Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Good afternoon brothers and sisters đź‘‹

Based on a true story!
Mimi nafanya kuiwasilisha kwenu, hivo fuatana nami mpaka mwisho.

Mimi naitwa Alphonse ni kijana niliezaliwa miaka 36 iliyopita yaani 1986 huko mkoani Kilimanjaro katika hospital ya KCMC. Kwetu tupo watatu mimi na dada zangu wawili, wa kwanza Anna alizaliwa 1988 na mwingine Agness alizaliwa 1992. Baba ni mchaga wa rombo useri na mama ni mchaga wa marangu kirua. Baba alikuwa mfanyabiashara mkubwa hapa jijini Arusha wa vitambaa maeneo ya kilombero na mama yeye alikuwa mtumishi yaani mwalimu katika shule ya Arusha Secondary School kifupi Arusha sec. Tulikuwa tukiishi sakina maeneo ya silentini ndipo wazazi walipojenga.

Maisha yetu kwa kweli yalikuwa mazuri sana hapakuwahi kuwa na shida nyumbani upendo ulitawala na ndugu walitupenda sana na kila tukifunga shule basi bibi wa huko kijijini wa pande zote kila mmoja alikuwa anang'ang'ania tukakae kwake. Shule tulisoma nzuri mimi nakumbuka nilisoma st. Constantine iliyopo Arusha, shuleni tulienda kwa school bus na kurudi kwa school bus. Hata shuleni kulikuwa na tour za kwenda mbuga za wanyama mbali mbali na vivutio vingine nchini.

Kwa kweli shida sikuwahi kuzijua maana nyumbani tulikuwa hatuli maharage na dagaa maana mama alikuwa na vidonda vya tumbo. Nakumbuka hata nguo nlikuwa nafuliwa na dada wa kazi ambaye alikuwa mwenyeji wa Singida. Asubuhi ilikuwa lazima tule cornflex na maziwa. Nilikuwa mtoto wa geti kali hata kucheza ni ndani kwa ndani tu.
Mwaka 1995 nakumbuka nikiwa shule alikuja mjomba shule hivyo niliitwa ofisini kwa mwalimu mkuu nakuambiwa nirudi nyumbani. Tuliondoka na mjomba kwenye gari aina pegeout mpaka nyumbani ambapo kulikuwa na watu wengi tayari, sikujua nini kinaendelea kwa hiyo mimi na wadogo zangu tulikuwa na mjomba muda wote, ndipo baadae alipokuja baba mkubwa na kutuambia baba na mama hawapo tena! Mdogo wangu aliuliza wamesafiri watarudi lini? Alijibiwa hawatarudi tena na sasa ninyi ni jukumu letu.

Mimi sikuielewa na hakuna ambaye pia alielewa tukazidi kuhoji na tuliambiwa tu wameenda mbinguni kwa Mungu. Bado kwetu kuamini na kuelewa ilikuwa ngumu lakini tulienda kuzika Rombo na huko tulilia sana ila mdogo wetu wa mwisho Agness yeye wala hakulia ni kama alikuwa haelewi kinachoendelea. Mazishi yalikamilika hakuna aliyekuwa na nawasi wasi sana ila ndio hivo tulishabaki yatima bila kujijua.

Kilichobaki hapo ni mgawanyo wa mali na kwa mila zetu mimi ndio nilimikishwa mali zote za Mzee ikiwemo mashamba huko Rombo na nyumba hapo sakina. Na huko Rombo pia mzee alijenga nyumba yake. Kule kwa mama kirua pia napo mzee alimjengea mama mkwe wake nyumba.

Basi baba mkubwa ambaye alikuwa akiishi dar kwa wakati huo alisema angetuchukua tukaishi kwake huko dar na kwamba angetusomesha mpaka tutakapokuwa. Ile nyumba baba mkubwa alisema isiuzwe bali waishi ndugu zetu nayeye pia akiwa anakuja arusha aweze kufikia huko.

