huna pakwenda kushtaki anakuambia wazi wazi.

Nikaachana na hiyo kazi nikaingia kwenye uana polo na kwa nyakati hizo migodi ya Tanzanite ilikuwa inatema sana madini haswa mgodi wa Ray** na Lemak**. Ila kiujumla nilishindwa na haswa kutokana na kula msoto sana na magonjwa ya tumbo haswa typhoid ni kitu cha kawaida.

Na kwa nyakati hizo tofauti na sasa ilikuwa hulipwi hela ila mawe yakipatikana tajiri anachukua chake ndio na nyie mpate mgao ila inategemea na makubaliano.

Wengi sana tulienda na tulishindwa na wapo waliofanikiwa tukiwaona. Hivo nilipata kampani ya watu wa Ngarenaro nikaungana nao kwenda Arusha kujaribu bahati tena huko!

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Moshi kulikuwa na vibaka wakiitwa kokomoti enzi za 90s
 
Back
Top Bottom