Sikuwahi kujua kuhusu hati ya nyumba, mafao yoyote ya mama maana alikuwa mtumishi na wala kujua kama mzee alikuwa na hela benki au akiba yoyote. Mzee alikuwa na magari 3 pegeout ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kupeleka abiria namanga, defender 110 ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kubeba abiria kutoka mererani kaza moyo kupitia mbuguni mpaka arusha mjini na staut nyeupe ambayo ndio alikuwa akiiendesha yeye katika shughuli zake ilikuwa ikimsaidia sana. Ila baba na mama walipata ajali ndani ya hiyo staut maeneo ya mto nduruma na umauti kuwafika hapo hapo!

Pegeout alibaki nayo mjomba akiendelea na ruti za namanga na ile defender 110 baba mkubwa aliipeleka kijijini ikafanye kazi ya kubeba maziwa na kuleta moshi mjini. Statut ilibaki imekaa juu maye na ilichinjwa ikauzwa.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatilia mkasa huu wa maisha ya kweli unaosisimua na kutoa machozi.
Ikikupendeza hiI adisi uwe unanitumia 1kwa1
 
Chugga nilipapenda sana yaani tengeru sokoni t-shirt ni bukubuku ila ukiipandisha town huko sanawari bila 15000 huitoi dukani,Kiatu cha 5000 Tengeru ukifika Clock on bila 70000 hupati kiatu.....wazee wa fursa wanazitumia haswa
Mara ya kwanza naingia arusha 2011,nilishangaa kuona kiatu cha 70,000 na nguo za mtumba mashati ya 15,000 niliondoka nikawa nawaza hvyo viatu wanavivaa wakina na nani

Mashati na kadeti kali nilinunua hzo nilizipenda,tena kuna kadeti kali zaidi ya zile za spesho
 
Jamaa keshatuachia manyoya mboga kakimbia nayo. Mpaka mda huu hola hakuna mwendelezo wala nini, oya mwamba lete nondo basi mbona kimya mdau ujue hili story lako limekata kikamanda sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kumbe na wewe unaumia? Unakumbuka ulivyozira hapa na kuwaacha watu na alosto?
 
Good morning brothers and sisters đź‘‹
Sehemu ya 8

Tulienda Njiro na kuangaza maeneo hayo, tukashuka mpaka contena na kwenda kutia nanga makaburini kule Njiro.

Huko tulishtua kwanza bangi maana vichwa tulihisi vimechoka sana na kujiboost kidogo na ugoro maana kipindi hicho kuberi ilikuwa imeanza kupigwa vita sana kuwa inaleta kansa n.k. Tulivuta mpaka usingizi ukatuijia tukalala pale pale makaburini. Kuja kushtuka mida ishaenda sana.

Tukaondoka na kwenda Philips hapo tulikutana mr x ambaye alitupa zana za kazi na gari moja kwa ajili ya tukio. Na dereva pia alitupatia wa kwake ili tusije tukamgeuka.

Hapo hatukuonana na mdosi zaidi ya mpambe wake Mr x. Alfajiri mapema kabla hata adhana haijalia tuliamua kwenda eneo la tukio, kulikuwa na geti la kuingilia pale PPF ukiachana na ile njia ya kwenda cocacola. Tulifika nyumbani kwa muhindi jumba la kifahari la ghorofa moja limepigwa vigae vyekundu juu na sio bati.

Nyumba ilikuwa na electric wires zile kuzunguka uzio wa nyumba, na mbwa watatu hawa German shepherd yameshiba kweli. Pia kulikuwa na kijana wa kazi anayelala servant kotaz.

Mimi Mroso aliinama Palangyo akapanda kwa juu ili ashike ukuta adandie( zile nyaya zikishikwa na kitu huwa zinapiga alarm zinalia) hivyo Palangyo alijitahidi asiziguse na wote mkononi tulikuwa tumevaa gloves 🧤 hivo hatukuogopa shoti.

Nyakati hizo ili uwende kuwaibia wadosi majumbani kwao haswa maeneo ya Njiro au Uzunguni kule lazima uwe na zile silencer ambazo zilikuwa zinakodishwa na Mmanga mmoja huko Horohoro. Na pia lazima uwe na nyingine ambayo sio silencer kwaajili ya kuleta heshima kwanza na kutisha watu.

Mbwa zilikuwa zinaunguruma huku udenda unawatoka na wanajua kunusa balaa, Palangyo hakupoteza muda alianza kufyetua mmoja baada ya mwingine, mimi nikainama Mroso akanikanyaga apande ukuta na mimi nikachumpa kurukia ukuta maana nilikuwa mwepesi na nimezoea. Wote tulikuwa ndani hivyo tukaanza na servant kotaz jamaa amelala hana habari, dirisha lake liko wazi tukachukua cd moja ambayo ilikuwa imelowekwa kwenye tindikali X alafu inaachwa ikauke. Ile mnaichoma pale kama udi mnamuacha alale unono.

Tukaanza kuzunguka madirishani kuchungulia na tukapata upenyo dirisha la jikoni halikufungwa, tukakata nondo moja kwanza mimi nikaingia halafu ikakatwa ya pili akaingia Mroso na Palangyo. Palangyo na Mroso wakaenda juu mimi nikabaki chini maana ndipo kulikuwa na chumba cha house girl. Nikajaribu kufungua, kilikuwa kimefungwa kwa ndani nikamgongea na kukohoa, yeye asijue hili wala lile akafungua hata hajamaliza kufungua vizuri mimi nilipita na teke moja mpaka ndani na ule usingizi na wenge alienda chini mimi nikamrukia nakumuoneshea upanga na akae kimyaa.

Mroso aliniita kwa jina la kazi nije juu hivyo nikamnyanyua yule dada na kupanda naye juu kule nikakuta wote washawekwa chini ya ulinzi.

Muhindi alikuwa na mke wake na mtoto mmoja wa kike na ndugu zake wawili watu wazima. Huwa kwenye maisha yao hawana mzaha, kabisa Mroso aliniambia mkate mkono huyo mzee wanatusumbua kutupa hela yule muhindi akasema hapana, nawapa hela na chumbani kwake na mke wake walikuwa na sanduku limejaa hela nyingi sana ni sefu kwaajili ya kuhifadhia pesa, Mroso alimwambia fungua na bila hiyana muhindi alifungua, nikaambiwa beba twende tuongozane na muhindi na mke wake mpaka nje ya geti.

Hivyo walitufungulia na ndani alibaki Mroso na Palangyo na kule nje mimi na dereva ambao tuliwaamuru walale chini. Kule ndani waliwafunga kamba na kuwafungia wote chooni na kutoka nje yule muhindi na mke wake tukawapakia kwenye gari na kwenda kuwatelekeza kule dampo napo huko huko Njiro.

Hivyo sisi tuliondoka na tulienda Kijenge Mwanama hapo tulichukua gari nyingine aina ya mazda na dereva mwingine tukaenda mpaka Sekei, na penyewe tulibadilisha gari na kuingia kwenye carina nyeusi kisha tukaondoka na kuelekea Kimandolu ambapo tulimkuta mdosi na watu wake.

Hela zilihesabiwa na sisi tulikabidhi zana za kazi huku mdosi akitukazia sana macho. Baada ya hapo jamaa akaja kumng'ata sikio mdosi. Mdosi akasema mbona hela ni chache sana hizi hapa mgao wenu utakuwa mdogo sana, hivyo kila mtu atapata milioni 3 jumla tisa. Wote tukagoma tukiamini mdosi hatutendei haki na kwanini hakutaka kuhesabu hela mbele yetu?

Mdosi alimwita jamaa mmoja yupo kimya sana akamwambia wape hizo hela kama hawataki malizana nao.

Wote tuliangaliana huku mdosi akiondoka tukaona hamna namna tukapokea na kuondoka na sisi. Kesho yake ulikuwa ni msako mkali sana wa polisi maana hela ziliibiwa nyingi sana, huku kiwango kikisemekana kuwa milioni 500 na sisi tuliambulia milioni 3 kila mmoja!

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Mara ya kwanza naingia arusha 2011,nilishangaa kuona kiatu cha 70,000 na nguo za mtumba mashati ya 15,000 niliondoka nikawa nawaza hvyo viatu wanavivaa wakina na nani

Mashati na kadeti kali nilinunua hzo nilizipenda,tena kuna kadeti kali zaidi ya zile za spesho
Ata mimi nilinunua kiatu clock on ila nilipopagundua Tengeru nikajiona boya aisee
 
Back
Top Bottom